Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka

Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka

Watu tulisema atakua na makosa ya kujibu hakuna cha kubambikiwa kesi wala nn,sema wapinzani wanapenda kutetea sana mambo kama hayo,imebaki wanasiasa wenyewe


Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuwa na kosa. Na hakuna pesa iliyolipwa. Ameelekezwa cha kufanya ili aachiwe. Hata pesa aliyoambiwa alipe, hajalipa, ameambiwa atalipa taratibu. Lakini hatalipa.

Tunafanya mambo ya aibu na fedheha kubwa mbele ya uso wa Dunia.
 
Sasa mchange alipe hizo million 200+.Ama vepe mme wangu ?
Uliwahi kusikia mtu anaachiwa huru na mahakama bila ya kulipa faini aliyohukumiwa? Hiyo imetajwa tu, hakuma hata shilingi iliyolipwa, na hakuna itakayolipwa.
 
Katika nafsi yangu siamini hayo yalosemwa,maana mwanzo waliomba kukutana naye unadhani Nini kilizungumzwa?.

Je Kama alishinikizwa akubali makosa na kuyakiri ndo apate msamaha,kea mateso aliyokwisha yapata unadhani angekataa?

Kama kweli alikuwa na makosa tokea mwanzo,kwa Nini hajahukumiwa tokea pale awali?.
Je mnadhani kwa nini Rais alitangaza msamaha mara tu baada ya watu kukaa rumande kwa mda mrefu?.(hapa walosoma logic watanisaidia).

Je mara baada ya msamaha wa Rais kwa watakao kiri makosa na kuomba msamaha,je Kabendera pia alikuwa miongoni mwao?

Mnafikiri sababu Ni zipi Hadi Luge kuendelea kukomaa lumande?.

Tujihoji haya maswali,nitarudi kwa kesho usiku.
 
Kilatha,
Tuna mwendo kweli mrefu mpaka watu wote tutakapojitambua sisi kama nchi tuko wapi. Kilatha umeandika kwa hisia tu ya upande unaouunga mkono kwenye suala hili. Licha ya hiyo hali ya kuwa ‘heavily dependent on aid’, Tanzania ni nchi huru na ina haki ya kuchagua na kufanya maamuzi yake yenyewe.

Kama nchi, vilevile ina vipaumbele vyake na maslahi yake. Maslahi ya nchi (National Interest) yanasimamiwa na kulindwa na Serikali yenye ridhaa iliyopo madarakani. Ukitaka kujua kwamba kuna nchi na Serikali yake, chezea maslahi yake kwa kisingizio kwamba ni nchi ‘heavily dependent on aid’ halafu uone kitakachokutokea!

Tatizo ukiendekeza maslahi binafsi ya kiuchumi au kisiasa, unaweza kujisahau na kudharau kuona kwamba maslahi ya nchi yanapewa kipaumbele juu ya maslahi binafsi. Madhara ya dharau hizo ni makubwa pale unapogundulika.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 duu ! Mbavu zangu mie !!! 😂😂😂😂
Usipende kusababisha au kuzidisha maumivu kwa wengine maana wote tumeumbwa na damu,tena usiombe yakukute wanayopitia hawa wakosoaji wakamatwapo/kutekwa.Wengine huomba wauliwe kabisa ili wasiendelee kuteswa kwa kutwezwa.Soma tu comments/u comment hapa JF.

Uwezekano mkubwa ni kuwa hizi kesi ni za kimkakati zaidi kufifisha fikra/mawazo mbadala ya kiuongozi.Walioshika mpini wanajihakikishia hakuna wakosoaji wakitaka kufanya yao.Fungua macho zaidi nawe utaona.
 
Hakuwa na kosa. Na hakuna pesa iliyolipwa. Ameelekezwa cha kufanya ili aachiwe. Hata pesa aliyoambiwa alipe, hajalipa, ameambiwa atalipa taratibu. Lakini hatalipa.

Tunafanya mambo ya aibu na fedheha kubwa mbele ya uso wa Dunia.
Wanafanya vituko as if watu wote duniani ni wana CCM ambao hawaruhusiwi kuhoji chochote.Tunapitisha na kutekeleza maagizo/maelekezo ya mwenyekiti na siyo ya wenyenchi.
 
Mwandishi wa habari kaachiwa. Kakaa rumande kwa kinachoelezwa na wanaharakati kuwa uhuru wake wa kujieleza. Serikali inasema ni utakatishaji wa fedha na ukwepaji kodi.

Ni vema tukajiuliza sababu kubwa ya yeye kuambiwa katakatisha fedha na kakwepa kodi. Mara nyingi serikali ikiona unaisumbua inakutafutia sababu. Inakupekenyua. Itangalia akaunti zako za benki, mali zako na mambo mengine kama yanaoana na ulivyo. Na akaunti ndio zinashtaki zaidi. Fedha za dili zinaingia, siku zinaenda, ukija kuulizwa huna la kujibu.

Ni Kabendera peke yake anayeweza kutuambia kwa ukweli kwa nini asingiziwe makosa hayo. Waliona nini mpaka wamwambie kakwepa kodi na kutakatisha fedha.

Namhurumia sana ila tujifunze pia. Nami nikiwemo kwenye kujifunza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaweza kuwa account yake ilikuwa Inatumika vibaya kwa fedha haramu
 
Jibu ni moja ukosoaji awami hii haurusiwi..mifano iko.mingi just tu afisa elimu alisema mwalimu atakae kua upinzani atapewa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Serikali (institution yenye power) ikiamua kukutafuta haikukosi..

Kuna hadithi ya swala na fisi..., fisi alimuona swala anakunywa maji akamwambia lazima nikufanye kitoweo..., swala akamjibu ni nini nimekukosea..., fisi akamwambia mwaka juzi ulinitukana..., swala akasema duh mbona mwaka juzi nilikuwa sijazaliwa..., fisi akasema anyway hata kama haukuwa wewe basi alikuwa mjomba wako....
 
Congo,
Huyu mtu ni mwandishi wa habari na habari alizokuwa anafanya alikuwa anaziuza kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Kwa hiyo alikuwa halipwi haya madafu yetu.

Kwa hiyo ukilipwa dola 3000 jua hiyo ni milioni 6,900,000 na ukute zinaingia kila week na ukute anaandikia vyombo zaidi ya viatatu je kuwa na pesa kwa kutumia jasho lako ni dhambi. Je akitumiwa pesa hizo Bank si kuna ushuru unakatwa na Bank na kuingia kwenye mfumo wa kodi, sasa ukwepaji wa kodi unatoka wapi.

Je, akitumia hela hiyo kama mwananchi serikali kila anachofanya si analipia VAT, unatakatisha pesa pesa zako zinapokuja zikiwa haramu hazijulikani source, unauza madawa au unasafirisha binadamu
 
Moja ya tuhuma dhidi ya Kabendera ni kuongoza kundi la uhalifu, mahakama imemtoza faini ili kesi ifutwe! Na arudi mtaani naye amelipa na karudi mtaani.
Sahihisho, kichwa kisomeke .......UKARUDI mtaani.
 
Angetoka bila mashariti ningekuelewa,MTU kakaa miezi saba na analipa million 274 halafu halafu unaleta nyenyeee!!!
Katoka kwa shinikizo la mabeberu kwa kuhofia kunyimwa misaada na sio kwa sababu ya huruma
 
Back
Top Bottom