Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka

Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka

Kwahiyo hata hilo genge lake la uhalifu limesamehewa? Ni akina nani wako kwenye hilo genge ambalo serikali wameshindwa kuwapata?
 
wakatanta,
Hivi mtu wa kawaida anaweza kuwa na siri za serikali? Sasa atajuaje kama ni siri wakati yeye hajaajiriwa kutunza siri hizo na hajala kiapo cha kuzitunza.
 
Angetoka bila mashariti ningekuelewa,MTU kakaa miezi saba na analipa million 274 halafu halafu unaleta nyenyeee!!!
Kaamua kununua Uhuru wake shida IPO wapi kukiri kosa sio kutenda kosa.Mbona kashtakiwa yeye pekee vipi hilo genge la wahalifu umeliona?
 
Msuluhishi,
Ngoja nikupe perspective za GDP ya marekani na U.K (wakiwa kama mabeberu wawili walio wasumbufu zaidi kwa nchi nyingi duniani); na mwisho tulinganushe na uchumi wa Tanzania

US GDP $19.39 trillion
UK GDP $2.662 trillion
Tanzania GDP $52.09 billions au $0.0521 trillion (according to WB)

In other words uchumi wa Tanzania ndio kwanza 1.96% ya uchumi wa UK au 0.3% kwa US.

Pili ili mtu kukuhujumu lazima kuwe trade au hata competition front mnayogombea trade value ya Tanzania na UK aizidi hata $500 million yaani ata miji yao midogo kama Berkshire na Swindon ukute zina trade value zaidi ya hiyo; kwa US ata tusijilinganishe kabisa.

Kuna watu humu wanaweza ona Magu anakopa sana; la hasha sio kwamba waliomtangulia walikuwa awataki isipokuwa walikuwa awapewi wanapoomba kwa sababu impact ya hela ilikuwa aionekani.

Walau huyu wanampa na kinachofanyika it’s in their interest uwezi kwenda kuwekeza heavily nchi ambayo aina infrastructure especially za usafiri na nishati ya uhakika.

Unaponyimwa mkopo na IMF/WD ni kwa sababu hata wao wanatakiwa kuzingatia risk model hili kuzuia mambo ya kukopesha watu kushinda uwezo wao wa kulipa; kumbuka deni letu leo dogo kwa sababu moja wapo Mkapa alifutiwa karibu lote maana nchi ilikuwa aina uwezo wa kulipa kulazimisha ilikuwa kuturudisha kipindi cha miaka ya mwisho ya JKN.

So unaponyimwa they do that with specific reasons behind maana hizo hela pia nyuma zina lenders wengine na wenyewe WD/IMF wanazi channel tu.

Misaada ya direct kutoka nchi mabeberu inakuja na condition za Democratic au social/moral values zao na ni sahihi kabisa kama nchi kukataa mengine hili kulinda tamaduni zetu; lakini wakikunyima pia usilie kwa sababu ya masharti hayo hayo unayokataa that is what freedom of choice.

Lakini kusema kuna mtu anataka kutuhujumu kiuchumi ni kujifurahisha sio US wala UK; na allies wao wote kutuhujumu nchi kama Tanzania kwa kweli ata huko kwenye vikao vya UN nchi nyingi zingesema sio sawa mnavyowafanyia nchi maskini kama ile.

Ukisema sijui madini; apparently utakuwa ujasikia Mongolia kuna nini chini ya ardhi huko ndio kwenye interest maana wanapeleka na assembly plant ya caterpillar kabisa wakachimbe vizuri.
 
Cherenganya,
Chifu, hakuna aliyeonesha vyeti hapa. Umeniambia hapo juu kuwa sikuwa na akili hivyo nisingeweza kusoma hiyo Sheria. Nami nimekujibu si kuwa sikuwa na akili kama ambavyo umefikiri au nilikosa vigezo bali ni kwamba nilipita njia nyingine si kwa kukosa akili bali Sheria haikuwa kipaumbele kwangu.
 
Na. Habibu Mchange

Nitafurahi sana kama ndugu Zitto atapingana na ukweli huu rahisi kuhusu Kabendera

Inasikitisha sana kuona baada ya Erick Kabendera kukiri mwenyewe kutenda makosa katika mashtaka ya utakatishaji fedha na kukwepa kodi na kukubali kulipa fidia ya jumla ya milioni 100,250,000, kama kianzio na kisha kulipa wastani wa milioni 29 kila mwezi kukamilisha makubaliano ya kisheria aliyosaini.

Tumemshuhudia kwa kasi kubwa mwanasiasa anayeelekea kuwa uchwara na mchumia tumbo lake ambaye amejivika utetezi wa kila jinai hapa nchini na kuivisha usiasa Ndugu Zitto Kabwe akiandika mitandaoni kuwa Kabendera amenunua uhuru wake.

Zitto anadai bila aibu wala haya kuwa Kabendera amelipia kuipata haki yake ya kuwa huru huku akijua wazi kuwa Mahakama za Tanzania hazijawahi hata siku moja kuuza uhuru wala kutaraji kuuza haki ya mtu

Mimi nafahamu kuwa kwa kiasi fulani Zitto alikuwa na uswahiba na Kabendera, ninafahamu pia uswahiba wake na Kabendera aliuzidisha chumvi mara tu Kabendera kuingia kwenye matatizo ya uvunjaji wa sheria za nchi.

Nafahamu bila chembe ya aibu wala shaka, kuwa Zitto amechagua makusudi kupotosha ukweli ili apate huruma yake ya kisiasa na aendelee kuungwa mkono kama mtetezi wa wanyonge ama mkosoaji mkuu wa uongozi wa Rais Magufuli

KILICHOMPONZA KABENDERA HIKI HAPA

panapotokea wapotoshaji wa makusudi kama Zitto kabwe na wenzake, wakaamua makusudi kupotosha ukweli huku wakijua kufanya hivyo si sawa kwa MASLAHI ya umma. Ni vyema sisi wengine tukajaribu kuusaka ukweli na kuusema kama ulivyo.

Mimi kama mdau wa habari, nimebahatika Kuisoma hati ya Taarifa sahihi inayomuhusu Kabendera katika shauri lake, hati ambayo imesainiwa na kuthibitishwa na Kabendera mwenyewe.

Kwa taarifa tu ya watu wema wanaipenda nchi hii, ndugu Erick Kabendera amekiri kufanya makosa yote aliyotenda ambayo ni wazi kabisa amejua asingeweza kuchomoka na hivyo kuchagua kutumia sheria ya usuluhishi wa makosa.

Zitto anafahamu wazi kwamba Kabendera katika kuhakikisha anatekeleza uhalifu wa kutakatisha fedha alisajili kampuni mbili ambazo hazikuwa hata na ofisi na katika usajili akadanganya ofisi zipo eneo ambalo kumbe ni nyumbani kwake.

Zitto na wenzake wanafahamu wazi kuwa Machi 23 2010. Kabebdera alisajili kampuni ya Voxy Media Centre Ltd na akapewa cheti cha usajili No. 75572 kutoka BRELA lakini mbaya zaidi alitumia anuani ya posta ya mtu binafsi ambaye ni miongoni mwa genge lake la uhalifu ambayo ni P.O. Box 7439 na kueleza kuwa ndiyo anuani ya kampuni yake.

Zittto anafahamu kuwa Januari 11, 2016, Kabendera na mke wake Loy Philip Kabendera walifungua tena kampuni ya PR ijulikanayo kama Sitrep Co. Ltd yenye cheti cha usajili kutoka BRELA No. 122885.

Katika usajili wa kampuni hiyo Kabendera amekiri kuwa walighushi fomu mbalimbali na kudanganya kuwa ofisi zipo Block No. 13 Plot 23 Mbweni Mpiji ambapo baada yabuchunguzi ikabainika eneo hilo ni nyumbani kwake. Alitumia taarifa hizo za uongo kuomba leseni ya kufanya biashara ya PR na akapatiwa leseni No. 2209221.

Zitto anafahamu kuwa baada ya kukamilisha mchakato wa kufungua kampuni, kabendera na mkewe na wenzake wakaanza kufungua akaunti nyingi za benki nyingine kwaajili ya Dola za Marekani na nyingine ya Pauni na akaunti binafsi na baada ya hapo akaanza kuingiziwa fedha kutoka nje na ndani ya nchi.

Zitto asijitoe ufahamu na ajue kwamba, watanzania tunajua kuwa Aprili 2, 2016 kabendera na mkewe walifungua akaunti No. 0250440251400 kwajili ya kuingiza USD(Dolla za kimarekani) na nyingine No. 0350440251400 kwaajili ya Paundi za Uingereza katika benki ya CRDB tawi la

Zitto anafahamu kuwa Kabendera alifungua akaunti binafsi kwaajili ya Dola za Marekani yenye No. 0250275464500 na nyingine No. 01J2013248400 CRDB tawi la Kijitonyama.

Zitto na MAKUWADI wengine wa MABEBERU wanajua kuwa baada ya hapo mamilioni ya Shilingi, dola la Paundi yalianza kuingia kwenye hizo akaunti huku zingine zikihamishwa kutoka akaunti za kampuni kwenda akaunti binafsi na kutoka kampuni moja kwenda nyingine.

Zitto anajua kuwa kati ya tarehe 1 Januari 2015 na tarehe 29 Julai 2019 Kabendera alipokea fedha za kimarekani USD 230,358.83 sawa na zaidi ya milioni 534 za kitanzania kwenye akaunti yake binafsi ambazo zilitoka kampuni mbalimbali za nje na ndani zikiwemo K2 Intelligence Ltd, Palladium (Tanzania) Ltd, Eurasia Group Ltd, International Crisis Rou na zingine nyingi za nje.

Zitto anafahamu kuwa Kati ya Januari mosi 2015 na Agosti 29, 2019 Kabendera na mke wakiwa wanahisa na wakurugenzi wa Sitrep Co. Ltd walipokea Dola za Marekani 432,000,541.64 sawa na shilingi bilioni Shilingi bilioni 1.01 za kitanzania.

Zitto kabwe anafahamu kuwa Kabendera pia katika wakati huo huo aliingiziwa kiasi cha Paundi za Uingereza 119,000,130.84. Sawa na zaidi ya shilingi milioni 305 za kitanzania.

Zitto kabwe anafahamu kuwa pamoja na kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka ndani na nje ya nchi, Kabendera alikiri kuwa hakuwahi kufaili 'Tax returns' .

Zitto anafahamu kuwa Kabendera mwenyewe amekiri kuwa yeye na mkewe kati ya Julai 29 na Julai 9, 2019 walihamisha Dola 25,303 kutoka Sitrep Co. Ltd kwenda akaunti binafsi ya Kabendera na katika kipindi hicho chote alilipa kodi ya Sh 1,376,400 tu na kukwepa kulipa kodi ya Sh 173,249,047.

Zitto na MAKUWADI wengine wa MABEBERU, wanafahamu kuwa Kabendera amekiri kutenda makosa hayo yote na kusaini makubaliano na Ofisi ya Mashtaka na kukubali kulipa fidia ambapo amelipa Sh milioni 100 kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na Sh 250,000 kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

USHAURI KWA KABENDERA

Ninakushauri ndugu Erick Kabendera, usimuendekeze Zitto kabwe atakupoteza, Zitto kabwe ni mwanasiasa ambaye yupo tayari kusema, kufanya, kuongea, kuongopa lolote kwa sasa ili tu apate sifa ya kisiasa.

Kwa tuhuma kama hizi ulizozikiri mwenyewe, kutokea mwanasiasa kama Zitto kuropoka ropoka mitandaoni inatufanya sisi tunaofuatilia nyendo hizi tuone kuna walakini katika mahusiano yenu.

Ninaishia hapa kwa leo, nikisema KABENDERA MKANYE ZITTO ATAKUHARIBIA ZAIDI.
 
Sasa ndugu yetu mbona kama nawe unakengeuka kutokana na kutangaza kile Kabendera na nyinyi mlikubaliana sasa unautangazia umma ili iweje?

Huoni kama humtendei haki mteja wenu?

In God we Trust
 
Tayari mleta mada either kwa kujua au kutojua tayari kesha mvunjia haki Kabendera kwa kuanika siri zake
Tatizo langu ni kale kakipengele ka CONFIDENTIALITY maana hapo uwezi pata undani wa majadiliano kati ya Kabendera na DPP naishia hapo. tutaona hitimisho kwa ajili ya PRESS RELEASE.

In God we Trust
 
Siasa za Tanzanian
Movie linaendelea na linaelekea patamu sasa pale mda wa watazamaji kupandwa na midadi.
 
Panapotokea wapotoshaji wa makusudi kama Zitto kabwe na wenzake, wakaamua makusudi kupotosha ukweli huku wakijua kufanya hivyo si sawa kwa MASLAHI ya umma. Ni vyema sisi wengine tukajaribu kuusaka ukweli na kuusema kama ulivyo. Mimi kama mdau wa habari, nimebahatika Kuisoma hati ya Taarifa sahihi inayomuhusu Kabendera katika shauri lake, hati ambayo imesainiwa na kuthibitishwa na Kabendera mwenyewe.

Kwa taarifa tu ya watu wema wanaipenda nchi hii, ndugu Erick Kabendera amekiri kufanya makosa yote aliyotenda ambayo ni wazi kabisa amejua asingeweza kuchomoka na hivyo kuchagua kutumia sheria ya usuluhishi wa makosa. Zitto anafahamu wazi kwamba Kabendera katika kuhakikisha anatekeleza uhalifu wa kutakatisha fedha alisajili kampuni mbili ambazo hazikuwa hata na ofisi na katika usajili akadanganya ofisi zipo eneo ambalo kumbe ni nyumbani kwake. Zitto na wenzake wanafahamu wazi kuwa Machi 23 2010. Kabebdera alisajili kampuni ya Voxy Media Centre Ltd na akapewa cheti cha usajili No. 75572 kutoka BRELA lakini mbaya zaidi alitumia anuani ya posta ya mtu binafsi ambaye ni miongoni mwa genge lake la uhalifu ambayo ni P.O. Box 7439 na kueleza kuwa ndiyo anuani ya kampuni yake.

Zittto anafahamu kuwa Januari 11, 2016, Kabendera na mke wake Loy Philip Kabendera walifungua tena kampuni ya PR ijulikanayo kama Sitrep Co. Ltd yenye cheti cha usajili kutoka BRELA No. 122885. Katika usajili wa kampuni hiyo Kabendera amekiri kuwa walighushi fomu mbalimbali na kudanganya kuwa ofisi zipo Block No. 13 Plot 23 Mbweni Mpiji ambapo baada yabuchunguzi ikabainika eneo hilo ni nyumbani kwake. Alitumia taarifa hizo za uongo kuomba leseni ya kufanya biashara ya PR na akapatiwa leseni No. 2209221.

Zitto anafahamu kuwa baada ya kukamilisha mchakato wa kufungua kampuni, kabendera na mkewe na wenzake wakaanza kufungua akaunti nyingi za benki nyingine kwaajili ya Dola za Marekani na nyingine ya Pauni na akaunti binafsi na baada ya hapo akaanza kuingiziwa fedha kutoka nje na ndani ya nchi. Zitto asijitoe ufahamu na ajue kwamba, watanzania tunajua kuwa Aprili 2, 2016 kabendera na mkewe walifungua akaunti No. 0250440251400 kwajili ya kuingiza USD(Dolla za kimarekani) na nyingine No. 0350440251400 kwaajili ya Paundi za Uingereza katika benki ya CRDB.

Zitto anafahamu kuwa Kabendera alifungua akaunti binafsi kwaajili ya Dola za Marekani yenye No. 0250275464500 na nyingine No. 01J2013248400 CRDB tawi la Kijitonyama. Zitto na MAKUWADI wengine wa MABEBERU wanajua kuwa baada ya hapo mamilioni ya Shilingi, dola la Paundi yalianza kuingia kwenye hizo akaunti huku zingine zikihamishwa kutoka akaunti za kampuni kwenda akaunti binafsi na kutoka kampuni moja kwenda nyingine. Zitto anajua kuwa kati ya tarehe 1 Januari 2015 na tarehe 29 Julai 2019 Kabendera alipokea fedha za kimarekani USD 230,358.83 sawa na zaidi ya milioni 534 za kitanzania kwenye akaunti yake binafsi ambazo zilitoka kampuni mbalimbali za nje na ndani zikiwemo K2 Intelligence Ltd, Palladium (Tanzania) Ltd, Eurasia Group Ltd, International Crisis Rou na zingine nyingi za nje.

Zitto anafahamu kuwa Kati ya Januari mosi 2015 na Agosti 29, 2019 Kabendera na mke wakiwa wanahisa na wakurugenzi wa Sitrep Co. Ltd walipokea Dola za Marekani 432,000,541.64 sawa na shilingi bilioni Shilingi bilioni 1.01 za kitanzania. Zitto kabwe anafahamu kuwa Kabendera pia katika wakati huo huo aliingiziwa kiasi cha Paundi za Uingereza 119,000,130.84. Sawa na zaidi ya shilingi milioni 305 za kitanzania.

Zitto kabwe anafahamu kuwa pamoja na kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka ndani na nje ya nchi, Kabendera alikiri kuwa hakuwahi kufaili 'Tax returns' . Zitto anafahamu kuwa Kabendera mwenyewe amekiri kuwa yeye na mkewe kati ya Julai 29 na Julai 9, 2019 walihamisha Dola 25,303 kutoka Sitrep Co. Ltd kwenda akaunti binafsi ya Kabendera na katika kipindi hicho chote alilipa kodi ya Sh 1,376,400 tu na kukwepa kulipa kodi ya Sh 173,249,047. Zitto na MAKUWADI wengine wa MABEBERU, wanafahamu kuwa Kabendera amekiri kutenda makosa hayo yote na kusaini makubaliano na Ofisi ya Mashtaka na kukubali kulipa fidia ambapo amelipa Sh milioni 100 kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na Sh 250,000 kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

USHAURI KWA KABENDERA
Ninakushauri Ndugu Erick Kabendera, usimuendekeze Zitto kabwe atakupoteza, Zitto kabwe ni mwanasiasa ambaye yupo tayari kusema, kufanya, kuongea, kuongopa lolote kwa sasa ili tu apate sifa ya kisiasa. Kwa tuhuma kama hizi ulizozikiri mwenyewe, kutokea mwanasiasa kama Zitto kuropoka ropoka mitandaoni inatufanya sisi tunaofuatilia nyendo hizi tuone kuna walakini katika mahusiano yenu. Ninaishia hapa kwa leo, nikisema KABENDERA MKANYE ZITTO ATAKUHARIBIA ZAIDI.
 
Back
Top Bottom