Panapotokea wapotoshaji wa makusudi kama Zitto kabwe na wenzake, wakaamua makusudi kupotosha ukweli huku wakijua kufanya hivyo si sawa kwa MASLAHI ya umma. Ni vyema sisi wengine tukajaribu kuusaka ukweli na kuusema kama ulivyo. Mimi kama mdau wa habari, nimebahatika Kuisoma hati ya Taarifa sahihi inayomuhusu Kabendera katika shauri lake, hati ambayo imesainiwa na kuthibitishwa na Kabendera mwenyewe.
Kwa taarifa tu ya watu wema wanaipenda nchi hii, ndugu Erick Kabendera amekiri kufanya makosa yote aliyotenda ambayo ni wazi kabisa amejua asingeweza kuchomoka na hivyo kuchagua kutumia sheria ya usuluhishi wa makosa. Zitto anafahamu wazi kwamba Kabendera katika kuhakikisha anatekeleza uhalifu wa kutakatisha fedha alisajili kampuni mbili ambazo hazikuwa hata na ofisi na katika usajili akadanganya ofisi zipo eneo ambalo kumbe ni nyumbani kwake. Zitto na wenzake wanafahamu wazi kuwa Machi 23 2010. Kabebdera alisajili kampuni ya Voxy Media Centre Ltd na akapewa cheti cha usajili No. 75572 kutoka BRELA lakini mbaya zaidi alitumia anuani ya posta ya mtu binafsi ambaye ni miongoni mwa genge lake la uhalifu ambayo ni P.O. Box 7439 na kueleza kuwa ndiyo anuani ya kampuni yake.
Zittto anafahamu kuwa Januari 11, 2016, Kabendera na mke wake Loy Philip Kabendera walifungua tena kampuni ya PR ijulikanayo kama Sitrep Co. Ltd yenye cheti cha usajili kutoka BRELA No. 122885. Katika usajili wa kampuni hiyo Kabendera amekiri kuwa walighushi fomu mbalimbali na kudanganya kuwa ofisi zipo Block No. 13 Plot 23 Mbweni Mpiji ambapo baada yabuchunguzi ikabainika eneo hilo ni nyumbani kwake. Alitumia taarifa hizo za uongo kuomba leseni ya kufanya biashara ya PR na akapatiwa leseni No. 2209221.
Zitto anafahamu kuwa baada ya kukamilisha mchakato wa kufungua kampuni, kabendera na mkewe na wenzake wakaanza kufungua akaunti nyingi za benki nyingine kwaajili ya Dola za Marekani na nyingine ya Pauni na akaunti binafsi na baada ya hapo akaanza kuingiziwa fedha kutoka nje na ndani ya nchi. Zitto asijitoe ufahamu na ajue kwamba, watanzania tunajua kuwa Aprili 2, 2016 kabendera na mkewe walifungua akaunti No. 0250440251400 kwajili ya kuingiza USD(Dolla za kimarekani) na nyingine No. 0350440251400 kwaajili ya Paundi za Uingereza katika benki ya CRDB.
Zitto anafahamu kuwa Kabendera alifungua akaunti binafsi kwaajili ya Dola za Marekani yenye No. 0250275464500 na nyingine No. 01J2013248400 CRDB tawi la Kijitonyama. Zitto na MAKUWADI wengine wa MABEBERU wanajua kuwa baada ya hapo mamilioni ya Shilingi, dola la Paundi yalianza kuingia kwenye hizo akaunti huku zingine zikihamishwa kutoka akaunti za kampuni kwenda akaunti binafsi na kutoka kampuni moja kwenda nyingine. Zitto anajua kuwa kati ya tarehe 1 Januari 2015 na tarehe 29 Julai 2019 Kabendera alipokea fedha za kimarekani USD 230,358.83 sawa na zaidi ya milioni 534 za kitanzania kwenye akaunti yake binafsi ambazo zilitoka kampuni mbalimbali za nje na ndani zikiwemo K2 Intelligence Ltd, Palladium (Tanzania) Ltd, Eurasia Group Ltd, International Crisis Rou na zingine nyingi za nje.
Zitto anafahamu kuwa Kati ya Januari mosi 2015 na Agosti 29, 2019 Kabendera na mke wakiwa wanahisa na wakurugenzi wa Sitrep Co. Ltd walipokea Dola za Marekani 432,000,541.64 sawa na shilingi bilioni Shilingi bilioni 1.01 za kitanzania. Zitto kabwe anafahamu kuwa Kabendera pia katika wakati huo huo aliingiziwa kiasi cha Paundi za Uingereza 119,000,130.84. Sawa na zaidi ya shilingi milioni 305 za kitanzania.
Zitto kabwe anafahamu kuwa pamoja na kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka ndani na nje ya nchi, Kabendera alikiri kuwa hakuwahi kufaili 'Tax returns' . Zitto anafahamu kuwa Kabendera mwenyewe amekiri kuwa yeye na mkewe kati ya Julai 29 na Julai 9, 2019 walihamisha Dola 25,303 kutoka Sitrep Co. Ltd kwenda akaunti binafsi ya Kabendera na katika kipindi hicho chote alilipa kodi ya Sh 1,376,400 tu na kukwepa kulipa kodi ya Sh 173,249,047. Zitto na MAKUWADI wengine wa MABEBERU, wanafahamu kuwa Kabendera amekiri kutenda makosa hayo yote na kusaini makubaliano na Ofisi ya Mashtaka na kukubali kulipa fidia ambapo amelipa Sh milioni 100 kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na Sh 250,000 kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.
USHAURI KWA KABENDERA
Ninakushauri Ndugu Erick Kabendera, usimuendekeze Zitto kabwe atakupoteza, Zitto kabwe ni mwanasiasa ambaye yupo tayari kusema, kufanya, kuongea, kuongopa lolote kwa sasa ili tu apate sifa ya kisiasa. Kwa tuhuma kama hizi ulizozikiri mwenyewe, kutokea mwanasiasa kama Zitto kuropoka ropoka mitandaoni inatufanya sisi tunaofuatilia nyendo hizi tuone kuna walakini katika mahusiano yenu. Ninaishia hapa kwa leo, nikisema KABENDERA MKANYE ZITTO ATAKUHARIBIA ZAIDI.