Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019

Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019

Voda ana kadiriwa kua na wateja 19M nchi nzima
Endapo wateja 1,000,000 tu wata nunua vocha za jero (500) kwa siku 7 tu ako kapesa kana lipwa kwa M pesa ya kabenda chap

1M × 500 × 7
= 3,500,000,000
Voda inawalindaje wateja 19m?
 
IMG-20240426-WA0072.jpg


Anaomba fidia ya USD 1.0 Million sawa na TSH 2.5 Billion. Soma bandiko hapo juu ambalo VODACOM walilipokea jana 25/ 04/ 2025 kutoka kwa Wanasheria wa Eric Kabendera
 
Dola milioni moja inaandikwa
Usd 1m ( usd 1millmion ) sasa huyu amesema dola milioni 1. Halafu akaandika usd 1000,000 milioni. Yaani milioni ziwe milioni duuuu .
 
Mzaa mzaaa kabenderaa anaenda kulamba mabilion kama kina Mana FA..
Watu wanadhani mzaha......ukisikia ukitazama ile kesi ya Ugaidi ya Mbowe ndio utajua Mitandao ya simu inatakiwa kuwa na Ulinzi imara kwa wateja wake.
Tuliona wale ma Eng na Lawyers wa Tigo walivyopata taabu kujibu maswali ya Mawakili na Jaji.
 
Mwandishi wa Habari, ERICK KABENDERA ameitaka Kampuni ya Simu ya VODACOM TANZANIA kumlipa USD 1,000,000 MILIONI ndani ya SIKU 14 kwa Kufanikisha kutekwa kwake mwaka 2019.

Amefanya hivyo kupitia kwa WAKILI wake Peter Madeleka.

View attachment 2974231

Kabendera siyo mjinga.Huwa namtafsiri kama miongoni wandishi wa habari wachache sana ambao ni smart sana hapa bongo.toka 2019 mpaka leo ni muda umepita,nadhani kuna ushahidi alikuwa anakusanya.Ila pia alipitia mateso makubwa sana na ile kesi yake ya uhujumu uchumi.Kwamba alikuwa na hatia au la,hilo tunawaachia vyombo husika!
 
Mwandishi wa Habari, ERICK KABENDERA ameitaka Kampuni ya Simu ya VODACOM TANZANIA kumlipa USD 1,000,000 MILIONI ndani ya SIKU 14 kwa Kufanikisha kutekwa kwake mwaka 2019.

Amefanya hivyo kupitia kwa WAKILI wake Peter Madeleka.

View attachment 2974231
Naomba uweke yote iliyokamilika ili na sisi tuchambue ana kesi au anajisumbusla
 
Labda kama angeweza kufungua hiyo kesi kwenye mahakama ya kimataifa. Lakini hakuna uwezekano wowote wa yeye kupata haki kwa kosa lililofanywa kwa maagizo ya rais. Hapa kwetu rais ni Mungu, hata katiba imempa kinga ya kufanya uhalifu.
 
Back
Top Bottom