Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji

Kama Kabendera alikuwa amenunuliwa na watu wa nje na serikali ilikuwa na uthibitisho huo ingemnunua tu au kumlipa zaidi aungane na kina Musiba kuisema vizuri, hii ilikuwa njia rahisi zaidi na safi ya kudili naye.
 
Yupi yule baniani
 
Hawakuwa wanaandika kuuza wapate fedha, walikuwa wanaandika na lengo la kusaidia.
Ndio maana nimemtofautisha Kabendera na Mhaya mwenzake aliyeandika kupinga deal la Ngorongoro kati ya serikali ya Mwinyi na Waarabu.

Hata na sisi tunao waandishi waliopinga bwawa la umeme kwenye makala zao. Haimaanishi kila mwandishi aliyepinga alikamatwa. Marekani waliopinga msaada kwa Israel na Ukraine hawana kesi, Snowden aliyetoa siri za surveillance ana kesi.
 
Waandishi wa habari, makala au analysts wa vyombo vikubwa vya habari duniani wanalipwa pesa nzuri tu, pesa anayolipwa mtu anayeandikia The Economist au The Times haiwezi kuwa ndogo hasa ukizingatia anatoka Tanzania ambapo waandishi wa calibre yake ni wa kutafuta kwa tochi nchini. Sasa Kabendera aliyekuwa anaandikia magazeti mengi makubwa ya kimataifa kwa nini asiwe na pesa nzuri hadi ufikirie kanunuliwa?!
 
Inawezekana ni moja ya mbinu kati ya nyingi kumchafua hayati JPM na kufifisha legacy yake; kwenye malumbano kusifiana hakupo, kuchafuana ndio mtindo.
Kibaya zaidi, hayati JPM alishanyamaza; hawezi tena kujitetea kwa lolote litakalosemwa dhidi yake na wapinzani wake.
Bado utumishi uliotkuka wa hayati JPM utaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi ijayo tangu akiwa Mbunge, Naibu Waziri, Waziri hatimae Rais.
Kipindi cha chini ya miaka kumi JPM kuwa Rais, alifanikiwa kusukuma mambo mengi makubwa ambayo kwa awamu zilizomtangulia hayakuwa kufanyika; yanajulikana, sina haja ya kuyataja.
Najua JPM alikuwa mwanadamu kama mimi na wewe, alikuwa na mapungufu yake kama ambavyo watangulizi wake walikuwepo nayo na watakaofuata pia watakuwa nayo.
Msameheni pale alipowakosea, kama mimi na wewe tunavyosamehewa na wenzetu tuliowakosea sana; tusimhukumu, nasi tusije tukahukumiwa.
Mungu ampe pumziko la amani hayati JPM; Amin.
 

Sio kweli mbele ya mwenyezi Mungu. Ukweli ni kuwa yeye aliwekwa kifungoni wakati wa utawala wa JPM

Operations za Kibiti zilikuwa mbali na haya anayoyasema. Pia atuambie nani alikuwa nyuma ya waliokuwa wanaua wana usalama na kuteka ili waanzishe dola yao kule kibiti maana inaelekea anafahamu mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…