Mkuu, samahani hivi kuna ushahidi gani kuwa Mo Dewji alitekwa na serikali? Maana mwenyewe alikuwa akihojiwa BBC akadai ni watu wa nje ya nchi.. Na Magufuli alisikika akimkosoa Mambosasa kuhusu maelezo ya polisi waliyokuwa wakitoa
Naomba kama utakua na chanzo plz, maana na mimi natafuta sana ukweli wa hili swala
Ni vigumu kupata ushahidi wa moja kwa moja kwa sababu watekaji wa serikali hawaachi risiti yenye sahihi na alama za vidole kusema "Sisi ni watekaji wa serikali, majina yetu ni haya, tumetoka ofisi fulani, barua za utekaji tulizopewa ni hizi hapa".
Na hata kesi ya Mo Dewji haina ushahidi wa moja kwa moja kuwa alitekwa na serikali.
Ninachosema ni kwamba, nilivyoambiwa Dewji alitekwa na serikali ilikuwa vigumu sana kuamini habari hiyo. Ilionekana kitu cha ajabu sana. Bado kidogo nigombane na mtu kwa sababu niliona ananiletea habari za "conspiracy theories" tupu ambazo hazina ushahidi wala chembe ya kuweza kuaminika.
Kadiri muda ulivyokwenda, utekaji ukawa kitu cha kawaida, serikali haikemei, watu wanatekwa na kupita sehemu nyingi zenye roadblocks za serikali, watu wanauawa baada ya kutekwa na watu wanaotumia gari zinazojulikana ni za serikali na rais anasema "kifo ni kifo tu", baadaye ndiyo nikichambua mambo naona kuwa kumbe hata nilivyopinga kuwa serikali haiwezi kuteka sakata la Mo Dewji, kuwa zile habari ni "conspiracy theories" tu, hazikuwa that implausible, hazikuwa za ajabu kama nilivyofikiri. Nilipinga kwa kwenda na uzoefu wangu tu kuwa huko nyuma habari kama zile zilikuwa nadra sana kuzisikia.
Magufuli kumkosoa Mambosasa na stories za watu wa nje inawezekana ni hadaa za kuwachanganya watu tu. Au inawezekana ni kweli serikali haijahusika.
Ninachosema si kwamba serikali imehusika. Ninachosema ni kwamba, habari ya kuwa serikali imehusika, ambayo hapo awali niliiona kuwa haiwezekani kabisa, ni conspiracy theory tu, baada ya utekaji kuwa kama fashion, haionekani kuwa haiaminiki kabisa kama nilivyoona mwanzo.
Tutafute ushahidi zaidi. Hawa walinzi wa Ikulu inawezekana kuna siku watafunguka. Kuna watu wanagoja mpaka wakikaribia kufa ndiyo wanatoa siri zao, kwa sasa bado wapo wapo tu.