Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji

Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji

Ni vigumu kuaminika, ni vigumu kuthibitishika.

Lakini wanasema Magufuli alikuwa na faili Mirembe.

Kuna mambo mengi kafanya yalikuwa magumu kuaminika.

Alivyotekwa Mo Dewji nilipata tatizo sana kuamini kuwa utekaji ule unaweza kuwa na mkono wa serikali. Niliona si rahisi serikali kifanya utekaji hivyo. Sikuziea utamaduni wa serikali kuteka watu kwa wazi hivyo.

Lakini, baadaye imejulikana kwa ushahidi wa kuridhisha kwa kiasi kwamba serikali imehusika sana kwenye utekaji.

Mara nyingine hatutaki kukubali kuwa vitu fulani ambavyo sisi tunaviona vibaya sana vinaweza kutokea.

Ukweli ni kwamba, ni vigumu kuhakikisha Magufuli aliua au hakuua. Kama kaua kweli, wanaojua na kuweza kuaminika (mfano walinzi wa ndani wa Ikulu) hawawezi kukubali kwa sasa. Labda baadaye.

Mawazo ya watu hayataki kukubali ukweli wa kwamba "hapa hatuna jibu la uhakika, tusubiri tuchunguze tupate jibu la uhakika".

Karibu mara zote yanataka kuchukua upande na kuuamini bila ushahidi wa kutisha.
Mkuu, samahani hivi kuna ushahidi gani kuwa Mo Dewji alitekwa na serikali? Maana mwenyewe alikuwa akihojiwa BBC akadai ni watu wa nje ya nchi.. Na Magufuli alisikika akimkosoa Mambosasa kuhusu maelezo ya polisi waliyokuwa wakitoa
Naomba kama utakua na chanzo plz, maana na mimi natafuta sana ukweli wa hili swala
 
Umeandika maelezo marefu.

Na mimi nakuuliza hoja yako ni nini kwenye maelezo yote haya?
Hoja ninkwamba hiyo ni picha ya kweli ya Magufuli na picha yoyote halali ya Magufuli ni halali kuitumia kwenye cover la kitabu cha Magufuli.

Malalamiko yangekuwa na point kama picha ingekuwa si ya kweli ni ya kutengenezwa.

Sasa ukiikataa picha hii kutumika kwenye cover la kitabu unakataa nini?

Picha si ya Magufuli?

Magufuli hakuwa na bastola?
 
Za chini chini zinasema huyo kijana alipigwa risasi na vijana wa aliyekuwa mkuu wa mkoa pendwa enzi za magufuli, kisha mwili wake ukatumbukizwa kwenye pipa la sulfuric acid na kuyeyuka wote na hiyo haikuwa amri ya magufuli, na wala hakuwa mbaya kama watu wanavyotaka kutuaminisha mbaya wa nchi anajulikana ila watu wanajitoa ufahamu tu
 
Kuna bwana mmoja alikuwa anauza madawa ya kulevya..amefariki juz hapa alikuwa gerezani(miaka 30)..mtu WA tanga..
Siku amekamatwa akasafirishwa mpaka state...mzee akamuona ..akamuuliza kumbe wewe ndio desh desh Yanga!!?..Kisha akasema nilikuwa nataka nikuone...Kisha akawaambia walio mleta.."Nendeni mkashughulike nae"....
Mzee alikuwa mkali lakini sio kufikia hatua ya kuua kwa bastola yake""..I stand to be corrected.
LIKUD
 
Hoja ninkwamba hiyo ni picha ya kweli ya Magufuli na picha yoyote halali ya Magufuli ni halali kuitumia kwenye cover la kitabu cha Magufuli.

Malalamiko yangekuwa na point kama picha ingekuwa si ya kweli ni ya kutengenezwa.

Sasa ukiikataa picha hii kutumika kwenye cover la kitabu unakataa nini?

Picha si ya Magufuli?

Magufuli hakuwa na bastola?
Hiyo picha imewekwa hapo kujaribu kutetea hoja ya uongo ya mauaji ya Ben ndani ya ikulu.
 
Hoja ninkwamba hiyo ni picha ya kweli ya Magufuli na picha yoyote halali ya Magufuli ni halali kuitumia kwenye cover la kitabu cha Magufuli.

Malalamiko yangekuwa na point kama picha ingekuwa si ya kweli ni ya kutengenezwa.

Sasa ukiikataa picha hii kutumika kwenye cover la kitabu unakataa nini?

Picha si ya Magufuli?

Magufuli hakuwa na bastola?
Wapi nimekataa picha isitumike?
 
Huwa napata shida na maelezo ya Kabendera.

Kulikuwa na haja gani ya kumleta nyumbani kwake (IKULU ) kumuulia pale ?

Sio El Chapo, wala Mobutu Sese Seko, wala Al Capone the Mafia boss, ambae aliwahi kumleta mbaya wake sebuleni kwa mkewe na watoto, amshutie hapo.

Kuna ma torture chamber na majela ya kijeshi huko ndio madikteta ambao wanataka kuwahoji ma critics wao na kuwa shuti wao personally kama kina Saddam Hussein huwa wanakutana nao huko. Sio kwenye dining table ya mkewe.
 
Kuna bwana mmoja alikuwa anauza madawa ya kulevya..amefariki juz hapa alikuwa gerezani(miaka 30)..mtu WA tanga..
Siku amekamatwa akasafirishwa mpaka state...mzee akamuona ..akamuuliza kumbe wewe ndio desh desh Yanga!!?..Kisha akasema nilikuwa nataka nikuone...Kisha akawaambia walio mleta.."Nendeni mkashughulike nae"....
Mzee alikuwa mkali lakini sio kufikia hatua ya kuua kwa bastola yake""..I stand to be corrected.
Yanga Omary amefariki?
 
Mkuu, samahani hivi kuna ushahidi gani kuwa Mo Dewji alitekwa na serikali? Maana mwenyewe alikuwa akihojiwa BBC akadai ni watu wa nje ya nchi.. Na Magufuli alisikika akimkosoa Mambosasa kuhusu maelezo ya polisi waliyokuwa wakitoa
Naomba kama utakua na chanzo plz, maana na mimi natafuta sana ukweli wa hili swala
Ni vigumu kupata ushahidi wa moja kwa moja kwa sababu watekaji wa serikali hawaachi risiti yenye sahihi na alama za vidole kusema "Sisi ni watekaji wa serikali, majina yetu ni haya, tumetoka ofisi fulani, barua za utekaji tulizopewa ni hizi hapa".

Na hata kesi ya Mo Dewji haina ushahidi wa moja kwa moja kuwa alitekwa na serikali.

Ninachosema ni kwamba, nilivyoambiwa Dewji alitekwa na serikali ilikuwa vigumu sana kuamini habari hiyo. Ilionekana kitu cha ajabu sana. Bado kidogo nigombane na mtu kwa sababu niliona ananiletea habari za "conspiracy theories" tupu ambazo hazina ushahidi wala chembe ya kuweza kuaminika.

Kadiri muda ulivyokwenda, utekaji ukawa kitu cha kawaida, serikali haikemei, watu wanatekwa na kupita sehemu nyingi zenye roadblocks za serikali, watu wanauawa baada ya kutekwa na watu wanaotumia gari zinazojulikana ni za serikali na rais anasema "kifo ni kifo tu", baadaye ndiyo nikichambua mambo naona kuwa kumbe hata nilivyopinga kuwa serikali haiwezi kuteka sakata la Mo Dewji, kuwa zile habari ni "conspiracy theories" tu, hazikuwa that implausible, hazikuwa za ajabu kama nilivyofikiri. Nilipinga kwa kwenda na uzoefu wangu tu kuwa huko nyuma habari kama zile zilikuwa nadra sana kuzisikia.

Magufuli kumkosoa Mambosasa na stories za watu wa nje inawezekana ni hadaa za kuwachanganya watu tu. Au inawezekana ni kweli serikali haijahusika.

Ninachosema si kwamba serikali imehusika. Ninachosema ni kwamba, habari ya kuwa serikali imehusika, ambayo hapo awali niliiona kuwa haiwezekani kabisa, ni conspiracy theory tu, baada ya utekaji kuwa kama fashion, haionekani kuwa haiaminiki kabisa kama nilivyoona mwanzo.

Tutafute ushahidi zaidi. Hawa walinzi wa Ikulu inawezekana kuna siku watafunguka. Kuna watu wanagoja mpaka wakikaribia kufa ndiyo wanatoa siri zao, kwa sasa bado wapo wapo tu.
 
Huwa napata shida na maelezo ya Kabendera.

Kulikuwa na haja gani ya kumleta nyumbani kwake (IKULU ) kumuulia pale ?

Sio El Chapo, wala Mobutu Sese Seko, wala Al Capone the Mafia boss, ambae aliwahi kumleta mbaya wake sebuleni kwa mkewe na watoto, amshutie hapo.

Kuna ma torture chamber na majela ya kijeshi huko ndio madikteta ambao wanataka kuwahoji ma dissidents na kuwa shuti wao personally kama kina Saddam Hussein huwa wanakutana nao huko. Sio kwenye dining table ya mkewe.
Yeye mwenyewe aliwahi kujisema ni kichaa
 
Magufuli alifanya hili tukio kwa mkono wake na humu jf ililetwa mpaka thread na ilikuwa ni kipindi ambacho kulikuwa na madai kwamba aliuliwa kwenye Moja ya safe houses za usalama halafu akapelekwa kwenye kisiwa Fulani kule bahari ya Hindi akamezwa na chatu ndio wavuvi wakaja wakaona shati na handkerchief baada ya madai haya ndio jamaa mmoja akaja akasema hapana aliuwawa na JPM kwa mkono wake mwenyewe.
 
Back
Top Bottom