Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji

Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji

Mwandishi kwa makusudi kabisa ameamua kutumia picha ambayo ilikua ni siku Magufuli anawasilisha silaha zake kufanyiwa ukaguzi kwa maelekezo ya RC wa Dar.

Ambaye alitaka kila mkazi wa Dar apelekw silaha zake kufanyiwa ukaguzi. Ndipo ikapatikana hiyo picha. Watakaoona hicho kitabu na hawajui juu ya hilo wakisoma hicho kipande cha "he always carried a gun" kuna mtazamo wataupata.

Huyu kibaraka wa magharibi ana shida sana. Yeye anatunga tu hadithi za uongo. Sijui ni kwa manufaa ya nani
 
What is your point?

Hakubeba bunduki kila mara?

Hiyo picha inawezekana ni sehemu ya kutengeneza plausibility kwamba Magufuli alimuua Saanane kwa mkono wake mwenyewe.

Ukiweka madai kwamba Alhaji Ali Hassan Mwinyi alimuua mtu kwa mkono wake mwenyewe, kwa bastola, wakati hakuna ushahidi wowote kwamba Alhaji Ali Hassan Mwinyi alikuwa na bastola, hatujui hata kama alijua kutumia bastola, madai hayo yanapata ugumu kukubalika.

Ukiweka madai kwamba Magufuli alimuua mtu kwa mkono wake mwenyewe, ingawa madai hayo bado yana ugumu kuyahakiki, lakini ugumu wake si mkubwa kama yale madai ya Alhaji Ali Hassan Mwinyi, kwa sababu angalau Magufuli tunajua alikuwa na bastola, kuna ushahidi wa picha anaionesha, most likely anajua kuitumia.

Hiyo picha ni ya Magufuli, inajulikana, huwezi kusema kapakaziwa picha si yake.

What is your point?

Sijawahi ona kwenye law of evidence ikihusisha comparative or relativity evidence. Kila case inajitegemea. Hicho ilichosema hakiwezi kimtia hatiani mtu.
 
Mkuu Cheo Cha Urais kinakaliwa na Binadamu ..
Najua unashangaa sana kuona Jina Rais kuuwa ...

Lakini tambua yule alikuwa Binadamu tena mwenye hisia Kali na wakati mwingine alishindwa kutawala hisia zake ...

Nakupa mfano mmoja ...Mkuu wa Mkoa DSM alishauwa mtu ..akashusha na bia mbili baada ya tukio.. Tena akajisifia kibaka akiingia kwangu kuchukua kuku wangu hii ndio dawa ..
Anashindwa kujua mtu hana silaha na ni kibaka..lenga hata mguu
Nakubaliana nawe kabisa Rais ni mwanadamu wa kawaida kabisa kama sisi na ametoka miongoni mwetu, na hata miongoni mwetu wengine ni bora kwa kila kitu kuzidi Rais.
Ndio maana Rais anakuwa na wasaidizi wengi, tena wengine wana maarifa na upeo wa hali ya juu kuliko Rais.
Hii ni kwa sababu kila neno na tendo la Rais linapaswa kuwa sahihi ili kulinda heshima ya Rais na uRais.
Ndio maana ana kuwa na ulinzi mpaka anapo enda haja na hata faragha yake inakuwa chini ya ulinzi.

Tuhuma hizi kwenye hiki kitabu hata kama Magufuli angekuwa hai asinge athirika moja kwa moja yeye kama Magufuli ila u Rais ndio ungeathirika na moja kwa moja tunazungumzia serikali.
Ndio maana nika sema serikali haipaswi kuliacha jinsi lilivyo .
 
Nanukuu......
Kitabu cha “In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist” kilichoandikwa na Erick Kabendera, @kabsjourno kimeanza kuuzwa leo. Mwandishi anaeleza kuhusu kutekwa na kuuwawa kwa Ben Rabiu Focas Saanane, December 2016 alipigwa risasi na mwili wake kutupwa mto Rufiji.

View attachment 3189981View attachment 3189980
Wote tunachekelea huu upumbavu wa mwandishi...



....Ni hayo Tu!!
 
Ndo maana mpaka leo nikisikia jina la Magufuli likitajwa huwa natetemekaga nikihisi bado ni mtawala.

Mtakatifu meko alikuwa mafia sana.
Mimi ni mhanga wa udikteta wa huyo magufuli wa chato ndio maana alipofariki niliondoka na kwenda kunywa bia.
Leo watu wanaona kuua na kuteka ni kitu cha kawaida kwa kuwa muasisi wa hya mambo ni Magufuli
 
Angelisema Magufuli alitoa 'maelekezo' ningeweza kumwamini.

hili la kusema eti alikutanishwa na Magufuli Ikulu na kwa vile Magufuli alipenda kubeba bastola, eti akachomoa bastola na kumpiga risasi kwa mkono wake, hainiingii akilini mimi.
Ni ngumu sana jambo hilo kutendeka kama alivyolirahisisha kwa kuliandika.
Kwa magufuli iliwezekana kabisa
 
Watoke na majibu ya hilo na mengine,nirahisi sana kujiosha.
Tena mh rais wetu anatakiwa asiache kusema chochote hata kukemea tu maana alikua msaidizi wa kwanza wa mheshimiwa dkt Magufuli.
Kamwe haimpasi kuacha kuchafuliwa magufuli, hata kama alikua na mabaya kiasi gani kuna namna anapaswa kusitiriwa.
 
Tena mh rais wetu anatakiwa asiache kusema chochote hata kukemea tu maana alikua msaidizi wa kwanza wa mheshimiwa dkt Magufuli.
Kamwe haimpasi kuacha kuchafuliwa magufuli, hata kama alikua na mabaya kiasi gani kuna namna anapaswa kusitiriwa.
Akina Samia wenyewe hawapendi hata kusikia jina la mtakatifu meko alafu leo uwaambie wakemee akina kabendera are you serious? Samia na Kabendera ni wahanga wa umafia wa Magufuli
 
Nanukuu......
Kitabu cha “In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist” kilichoandikwa na Erick Kabendera, @kabsjourno kimeanza kuuzwa leo. Mwandishi anaeleza kuhusu kutekwa na kuuwawa kwa Ben Rabiu Focas Saanane, December 2016 alipigwa risasi na mwili wake kutupwa mto Rufiji.

View attachment 3189981View attachment 3189980
Jana nimekunywa supu ya kwasakwasa!! aka NYUMBU
 
Hoja ninkwamba hiyo ni picha ya kweli ya Magufuli na picha yoyote halali ya Magufuli ni halali kuitumia kwenye cover la kitabu cha Magufuli.

Malalamiko yangekuwa na point kama picha ingekuwa si ya kweli ni ya kutengenezwa.

Sasa ukiikataa picha hii kutumika kwenye cover la kitabu unakataa nini?

Picha si ya Magufuli?

Magufuli hakuwa na bastola?

Magufuli alikuwa ni Kiongozi wa nchi. Je mamlaka zimetoa ruhusa kutumika picha yake kwenye "kitabu cha aina hii"?
 
Back
Top Bottom