Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji

Erick Kabendera kupitia Kitabu chake: Ben Saanane aliuawa na Rais Magufuli na maiti yake ikatupwa Mto Rufiji

Kabendera ni mwandishi wa habari, akawa anaandika taarifa za kiuchunguzi na kutafuta majarida ya nje aziuze, sio asaidie. Mtofautishe na yule mwandishi aliyefariki awamu ya Mwinyi aliyeandika kuhusu Loliondo kuuzwa, huyo alitaka kusaidia nchi.

Waandishi kama Kabendera kuna wanaotuma taarifa nje, kuna wanaopewa agenda kutoka nje waziandike kwa wasomaji wa ndani na wa nje. Mfano andika agenda ya ubaya wa bwawa la umeme linalojengwa, andika ubaya wa bomba la mafuta kutoka Uganda kwamba linachafua mazingira (hii kandarasi walikuwa nayo Wakenya).

Snowden hakuwa spy, alikuwa contractor wa NSA na CIA kutokana na utaalamu wake. Akavujisha siri, akaiba data za serikali akashtakiwa, ila huwezi msikia analialia kumlalamikia Obama sababu alijua anachofanya. Kabendera yeye alijua kupokea miamala tu, kuhusu akigundulika hakutaja kujisumbua.
Kumbe alhaji mwinyi aliua
 
Wewe unataka ushahidi gani?

Pia unaweza kuandika chochote unachoona kinafaa, kama kuna mtu ana tatizo na kilichoandikwa ataenda kufungua kesi mahakamani.

Kwa hiyo yale ambayo yameandikwa na Kabendera kwamba amempiga risasi saa 8 Ikulu, hayahitaji ushahidi. Hivyo tumuamini?
 
Wewe unataka ushahidi gani?

Pia unaweza kuandika chochote unachoona kinafaa, kama kuna mtu ana tatizo na kilichoandikwa ataenda kufungua kesi mahakamani.
Nahisi kupitia kitabu hiki Beni ataachiwa huko aliko.
 
Kabendera angekuwa nchi kama Russia angeuwawa kwa sumu, China angenyongwa, Marekani angeuwawa na kudaiwa amefanya suicide, Israel uko ndio angefungwa kama Mordechai Vanunu.

Kabendera alikuwa anauza taarifa za nchi nje kwa siri, lengo sio kusaidia nchi bali kupata faida binafsi za kiuchumi. Uko ndio akapata hela akajenga mjengo wake mkubwa alionao sasahivi.

Taarifa zake sometimes zilikuwa sahihi, ila hazikuwa na faida kwetu akiziuza nje.

Huyu hata angeambiwa andika kusema Tanzania inadhamini na kuwapa silaha waasi wa DRC ili inunue madini kwao angeandika. Yeye mradi alipwe, ndio maana alikamatwa na hela hazijulikani zimetoka wapi na kwa malipo ya nini. Waandishi kama hawa wapo wengi Nigeria na bara la Afrika, wananunuliwa kwa vipande vya fedha.

Kuhusu kukataliwa kutoka kizuizini akamzike mama yake hiyo sio ajabu mbele ya sheria. Wenzake kina Snowden wakichezea national interests hawaleti chuki kwa waliowakamata, hakunaga mole, double agent au spy anayekamatwa alafu akamchukia aliyemkamata. Huyo anakuwa kavamia fani.

Yoda
Chukua maarifa haya kutoka kwa huyu mjuvi. Ana majibu ya maswali mengi uliyouliza.
 
Magufuli alifanya hili tukio kwa mkono wake na humu jf ililetwa mpaka thread na ilikuwa ni kipindi ambacho kulikuwa na madai kwamba aliuliwa kwenye Moja ya safe houses za usalama halafu akapelekwa kwenye kisiwa Fulani kule bahari ya Hindi akamezwa na chatu ndio wavuvi wakaja wakaona shati na handkerchief baada ya madai haya ndio jamaa mmoja akaja akasema hapana aliuwawa na JPM kwa mkono wake mwenyewe.

Bro pitia upya ulichoandika. Wanaita contradiction
 
Nasema nina uhakika kwa sababu hana ushahidi mwingine wa kuaminisha watu kuhusu allegation aliyoitoa kwa Magu...

Mtu mwenye akili isiyo fikiri kimantiki ni rahisi kuamini ni kweli Magufuli alimuua Ben kwa kuangalia picha ya cover tu...

Hili hapa lazima mamlaka ziingilie kati. Maana hapa ni kuichafua serikali bila kujali rais aliyeko madarakani
 
Hizi taarifa alizipata na kudhibitisha lini kwanza?

Kama alizipata kabla muhusika hajafa kwanini aje atoe kitabu chake leo hii muhusika akiwa hayupo?

Na kama amekuja kuzipata baada ya muhusika kuwa marehemu, hicho kitabu chake kina masaada Gani Kwa Sasa? Tukamfukue marehemu kisha tumfungulie kesi ya mauaji au??
 
Kipindi cha Magu hakuna mwenye utimamu wa akili aliyepinga utawala ule wa kiimla ,ama taasisi zilizokuwa zikitetea justice ama uhuru wa Habari na ulinzi wa taarifa ilibaki salama.

JF yenyewe ilipitia misukosuko sio poaa wakimlazimisha Max atoe taarifa za watu,baada ya kukaza wakamfungulia makes kibao,Max Kisutu ilikuwa kama ghetto tu, haikutosha wakajaribu kufungia akaunti zote za taasisi, JF ikalazimika kupunguza wafanyakazi almost nusu, ili kubana matumizi,Max ikabibi Apunguzi mawakili aanze kujitetea mwenyewe kuukabili ukata, that dude was a lucifer typically.,halafu unakuja unasemasema tu kumtetea
Both opposition and government sources I have spoken to…

Hii ni serious allegation. Hivi Kabendera yupo Tanzania au alishahamia nje ya Nchi? Urais ni taasisi na wanaweza kumuita athibitishe hiki alichoandika

Ngoja tununue hicho kitabu tukisome neno kwa neno
Wamuite?

Vipi kama wakamuita naye akatoa uthibitisho?
 
Back
Top Bottom