A
Anonymous
Guest
Serikali ilitambulisha mfumo wa ESS kwa Watumishi wa Umma miaka mitatu iliyopita. Ndani ya mfumo huo kuna jukwaa la E-Utendaji (PEPMIS), ambalo mtumishi anatakiwa kuingiza majukumu yake ya kazi kila siku.
Bahati mbaya, kwa sasa mfumo huo hauko imara. Kuna muda unakuta jukwaa la E-Utendaji linapatikana na kuna muda hulipati kabisa.
Kimsingi, E-Utendaji ndiyo inayomfanya Mtumishi wa Umma aonekane anafanya kazi, kwa sababu kila siku anatakiwa kupandisha kazi anazozifanya. Sasa unaweza kuingia kwenye mfumo na usilikute jukwaa hilo, bila kuwepo kwa maelezo yoyote wala mtu anayewajibika.
Kwa mfano, jukwaa la E-Utendaji tangu jana, tarehe 7 Agosti 2026, halipatikani, hivyo huwezi kupandisha kazi yoyote. Na hakuna anayewajibika kwa hilo upande wa Wizara ya Utumishi.
Jukwaa hilo ndilo linaloonyesha utendaji wa mtumishi na baadaye hutumika katika masuala ya kupandishwa madaraja au kuongezewa mshahara. Wapo watumishi wengi ambao wameathiriwa na mfumo huo kutopandishwa madaraja kwa sababu alama zao ziko chini.
Ushauri kwa Serikali ni kwamba mfumo huo bado haujawa imara. Lazima tukubaliane uwe na kipindi cha majaribio na uboreshaji wa kutosha, badala ya kuendelea na mfumo huo kwa namna ambayo hatimaye inawaathiri wafanyakazi.