Ester Bulaya: Mtu siyo mkurugenzi, unatumia V8 la nini? Ni hujuma ya kiuchumi

Ester Bulaya: Mtu siyo mkurugenzi, unatumia V8 la nini? Ni hujuma ya kiuchumi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, amepongeza hatua za Serikali za kubana matumizi kupitia mapendekezo ya bajeti mpya, akieleza kuridhishwa na uamuzi wa kuondoa baadhi ya tozo kwa magari yanayotumia gesi na vifaa vya kielektroniki. Amesema hatua hiyo pamoja na mpango wa taasisi za umma kutumia magari ya umeme na gesi itasaidia kupunguza matumizi ya mafuta na kuelekeza fedha zaidi kwenye miradi ya maendeleo.

Akichangia Bajeti ya Serikali katika Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Tatu, Kikao cha Hamsini leo Juni 16, 2026, Bulaya alihoji matumizi ya magari ya gharama kubwa ya aina ya V8 kwa baadhi ya watumishi wasiostahili kuyatumia kwa mujibu wa majukumu yao. Alisema matumizi hayo yanaongeza mzigo wa gharama za mafuta wakati Serikali inaendelea kutafuta mbinu za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

"Lakini Mhe. Waziri usiishie hapo. Hivi mimi najiuliza, mtu sio mkurugenzi wa taasisi, sio mkurugenzi wa maeneo mbalimbali, hivi anatumia V8 ya nini? Ambazo zinatumia gharama kubwa kwenye mafuta."

 
hata kwa mkurugenzi nchi maskini kama Tanzania kutumia V8 ya million 500 inaonyesha tulivyokosa akili
Uko sahihi 100%
siyo mkurugenzi tu....,ni kwa watendaji karibu wote wa serikali hawana ulazima ww kutumia magari hayo...yanayotumia mafuta mengi,yanayohitaji kubadili vipuri ghali kila baada ya muda mfupi, na yanayonunuliwa kwa bei ghali...
Namshangaa Bulaya kuligusia hilo kijuujuu wakati hilo suala limepigiwa kelele na wadau wanaopenda serikali isiendeshwe kwa anasa kwa zaidi ya miaka 20 sasa...
Hesabu ya haraka ilikuwa ni V8 alfu 29 zinazohudumiwa na serikali..
Waziri
Naibu waziri
Katibu mkuu na manaibu wake
Mkurugenzi,
Kamishna na watendaji wao
Na hiyo ni wizara moja tu...
Bado ma-RC,ma-DC......,the list is endless
 
Wale nasikia wanayalipia sio bure, doubt it though
Hela wanazolipia ni mishahara itokanayo na kodi za wananchi.Bora hata hao wakurugenzi hutumika kukusanya mapato na kusimamia utendaji wa shughuli za maendeleo katika maeneo yao.Hao wabunge wanazalisha nini zaidi ya kupigia makofi wageni wanaotembea kwenye jengo la bunge?
 
alitakiwa aanze kuhoji kwanza kuhusu mtu asiye shabiki wa mpira, morocco alienda kufanya nini kwenye final ya afcon tena bila ruhusa ya spika.
 
The Government of Tanzania historically spent roughly TZS 558.4 billion annually on buying, fueling, and maintaining vehicles for public officials.
To give you an idea of the scale, this fleet consisted of more than 15,742 vehicles, 14,047 motorcycles, and 373 related
…hiyo ndio budget ya magari yetu wakuu, imezidi budget za wizara nyingi tuu, na ni karibu ya fedha za miradi ya maji nchi nzima
 
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, amepongeza hatua za Serikali za kubana matumizi kupitia mapendekezo ya bajeti mpya, akieleza kuridhishwa na uamuzi wa kuondoa baadhi ya tozo kwa magari yanayotumia gesi na vifaa vya kielektroniki. Amesema hatua hiyo pamoja na mpango wa taasisi za umma kutumia magari ya umeme na gesi itasaidia kupunguza matumizi ya mafuta na kuelekeza fedha zaidi kwenye miradi ya maendeleo.

Akichangia Bajeti ya Serikali katika Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Tatu, Kikao cha Hamsini leo Juni 16, 2026, Bulaya alihoji matumizi ya magari ya gharama kubwa ya aina ya V8 kwa baadhi ya watumishi wasiostahili kuyatumia kwa mujibu wa majukumu yao. Alisema matumizi hayo yanaongeza mzigo wa gharama za mafuta wakati Serikali inaendelea kutafuta mbinu za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

"Lakini Mhe. Waziri usiishie hapo. Hivi mimi najiuliza, mtu sio mkurugenzi wa taasisi, sio mkurugenzi wa maeneo mbalimbali, hivi anatumia V8 ya nini? Ambazo zinatumia gharama kubwa kwenye mafuta."

Huyu nae atulie ale kwa urefu wa kamba yake!! Sio wagurugenz pekee hata wabunge hawastahili kutembelea V8!! Kwa lipi haswa mpaka watembelee V8?
 
Huyu mama siku hizi hata simuelewi hoja zake, ni kweli tunao uwezo wa kujitegemea kibajat au anaongea tu.
Ni vile tu bajet yetu ni ya kimtindo lkn, lkn, lkn
 
Wanasiasa wa shithole countries ni wabinafsi tu,

Ukiingia highway unapishana na gari za polisi (PT kibao cheusi) kuanzia Kluger,Tako la nyani,probox na hizo LC single cab!!

Kamati za ulinzi za wilaya na mikoa zinaambatana na polisi wakiwa kwenye hayo hayo magari yao means hakuna excuses kwamba hayafiki maeneo ya ndanindani.
 
Back
Top Bottom