Ester Bulaya: Mtu siyo mkurugenzi, unatumia V8 la nini? Ni hujuma ya kiuchumi

Ester Bulaya: Mtu siyo mkurugenzi, unatumia V8 la nini? Ni hujuma ya kiuchumi

M
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, amepongeza hatua za Serikali za kubana matumizi kupitia mapendekezo ya bajeti mpya, akieleza kuridhishwa na uamuzi wa kuondoa baadhi ya tozo kwa magari yanayotumia gesi na vifaa vya kielektroniki. Amesema hatua hiyo pamoja na mpango wa taasisi za umma kutumia magari ya umeme na gesi itasaidia kupunguza matumizi ya mafuta na kuelekeza fedha zaidi kwenye miradi ya maendeleo.

Akichangia Bajeti ya Serikali katika Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Tatu, Kikao cha Hamsini leo Juni 16, 2026, Bulaya alihoji matumizi ya magari ya gharama kubwa ya aina ya V8 kwa baadhi ya watumishi wasiostahili kuyatumia kwa mujibu wa majukumu yao. Alisema matumizi hayo yanaongeza mzigo wa gharama za mafuta wakati Serikali inaendelea kutafuta mbinu za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

"Lakini Mhe. Waziri usiishie hapo. Hivi mimi najiuliza, mtu sio mkurugenzi wa taasisi, sio mkurugenzi wa maeneo mbalimbali, hivi anatumia V8 ya nini? Ambazo zinatumia gharama kubwa kwenye mafuta."

Mbona haulizi ilikuwaje Samia achukuliwe na magari mapya alipoenda kuapishwa kwenye gereji za chamwino? Tena katikati ya msiba baada ya kuwauwa ndugu na jamaa zetu???
Msitufanye wajinga
 
Tumechoka na usanii wao kila siku mada ni hiyo hiyo hakuna mabadiliko.
 
Back
Top Bottom