Esther Malleko - Uchumi wa mwanamke ukiimarika, watoto watakuwa salama

Esther Malleko - Uchumi wa mwanamke ukiimarika, watoto watakuwa salama

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Maleko amesema uchumi wa mwanamke ukiinuliwa, familia itakuwa na amani na ukatili dhidi ya watoto utapungua na hivyo kuwataka wanawake kutumia fursa ya mikopo inayotolewa kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri kuanzisha miradi ya kiuchumi ili kupata muda wa kuwa karibu na watoto na kuimarisha ulinzi dhidi yao.

Mhe. Malleko ameyasema hayo Februari 25, 2023, wakati akizungumza na wanawake wa Kata ya Uru Mashariki Wilaya ya Moshi, alipokuwa kwenye ziara ya kusikiliza kero, ambapo amewataka pia wanawake kuwa waminifu na kurudisha mikopo kwa wakati, ili na wanawake wengine waweze kunufaika.

"Hata tupige kelele vipi kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, tusipoanza kwenye familia, hatuwezi kukomboa hichi kizazi, hivyo ni lazima tuanzie huku chini, kuboresha uchumi wa mama na familia na baada ya hapo waweze kulea familia zao, kina mama tupige kelele, mama zungumza na watoto, msiogope, kuweni marafiki nao ili wawe wazi kuwaeleza yote wanayokutana nayo na wanayopitia, lakini pia tumlilie Mungu kunusuru kizazi cha sasa" - Mhe. Esther Maleko.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.50(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.50(1).jpeg
    47.1 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.49.jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.49.jpeg
    35.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.48(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.48(1).jpeg
    47.5 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.48.jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.48.jpeg
    47.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.46.jpeg
    WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.03.46.jpeg
    46.5 KB · Views: 6
watoto wananyanyaswa sababu mama zao hawana uchumi imara mh mbunge
"mawazo mengine kuionjesha nafsi sonona tu" huna akili
 
Back
Top Bottom