Esther Matiko: Tenda za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo zitangazwe upya

Esther Matiko: Tenda za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo zitangazwe upya

Kama huyo Esther Matiko amesema hivyo basi ni Mbunge mwenye upeo mdogo na hajitambui kabisa!
Bandari ya Bagamoyo ni investment proposal ya investors na siyo demand ya Nchi.
Kwa hiyo kusema Serikali itangaze tenda ni kama vile Sisi tunahitaji hiyo Bandari.Wabunge wajaribu kuwa makini.
 
Mbunge wa viti maalum kutokea Chadema mh Ester Matiko akichangia bungeni, amesema kama ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kutoka kwa Wachina una mashariti magumu, basi tenda zitangazwe upya na makampuni yaombe ili sisi Watanzania tuamue ni kampuni ipi itujengee kwa manufaa ya taifa letu.

My take.
Najua Ndugai na Chadema hawatapenda kusikia ushauri huu wao wamejigeuza wapiga debe wa wachina
Huwezi kuwakwepa wachina kwa sasa nchi yoyote duniani maana ndio wenye pesa
 
Hizi propaganda zimechachamaa baada ya chuma kuondoka! Hizi nguvu lazima kuna watu wana deals zao hapo. Mama Samia tumia vizuri vyombo vya usalama utajua ukweli!

Ukisikiliza wanasiasa wengi wana ajenda zao! Ukiharibu jumba bovu ni lako peke yako kama sasa hivi inavyotokea kwa JPM!
Mmh. Unajuaje labda na yeye anaisupport hiyo project ya Bandari ya Bagamoyo iendelee...na wapiga debe wamewekwa strategically?
 
Unachosahau ni kuwa wachina waliomba kuwekeza, bandari wamiliki wao na sii iwe yetu, sasa tenda ukitangaza means una hela za kujenga
Mbunge wa viti maalum kutokea Chadema mh Ester Matiko akichangia bungeni, amesema kama ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kutoka kwa Wachina una mashariti magumu, basi tenda zitangazwe upya na makampuni yaombe ili sisi Watanzania tuamue ni kampuni ipi itujengee kwa manufaa ya taifa letu.

My take.
Najua Ndugai na Chadema hawatapenda kusikia ushauri huu wao wamejigeuza wapiga debe wa wachina
 
Mkuu mimi nadeclare kuunga mkono huu mradi licha ya kuwa opposition

1. Miaka 99 ni leasing period na ipo kisheria hata wakatoliki wa nje walipofika kujenga mission zao walipewa hizo duration. Kwa kuuliza tu hvi mradi wa trillion 20+ kufikia maximum utilization ni miaka chini ya 100?

2. Kuhusu kodi miaka 33 ni break even..... Hta makampuni ya madini hayalipi kodi miaka ya mwanzo mpaka wa break even kwanza ili kurudisha gharama za uendesgaji na uwekezaji. Mfano mradi wa trillion 20 mpaka urudishe gharama na faida juu ni chini ya miaka 30??

Nadhani tusijadili kwa mihemko bali reasoning tu.... kingine uwekezaji wa aina hii tusifocus kwenye kodi tu bali MULTIPLIER EFFECT!! embu fikirieni DSE itatanukaje, mabenki ya ndani kupata ukwasi, ajira kutokana na service industry kupanuka mfano kampuni za bima, logistics, shipping kujenga ofisi/Subsidiary hapa Tz. Hayo pekee yakilipa kodi ni matrillion kuliko hata sahvi ambapo hayapo.

Nadhani mjadala u focus hapo kuliko direct benefits

Tunafidia vipi kuhusu bandari zingine kutofanya kazi kwa muda wote huo?
 
Mbunge wa viti maalum kutokea Chadema mh Esther Matiko akichangia bungeni, amesema kama ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kutoka kwa Wachina una mashariti magumu, basi tenda zitangazwe upya na makampuni yaombe ili sisi Watanzania tuamue ni kampuni ipi itujengee kwa manufaa ya taifa letu.

My take:
Najua Ndugai na Chadema hawatapenda kusikia ushauri huu wao wamejigeuza wapiga debe wa Wachina.
Sio Kawaida kusikia ushauri mzuri namna huu kutoka upande wa upinzani. Hapa namuunga mkono sana Matiku. Ni mwenda wazimu tu (kama alivyosema Magufuli na kusifiwa Africa nzima) anayeweza kuendelea na ule mkataba wa masharti ya kinyonyaji namna ile. Watu wanaounga mkono ujenzi wa ile bandari blindly (kama Ndugai) wanashangaza sana!
 
Bandari ya Dsm ina kina kifupi sana kuna meli kubwa haziwezi kufika zinaishia Darban kule South Africa na pia hata meli za kawaida hupanga foleni kwenye maji kusubiria kushusha mizigo kwa kifupi Bandari ya Dsm ilijengwa kwenye uchochoro ni gharama kubwa kuipanua zaidi.

Kama ni kina kirefu, kwa nini isiwe Tanga? Maana wataalamu wanasema Tanga ndiko kwenye kina kirefu zaidi.
 
Tunafidia vipi kuhusu bandari zingine kutofanya kazi kwa muda wote huo?
Kufidia kivipi? Hvi una una fremu zinakuingizia laki 5 kwa mwezi mtu akaomba kiwanja chako ajenga supermarket. Which in turn boda boda za mtaani kwenu zitaongeza wateja, utapewa kodi ya 3m kwa mwezi. Bado watoto wako waajiriwe humo.

Hivi kwa mahesabu hayo utataka fremu yako ifidiwe ile laki 5 kwa mwezi? Au utaangalia multiplier effect ya supermarket kuja mtaani kwako?

Mimi nachosema ni kwamba tunapojadili huu mradi tuangalie faida zisizo za moja kwa moja bali fursa zitakazotengenezwa na mradi. Mfano kampuni za bima za nje kujaa hapa, kampuni za logistics, Benki zetu kupata ukwasi, SGR kuongeza volume ya mizigo, ATCL kupata wateja, kuna cross selling kwenye sekta kma utalii, uvuvi maana mtu anaweza kuja kwa nia ya kuservice bandari lakini akaona fursa kwenye sekta zingine n.k kiufupi haya mambo yaangaliwe kwa muono huu sio kodi tu na Muendelezo wa bandari zingine.
 
WACHINA NDIO WENYE BEI NAFUU KULIKO WOTE. MKISEMA WAJE WAFARANSA MTAWEZA BEI ZAKE.

HAO WACHINA NA WAOMANI KIDOGO WANA BEI NAFUU LABDA TU MKATABA UPITIWE UPYA NA WATU WANAOWEZA KU-NEGOTIATE ILA SIO KABUDI.
 
Utatangazaje tenda "upya" wakati hakuna "tenda za mradi wa Bagamoyo" ambazo zilitangazwa mwanzoni?

Vile vile hakuna kitu kinachoitwa "maradi wa Bagamoyo". Uko kwenye mpango gani wa maendeleo? Au design yake iko wapi? This is verbal engineering.

Magufuli was right. Kitu kilichopo ni project proposal from China. Rais aliyekuwepo aliikubali labda bila kusoma details zake. Na Spika alilishwa chakula cha mchana na kuonyeshwa PowerPoint na kampuni husika na hilo likatosha kwake. Watu wenye conflict of interest wafanye presentation kwa Spika na hiyo itoshe kuamua? Only in Bongo.

Spika ni mtu mkubwa sana. Hapashwi kuwa kuwadi wa kampuni linalotaka kufanya majadiliano na serikali.
Tumenyonywa vya kutosha.
 
Marehemu magufuli alitaka Rushwa toka kwa Wachina wakagoma kutoa Rushwa kwa sababu walisema wanaleta maendeleo makubwa Tanzania pindi Bandari ikikamilika na pia watatoa ajila kwa wazawa tenda kwa kampuni za watanzania , magufuli alipoona Wachina wamekuwa wagumu kutoa Rushwa na mkataba upo ikulu na hakuna wa kuthubutu kuomba asome vizuri ndipo akaamua kuwatishia Wachina ili waogope watoe Rushwa lakini Wachina wakawa wagumu kutoa Rushwa, alipoona hakuna kitu akaamua kutengeneza propaganda kuwa mikataba ina miaka 99 kodi wanachukua Wachina akiwa na Lengo la kusaka huruma toka kwa wananchi aonekane ni Mzalendo wakati hakuwa mzalendo alikuwa mpigaji kama wapigaji wengine tu.
Kama alisema uongo wewe uweke hapa kwenye jamvi tuone kama vipengele hivyo havimo kwenye mkataba,au Mwambie Jk hajitokeze kupinga Maneno ya Magufuri na Kakonko kwamba vipengele hivyo havimo kwenye mkataba,ningekuona wa maana kama ingeliweka ha kipande tu cha mashariti yaliopo kwenye mkataba, lakini Wewe unakuja na blablaa.Sasa Hivi Watanzania hatuibiwi kizembekizembe tulisha jua janja yenu.Mungu ibariki Tanzania
 
Najua Ndugai na Chadema hawatapenda kusikia ushauri huu wao wamejigeuza wapiga debe wa Wachina.
KWAN NI LAZIMA TUJENGE BANDARI YA BAGAMOYO?
Itatumika ku export nini?ni bora tuimarishe bandari zilizopo kuliko kuanza miradi mipya
 
Mbunge wa viti maalum kutokea Chadema mh Esther Matiko akichangia bungeni, amesema kama ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kutoka kwa Wachina una mashariti magumu, basi tenda zitangazwe upya na makampuni yaombe ili sisi Watanzania tuamue ni kampuni ipi itujengee kwa manufaa ya taifa letu.

My take:
Najua Ndugai na Chadema hawatapenda kusikia ushauri huu wao wamejigeuza wapiga debe wa Wachina.
Chadema haina Wabunge wa Viti Maalum mbona Hamsikii?
 
Tayari bandari ya Dares salaam inaingiza meli kubwa sana
 
Back
Top Bottom