Esther Matiko: Tenda za ujenzi wa bandari ya Bagamoyo zitangazwe upya

Kama huyo Esther Matiko amesema hivyo basi ni Mbunge mwenye upeo mdogo na hajitambui kabisa!
Bandari ya Bagamoyo ni investment proposal ya investors na siyo demand ya Nchi.
Kwa hiyo kusema Serikali itangaze tenda ni kama vile Sisi tunahitaji hiyo Bandari.Wabunge wajaribu kuwa makini.
 
Huwezi kuwakwepa wachina kwa sasa nchi yoyote duniani maana ndio wenye pesa
 
Mmh. Unajuaje labda na yeye anaisupport hiyo project ya Bandari ya Bagamoyo iendelee...na wapiga debe wamewekwa strategically?
 
Unachosahau ni kuwa wachina waliomba kuwekeza, bandari wamiliki wao na sii iwe yetu, sasa tenda ukitangaza means una hela za kujenga
 

Tunafidia vipi kuhusu bandari zingine kutofanya kazi kwa muda wote huo?
 
Sio Kawaida kusikia ushauri mzuri namna huu kutoka upande wa upinzani. Hapa namuunga mkono sana Matiku. Ni mwenda wazimu tu (kama alivyosema Magufuli na kusifiwa Africa nzima) anayeweza kuendelea na ule mkataba wa masharti ya kinyonyaji namna ile. Watu wanaounga mkono ujenzi wa ile bandari blindly (kama Ndugai) wanashangaza sana!
 

Kama ni kina kirefu, kwa nini isiwe Tanga? Maana wataalamu wanasema Tanga ndiko kwenye kina kirefu zaidi.
 
Tunafidia vipi kuhusu bandari zingine kutofanya kazi kwa muda wote huo?
Kufidia kivipi? Hvi una una fremu zinakuingizia laki 5 kwa mwezi mtu akaomba kiwanja chako ajenga supermarket. Which in turn boda boda za mtaani kwenu zitaongeza wateja, utapewa kodi ya 3m kwa mwezi. Bado watoto wako waajiriwe humo.

Hivi kwa mahesabu hayo utataka fremu yako ifidiwe ile laki 5 kwa mwezi? Au utaangalia multiplier effect ya supermarket kuja mtaani kwako?

Mimi nachosema ni kwamba tunapojadili huu mradi tuangalie faida zisizo za moja kwa moja bali fursa zitakazotengenezwa na mradi. Mfano kampuni za bima za nje kujaa hapa, kampuni za logistics, Benki zetu kupata ukwasi, SGR kuongeza volume ya mizigo, ATCL kupata wateja, kuna cross selling kwenye sekta kma utalii, uvuvi maana mtu anaweza kuja kwa nia ya kuservice bandari lakini akaona fursa kwenye sekta zingine n.k kiufupi haya mambo yaangaliwe kwa muono huu sio kodi tu na Muendelezo wa bandari zingine.
 
WACHINA NDIO WENYE BEI NAFUU KULIKO WOTE. MKISEMA WAJE WAFARANSA MTAWEZA BEI ZAKE.

HAO WACHINA NA WAOMANI KIDOGO WANA BEI NAFUU LABDA TU MKATABA UPITIWE UPYA NA WATU WANAOWEZA KU-NEGOTIATE ILA SIO KABUDI.
 
Utatangazaje tenda "upya" wakati hakuna "tenda za mradi wa Bagamoyo" ambazo zilitangazwa mwanzoni?

Vile vile hakuna kitu kinachoitwa "maradi wa Bagamoyo". Uko kwenye mpango gani wa maendeleo? Au design yake iko wapi? This is verbal engineering.

Magufuli was right. Kitu kilichopo ni project proposal from China. Rais aliyekuwepo aliikubali labda bila kusoma details zake. Na Spika alilishwa chakula cha mchana na kuonyeshwa PowerPoint na kampuni husika na hilo likatosha kwake. Watu wenye conflict of interest wafanye presentation kwa Spika na hiyo itoshe kuamua? Only in Bongo.

Spika ni mtu mkubwa sana. Hapashwi kuwa kuwadi wa kampuni linalotaka kufanya majadiliano na serikali.
Tumenyonywa vya kutosha.
 
Kama alisema uongo wewe uweke hapa kwenye jamvi tuone kama vipengele hivyo havimo kwenye mkataba,au Mwambie Jk hajitokeze kupinga Maneno ya Magufuri na Kakonko kwamba vipengele hivyo havimo kwenye mkataba,ningekuona wa maana kama ingeliweka ha kipande tu cha mashariti yaliopo kwenye mkataba, lakini Wewe unakuja na blablaa.Sasa Hivi Watanzania hatuibiwi kizembekizembe tulisha jua janja yenu.Mungu ibariki Tanzania
 
Najua Ndugai na Chadema hawatapenda kusikia ushauri huu wao wamejigeuza wapiga debe wa Wachina.
KWAN NI LAZIMA TUJENGE BANDARI YA BAGAMOYO?
Itatumika ku export nini?ni bora tuimarishe bandari zilizopo kuliko kuanza miradi mipya
 
Chadema haina Wabunge wa Viti Maalum mbona Hamsikii?
 
Tayari bandari ya Dares salaam inaingiza meli kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…