Tetesi: ESTIM kujenga barabara Kimara - Kibaha

Ata bakhresa walimjengea nyumba yake anayoishi hadi hii leo masaki, ni muhindi mmoja anaitwa giri, anakaa mikocheni b.
 
Inakusaidia nini kuwa na njia sita kuanzia kimara-kibaha wakati huohuo kuingia mjini kuna barabara moja zinakuja 6 inatoka 1 msongamao hautapungua hapo ni matumizi mabaya ya fedha za mikopo
 
wahidni kibao nawaona pale wanasimamia
 
Mwendo kasi kibo hadi kimara unaposema upanuzi unamaanisha nini??
 
Una wasiwasi na Estim ama hutaki kwa vile ni ya kitanzania. Huoni miradi iliyofanya ama, Bagamoyo Msata kajenga nani? Massana Mbezi, Kinyrezi Kifurj, na zingine nyingi.
Lakini pia hela itabaki hapa Tanzania.
 
ESTIM wako vizuri sana kuna jengo pale Morocco wamejitahidi kwenye ujenzi. Pia suala la usalama kwa wafanyakazi wanajitahidi.
 
Hongera sana Rostam Aziz.

Licha ya scandal zote bado anazidi kuula tu.
 
Sasa nimeelewa, nilikuwa sielewi mwendo kasi inatanuliwa vipi.
 
Cha muhimu barabara ijengwe hii michakato ya tenda sometimes ni ubabaishaji tu
Mbona mnafukuza Wakurugenzi kwa kutotangaza tenda? Au kuna watu wako juu ya sheria?
 

jengo la umoja wa vijana
makao makuu ya uhamiaji
 
Mie sijui nani anamiliki Estim Construction japo naona wahindi wengi, jambo moja nna uhakuka nalo, wako vizuri kwenye kazi zao, Konoike anawapa sana kazi kwenye miradi yake. Hata kwenye pesa na mambo mengine wapo safi.

Hapa kama kuna cha kujadili, tuongelee tija ya mradi au jinsi mchakato wa tender ulivyoendeshwa lakini sio kutilia shaka ufanisi wa Estim.
 
Estim wapo vizuri kupita makampuni yote ya Tanzania hata africa mashariki.

Ukiangalia madaraja ya bonde la bagamoyo japo sijapita baada ya barabara kuisha hasa majira ya mvua wamejitahidi.

Tatizo kubwa walilo nalo kidogo ni kwenye ubunifu kidogo .

Mfano barabara ya goba kwenye kona max speed ni ndogo sana, ukizidi kidogo unamwaga gari.

Makumbusho wamefanya kazi nzuri sana lakini kwenye junction kidogo wangeweka ubunifu kuruhusu magari kupishana kwa urahisi ila kazi yao ipo bora kupita hata wachina na wajapan.

Tuwaunge mkono kwa sababu pesaa inabaki bongo na waongeze watalaam hasa kwenye design. Ujenzi wapo njema sana.

Kuhusu mradi wa kimara kibaha cha msingi consultant awe mzoefu na mambo ya highway design.

Estim kama contructor ana uwezo wa kudeliver on time.

Mungu ibariki tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…