Eternal Punishment cannot be understandable by any one

Eternal Punishment cannot be understandable by any one

Eternal punishment!! Hata kama ningekuwa muamini wa dini, hii doctrine ninsingeamini kwasababu nyingi tu. Naona imetegenezwa kufanya watu waogope.
Ili iweje sasa watu wakishaogopa? ndiyo inaleta maana gani watu wakiogopa?
 
If god does not like the way I live .let him tell me not you

Nitumie nguvu za nn kumtafuta,
Unaweza kuniambia hapa duniani tupo ili kufanya nini? na je,hakuna chochote tunachopaswa kufanya tuendelee kufanya hicho kinachotufanya tuwepo hapa duniani?
 
Mkuu kiranga unaongea kwa ujasiri kwamba hakuna Mungu huyo, ningependa kujua ni Mungu yupi unayepinga kwamba hayupo.
Mungu mwenye uwezo wote, upendo wote na ujuzi wote ambaye kaumba ulimwengu huu ambao unapinga hayo yote matatu.
 
Wakuu nashukuru kwa alieanzisha Uzi huu. Umeeleza vizuri kwamba itakuwa ni ajabu ikiwa Mungu atamhukumu mtu adhabu ya milele hata kama hakuzisikia habari zake Huyo Mungu,na ingekuwa hivyo adhabu ya milele isingekuwa ikieleweka. Lakini kwa mujibu Wa Biblia kuna namna ambayo Mungu atawahukumu watu ambao hawakupata nafasi ya kumjua kama ambavyo Mimi na wewe tumepata.(mfano walioishi kabla ya injili kuwafikia na ambao hawana uwezo Wa kuielewa injili(labda wenye ulemavu Wa akili na kadhalika)..naomba ninukuu kutoka katika Biblia..." Warumi 2:12. Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea(watahukumiwa) pasipo sheria,na wote waliokosa ,wenye sheria watahukumiwa kwa sheria.....14. Kwa maana watu Wa mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati,hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. 15.hao waionyesha kazi ya torati iliyoa ndikwa mioyoni mwao,dhamiri yao ikiwashuhudia,na mawazo yao ,yenyewe kwa yenyewe ,yakiwashitaki au kuwatetea;16 katika Siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawa sawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu." kwa maandiko hayo ni dhahiri kwamba Mungu(anayehubiriwa na Ukristo) atauhukumu ulimwengu kwa HAKI. Naamini sasa inaeleweka kama tukichukulia ukristo ndiyo dini pekee ya kweli.
Ndugu umeshasikia ipo kitu inaitwa Quran. Itafute uisome ili nawe usijepata sababu kuwa hukujua ukweli. Yesu hakuleta ukristo. Ujumbe wa Yesu, Moses, Abraham ni mmoja tu.

John 17:3 Now this is eternal life: that they know you, the only true God, and Jesus Christ, whom you have sent.

Jipime imani yako na hiyo aya.
 
Wakiogopa maana yake wafuate mafundisho ya din. Of course, haina maana jwanini agope
Kwahiyo ni kama hizi sheria zetu duniani mfano za kufungwa miaka 30 au kunyongwa,ni mambo yaleyale ya kutisha watu bila kuwa na maana.
 
post: 16877044 said:
Mungu mwenye uwezo wote, upendo wote na ujuzi wote ambaye kaumba ulimwengu huu ambao unapinga hayo yote matatu.
. Sioni namna ambayo inafanya ulimwengu huu upinge uwepo wa Mungu mwenye sifa hizo. Kwanza ni kwa sababu tunataka kumtafsiri kwamba ana sifa tatu tu. Kwa mfano: kama angekuwa na sifa moja ya Kuweza yote tu tusingetazamia aumbe ulimwengu unaoashiria upendo kwani hiyo isingekuwa sifa yake, lakini kwa sababu anaweza yote na ana upendo wote ulimwengu anaouumba unaendana na hizo sifa. Kwa kifupi namaanisha kuwa ulimwengu huu hautaeleweka kirahisi kama tukilazimisha Mungu awe na sifa hizo tatu tu. Chukulia kwa mfano Mungu huyo angekuwa akifanya jambo kama APENDAVYO yeye. Yaani angeweza kuumba ulimwengu vyovyote ila Kwa mapenzi yake Amechagua kuuumba hivi.
 
Ndugu umeshasikia ipo kitu inaitwa Quran. Itafute uisome ili nawe usijepata sababu kuwa hukujua ukweli. Yesu hakuleta ukristo. Ujumbe wa Yesu, Moses, Abraham ni mmoja tu.

John 17:3 Now this is eternal life: that they know you, the only true God, and Jesus Christ, whom you have sent.

Jipime imani yako na hiyo aya.
Nashukuru, nimekuwa nikiisoma Quran mara kadhaa nipatapo nafasi. Ila unasahau kwamba ukisema Yesu hakuleta uKristo unatumia Quran kuthibitisha hilo. Yaani unakuwa umeupuuzia ushahidi wote katika Biblia unaoonesha Yesu ndiye aliyeuleta Ukristo na unachagua vile ambavyo Quran inasema. Ni vizuri ukisema kwa mujibu wa Quran Yesu hakuleta ukristo. Na kuhusu andiko ulilonukuu ninashangazwa sana kwa sababu umechagua mstari mmoja kutoka katika Biblia unaoonekana kanakwamba unatetea hoja yako wakati kuna mistari mingi inayopingana na hoja zako(Uislamu kwa ujumla) kwa hiyo nashindwa kuelewa kuwa ikiwa unaamini mstari huo ni sahihi kwa nini ile mingine unaipuuza. Kwa mfano kitabu hicho hicho Yohana 1:1 na Yohana 1:14 vinamtaja Yesu kuwa ni Mungu. Na pia sura za mwisho za kitabu hicho zinaonesha kuwa Yesu alisulibiwa,akafa na kufufuka Siku ya tatu. Nakushauri usinukuu vifungu kutetea hoja fulani halafu ukawa hujali nukuu za kitabu hicho zinazopingana na hoja zako.
 
Look!

Let's say unazaliwa katika familia ya wapagani (wasiojua Mungu) then unaishi maisha ya taabu na shida na vipindi vifupifupi vya raha.

Unaishi miaka kadhaa (labda 43) hivi, ukiwa umeelemewa na msongo wa mawazo unaotokana na matatizo mbalimbali, magonjwa na hussles. Then unakufa bila kujua au kusikia kuhusu Mungu (Au hata kama umesikia).

Then gafla kiti cha enzi kinatokea, juu yake yupo Mungu mwenye upendo wote, mwenye uwezo wote. Anakuhukumu moto wa milele na milele kwa makosa uliyofanya ukiishi hapa duniani (ambapo napo ulikuwa na baadhi ya wema). Moto usiozimika, unounguza mara dufu ya moto wa kawaida (kwa mujibu wa vitabu vya dini). Hivi hii kitu nyie mnaelewa logic yake?

Hata binadamu tu hatujawahi kuwa na kifungo cha gerezani cha milele, iweje Mungu awe na adhabu kali namna hiyo? Can anyone tell me? I just can't understand!

Nawasilisha!
Pumzi tu inakudanganya tu wewe now umekula umeshiba hufikiri kwamba kuna Mungu post yako inaonyesha ni jinsi gani ulivyotosheka na dunia. ila subiri unaumwa upo muhimbili hapo ndipo utakapojua mungu yupo au la..
 
Nashukuru, nimekuwa nikiisoma Quran mara kadhaa nipatapo nafasi. Ila unasahau kwamba ukisema Yesu hakuleta uKristo unatumia Quran kuthibitisha hilo. Yaani unakuwa umeupuuzia ushahidi wote katika Biblia unaoonesha Yesu ndiye aliyeuleta Ukristo na unachagua vile ambavyo Quran inasema. Ni vizuri ukisema kwa mujibu wa Quran Yesu hakuleta ukristo. Na kuhusu andiko ulilonukuu ninashangazwa sana kwa sababu umechagua mstari mmoja kutoka katika Biblia unaoonekana kanakwamba unatetea hoja yako wakati kuna mistari mingi inayopingana na hoja zako(Uislamu kwa ujumla) kwa hiyo nashindwa kuelewa kuwa ikiwa unaamini mstari huo ni sahihi kwa nini ile mingine unaipuuza. Kwa mfano kitabu hicho hicho Yohana 1:1 na Yohana 1:14 vinamtaja Yesu kuwa ni Mungu. Na pia sura za mwisho za kitabu hicho zinaonesha kuwa Yesu alisulibiwa,akafa na kufufuka Siku ya tatu. Nakushauri usinukuu vifungu kutetea hoja fulani halafu ukawa hujali nukuu za kitabu hicho zinazopingana na hoja zako.
Katika mafundisho uliyofundishwa ulifundishwa kwamba Mungu anakufa?
Sasa jiulize ,kinachokufa kinaweza kuwa Mungu?

Link ISLAM: The Religion of All Prophets - GainPeace

Sasa ile aya ambayo niliinukuu, isome tena na tena, kuna kitu Yesu amekiweka wazi pale, "Mtafute," The only true God" ni yupi? Na Yesu ni nani kulingana na ile aya?

Ndugu nasema kwa usahihi ninaposema Yesu kristo hakuleta "uyesukristo"/ukristo kama ambavyo Muhammad hakuleta umuhammad au Moses hakuleta umoses. Natumai utatafakari.

Yesu alifufuka au alifufuliwa?
Kwani Yesu alikufa?
Hivi mwili wa mnyama au binadamu unaanza kuoza masaa ngapi baada ya kufa?
Yesu "alikufa" msimu wa joto au baridi? Umesema siku 3?
Wewe unaamini alikufa au alikuwa amezimia tu?

Hii nachomekea tu, ikikufaa well and good.

Dini zililetwa tu!
Refer to slave trade upate concept ya dini ya kiislamu then refer to the concept of agents of colonialism the ufahamu zaidi kuhusu ukristo!
Hizo story ziliandikwa ili ku-soften African hearts ili wasiwapinge ktk harakati zao za kutaka/ kutafuta rasilimali .walisema mpende Jirani yako kama nafsi yako, ukipigwa Kofi la kushoto geuza na la kulia.... Fikiria...
Kama umefika chuo refer course ya sociology vizuri nadhani unaweza ukapata na kukielewa ninachokisema.
 
Katika mafundisho uliyofundishwa ulifundishwa kwamba Mungu anakufa?
Sasa jiulize ,kinachokufa kinaweza kuwa Mungu?

Link ISLAM: The Religion of All Prophets - GainPeace

Sasa ile aya iinukuu, isome tena na tena, kuna kitu Yesu amekiweka wazi pale, "Mtafute," The only true God" ni yupi? Na Yesu ni nani kulingana na ile aya?

Ndugu nasema kwa usahihi ninaposema Yesu kristo hakuleta "uyesukristo"/ukristo kama ambavyo Muhammad hakuleta umuhammad au Moses hakuleta umoses. Natumai utatafakari.

Yesu alifufuka au alifufuliwa?
Kwani Yesu alikufa?
Hivi mwili wa mnyama au binadamu unaanza kuoza masaa ngapi baada ya kufa?
Yesu "alikufa" msimu wa joto au baridi? Umesema siku 3?
Wewe unaamini alikufa au alikuwa amezimia tu?

Hii nachomekea tu, ikikufaa well and good.

Narudia tena kwamba ikiwa unafikiri ile aya inaeleza kuhusu Mungu Wa kweli,una maanisha kuwa unaiheshimu Biblia kama kitabu tunachoweza kukitumia kuelewa kuhusu Mungu Wa kweli. Sasa nashangaa mbona husomi ushahidi mwingine katika Biblia unaothibitisha kuwa Yesu ni Mungu,alisulubiwa,akafa na siku ya tatu akafufuka. Kama kweli unataka kuelewa Ukweli kuhusu Ukristo usiisome Biblia ukiwa na mitazamo ya kwenye Quran, usisome ushahidi Wa kufa na kufufuka kwa Yesu huku ukilazimisha akilini mwako kwamba lazima inachosema Quran kiwe ndo sahihi. Kuhusu maswali yote uliyouliza yamejibiwa katika Biblia...tuanze na Yohana 17:3 Yesu anasema kwamba watu wamjue Mungu Wa kweli na Yesu kristo uliyemtuma. Hii inakupa shida kwa sababu inaonesha kanakwamba Mungu na Yesu ni tofauti, lakini kiBiblia Mungu ana Nafsi Tatu...inaitwa Utatu Mtakatifu Wa Mungu. Kwa hiyo huo mstari Yesu anapotaja Mungu Wa kweli anataja Nafsi ya Mungu ambayo inaitwa Mungu Baba. Sasa kosa unalofanya ni kulazimisha Mungu anayehubiriwa na Ukristo afanane na Mungu wa uislamu. Sasa sikulazimishi ukubali au ukatae dhana ya Mungu mwenye nafsi Tatu,lakini kila unapotaka kuisoma Biblia sharti ufahamu kuwa Mungu anayeelezwa hapo sio Allah...isome Biblia kama kitabu kinachojigemea kiUshahidi.
 
Dini zililetwa tu!
Refer to slave trade upate concept ya dini ya kiislamu then refer to the concept of agents of colonialism the ufahamu zaidi kuhusu ukristo!
Hizo story ziliandikwa ili ku-soften African hearts ili wasiwapinge ktk harakati zao za kutaka/ kutafuta rasilimali .walisema mpende Jirani yako kama nafsi yako, ukipigwa Kofi la kushoto geuza na la kulia.... Fikiria...
Kama umefika chuo refer course ya sociology vizuri nadhani unaweza ukapata na kukielewa ninachokisema.
Kuhusu kuletwa kwa dini na labda kwamba walizileta ili kufanikishe azma yao ya kuwatawala waafrika sina kipingamizi. Lakini unapotolea mfano maneno ya Yesu kwamba mtu akikupiga kofi shavu la kushoto mgeuzie na la kulia kwamba ni neno waliloandika ili kuwatawala waafrika unapotosha watu. Kwa sababu hukumbuki kwamba hayo maneno yameandikwa karne ya kwanza na watu ambao ni wayahudi halafu ukoloni Afrika umeanza kwa makadirio miaka ya 1800 na umeletwa na wazungu. Watu ambao Yesu anawaambia maneno hayo na wao wakayaandika ni mitume wake,na kwamba kupitia maneno hayo waliteswa na wengine wao waliuawa, hakuna aliyefaidika kupata mali au utawala miongoni mwao walioandika maneno hayo. HALAFU usisahau kuwa dini haikosi usahihi kwa sababu imeletwa ama walioileta walikuwa na malengo mabaya bali inakosa kuwa dini sahihi kama TU sio dini sahihi.
 
Dini zililetwa tu!
Refer to slave trade upate concept ya dini ya kiislamu then refer to the concept of agents of colonialism the ufahamu zaidi kuhusu ukristo!
Hizo story ziliandikwa ili ku-soften African hearts ili wasiwapinge ktk harakati zao za kutaka/ kutafuta rasilimali .walisema mpende Jirani yako kama nafsi yako, ukipigwa Kofi la kushoto geuza na la kulia.... Fikiria...
Kama umefika chuo refer course ya sociology vizuri nadhani unaweza ukapata na kukielewa ninachokisema.
Kila mtu anakuja na kusema dini zimeletwa na zimetungwa na watu,lakini hakuna aliyekuja kuthibitisha hilo ili tukubaliane na maneno yake.
 
Narudia tena kwamba ikiwa unafikiri ile aya inaeleza kuhusu Mungu Wa kweli,una maanisha kuwa unaiheshimu Biblia kama kitabu tunachoweza kukitumia kuelewa kuhusu Mungu Wa kweli. Sasa nashangaa mbona husomi ushahidi mwingine katika Biblia unaothibitisha kuwa Yesu ni Mungu,alisulubiwa,akafa na siku ya tatu akafufuka. Kama kweli unataka kuelewa Ukweli kuhusu Ukristo usiisome Biblia ukiwa na mitazamo ya kwenye Quran, usisome ushahidi Wa kufa na kufufuka kwa Yesu huku ukilazimisha akilini mwako kwamba lazima inachosema Quran kiwe ndo sahihi. Kuhusu maswali yote uliyouliza yamejibiwa katika Biblia...tuanze na Yohana 17:3 Yesu anasema kwamba watu wamjue Mungu Wa kweli na Yesu kristo uliyemtuma. Hii inakupa shida kwa sababu inaonesha kanakwamba Mungu na Yesu ni tofauti, lakini kiBiblia Mungu ana Nafsi Tatu...inaitwa Utatu Mtakatifu Wa Mungu. Kwa hiyo huo mstari Yesu anapotaja Mungu Wa kweli anataja Nafsi ya Mungu ambayo inaitwa Mungu Baba. Sasa kosa unalofanya ni kulazimisha Mungu anayehubiriwa na Ukristo afanane na Mungu wa uislamu. Sasa sikulazimishi ukubali au ukatae dhana ya Mungu mwenye nafsi Tatu,lakini kila unapotaka kuisoma Biblia sharti ufahamu kuwa Mungu anayeelezwa hapo sio Allah...isome Biblia kama kitabu kinachojigemea kiUshahidi.
Ndugu hiyo utatu ni dogma ya kanisa haina uhusiano wowote na mafundisho aliyofundisha Yesu.

Umewahi kuisoma hii?
Deuteronomy 6:4 Hear, O Israel: The LORD our God, the LORD is one.

na hii
John 14:28 "You heard me say, 'I am going away and I am coming back to you.' If you loved me, you would be glad that I am going to the Father, for the Father is greater than I.

Hii je nafsi moja inaomba msaada kutoka kwa nafsi ingine?
Matthew 27:46 About three in the afternoon Jesus cried out in a loud voice, "Eli, Eli, lema sabachthani?" (which means "My God, my God, why have you forsaken me?").

Na wewe pia ni nafsi ya nne ya Mungu? Au unaifahamu vipi hii aya?

John 20:17 Jesus said, "Do not hold on to me, for I have not yet ascended to the Father. Go instead to my brothers and tell them, 'I am ascending to my Father and your Father, to my God and your God.'"

Ujumbe umekufikia, siku ya hukumu utajitetea vipi kwa kumshirikisha Mungu?

Link The Surprising Origins of the Trinity Doctrine

Link2. God - a single entity and not a trinity | The Gospel Truth

... ushahidi mwingine katika Biblia unaothibitisha kuwa Yesu ni Mungu,alisulubiwa,akafa na siku ya tatu akafufuka. ... Kuhusu maswali yote uliyouliza yamejibiwa katika Biblia...tuanze na Yohana 17:3 Yesu anasema kwamba watu wamjue Mungu Wa kweli na Yesu kristo uliyemtuma. Hii inakupa shida kwa sababu inaonesha kanakwamba Mungu na Yesu ni tofauti, lakini kiBiblia Mungu ana Nafsi Tatu...inaitwa Utatu Mtakatifu Wa Mungu. Kwa hiyo huo mstari Yesu anapotaja Mungu Wa kweli anataja Nafsi ya Mungu ambayo inaitwa Mungu Baba. Sasa kosa unalofanya ni kulazimisha Mungu anayehubiriwa na Ukristo afanane na Mungu wa uislamu. Sasa sikulazimishi ukubali au ukatae dhana ya Mungu mwenye nafsi Tatu,lakini kila unapotaka kuisoma Biblia sharti ufahamu kuwa Mungu anayeelezwa hapo sio Allah...isome Biblia kama kitabu kinachojigemea kiUshahidi.

Mungu wa biblia sio Allah?
Mungu wa Yesu anaitwa nani?

Mafundisho ya Quran na Biblia yanapingana kuhusu mambo yote ya Msingi. Hakuna namna ambayo mtu anaweza kufanya upatanisho wa mafundisho ya vitabu hivi kwa namna yoyote, yaani tunabakiwa na uchaguzi mmoja tu- kukubali mafundisho ya kitabu kimoja ambacho tumeridhika kwamba ni sahihi na kuyakataa mafundisho ya kitabu kinachopingana. Kazi ambayo kila mtu anabaki nayo ni kujua kipi kati ya vitabu hivi ama vingine ni Neno La Mungu.

Hivyo tusisahau kwamba wahusika wote japokuwa wanafanana majina ni Tofauti kati ya vitabu hivi, Mungu,Yesu,Musa,Farao na wengine wote wanaelezwa tofauti kabisa na wanavyoelezwa katika kitabu kingine.

TUANZE hapa- katika Biblia Mungu ni mmoja na ana Nafsi Tatu Takatifu. Katika Quran Mungu ni moja na hana mshirika. Hapo hao ni Miungu tofauti kabisa (Allah si Eli(Yehova)). Katika Biblia Yesu ni Mwana Wa Mungu,alisulubiwa,akafa, Siku ya Tatu akafufuka na hakuna njia nyingine ya kufika mbinguni isipokuwa kwa njia ya Yesu. Katika Quran Yesu(Isa) ni mtume,hakufa wala kufufuka bali Allah alimchukua kimuujiza. Hapo pia ni watu tofauti kabisa (mmoja wa kufikirika na mwingine halisi) vivyo hivyo kwa mambo mengine yote.
Hii ndio sababu nilishangazwa ulipojaribu kunukuu maandiko katika Biblia unayoamini ni sahihi wakati unayapita kama huyaoni maand iko yanayoeleza tofauti. Mfano umenukuu Yohana 14:28 na unataka nione Yesu anaposema Baba ni MKUU kuliko mimi. Halafu unasahau kwamba hapohapo Yesu anamtaja Mungu kama BABA yake kitu ambacho wewe kama Muislamu hukubaliani nacho. Sasa nikueleweje, kwamba hapo ukweli ni neno Mkuu na sio neno Baba?

Kwa hiyo mengi katika uliyoandika ni mtazamo wa kiislamu na vile Quran inaeleza.

Kwa mujibu wa Biblia kuna mafundisho yafuatayo-- Kwamba Mungu(Yehova/Eli/YHWH) ni mmoja. Na kwamba ana Nafsi Tatu Takatifu. Kwamba Yesu ni Mwana Pekee wa Mungu( neno mwana lina maana yake kiBiblia, usitafsiri kirahisirahisi). Alifanyika mwili na kuishi duniani kama mwanadamu kamili karne ya kwanza, alisulubiwa,akafa, siku ya tatu akafufuka ili awe upatanisho kati ya mwanadamu mwenye dhambi na Mungu mtakatifu( kumpatanisha na nafsi yake Mwenyewe) na kadhalika wa kadhalika
 
Nikirudi kwenye mada tuliyonayo. Adhabu ya milele haitakuwa ya haki (au haitaeleweka) kama watu ambao kwa namna moja ama nyingine waliishi tofauti na mafundisho ya dini ya kweli( yoyote ambayo itakuwa ya kweli) lakini sio kwa kukusudia( watoto, walemavu Wa akili, watu wasiofikiwa na ujumbe huo na wengineo) halafu wakahukumiwa adhabu ya milele motoni. Hivyo dini zote zinapaswa zipimwe kwa jinsi suala hili litakavyotatuliwa ili tujiaminishe kuwa Mungu wanayemhubiri atatenda haki katika hukumu.

Kuhusu Ukristo nimekwisha kueleza hapo kwanza. Kwamba Mungu atatenda haki kwani atawahukumu wasiofikiwa na ujumbe kwa vile walivyoishi wakitetewa na kushitakiwa na Dhamiri zao. Rejea Warumi 2:12-16. Na kwamba baada ya Yesu kufa alishuka kuzimu kuwahubiri walioishi kabla yake. Yaani kila mtu atatendewa haki siku ya hukumu.
Ni wito wangu kwa watu wanaoamini dini zingine watueleze kwa mtazamo wa dini zao je haki itatendeka siku hiyo? La sivyo tuhitimishe kwamba dini pekee inayoonekana inaeleza haki itatendeka ni Ukristo.
 
Jaribu Kupitia Near death Experience,yaani watu ambao tayari walikumbana na matukio ya kuzimu na kwa pamoja hushuhudia Mfano mmoja wapo ni huyu Meja Msuya na pia isitoshe no one in this world anaweza aka claim kwamba hajawai kusikia habari za Mungu na hivyo kujitetea kwamba hizi ni habari mpya katika kizazi hiki.
 
Back
Top Bottom