Eternal Punishment cannot be understandable by any one

Eternal Punishment cannot be understandable by any one

Msicho elewa kuwa hata hivyo vitabu viliandikiwa na watu
Inshort n vitabu.vya kusadika tuu..

Napo amua kuvisoma.navisoma sawa navyo soma vitabu vingine..hakuna.cha zaid

Nacho ambulia n yale mazur na nayatumia ktk maisha ila sina huo muda na sion sababu ya kuabudu huyu mtu mmwetae mungu/allah
Nani amekwambia Mungu ni mtu? Au umesoma wapi hiyo?
Vitabu vimeandikwa na watu? Ulitaka viandikwe na nani?
Je ujumbe au yaliyomo pia ni maneno ya watu?
Sawa soma na hiki?
Link http://www.islamicbulletin.org/free_downloads/quran/bible_quran_science.pdf

Unategemea utaishi miaka mingapi?
 
Hii dunia ndio Jehanamu tosha.
Tabu, Magonjwa, Njaa, vifo, Vita etc.

Hakuna binadamu yeyote yule anaejua nini kinatokea baada ya kifo.
Wote tuna hisi tu .
 
Hii dunia ndio Jehanamu tosha.
Tabu, Magonjwa, Njaa, vifo, Vita etc.

Hakuna binadamu yeyote yule anaejua nini kinatokea baada ya kifo.
Wote tuna hisi tu .
Kama umejiumba hivi usemavyo ni sawa. Kama unaamini umeumbwa, kwa nini usiamini kile anachokwambia aliyekuumba?

Katika ulimwengu huu kila anayetengeza kifaa, anaandika na user's manual.
Mungu ameleta user guide/user's manual kupitia wajumbe wake. Ukiukataa ujumbe wake ambao unakueleza nini kinakusubiri baada ya kifo, baada ya kifo hutapata second chance.

kama utapata muda angalia video ambazo nimeweka kwenye uzi huu, ziko ambazo wanasayansi wanakubali sasa kuwa ipo " hereafter".
 
Sheria ya Mungu imewekwa Ktk Akili na Moyo wa kila mtu , hivyo kila mtu atahukumiwa kwa kadiri alivyopewa ,
 
Wakuu nashukuru kwa alieanzisha Uzi huu. Umeeleza vizuri kwamba itakuwa ni ajabu ikiwa Mungu atamhukumu mtu adhabu ya milele hata kama hakuzisikia habari zake Huyo Mungu,na ingekuwa hivyo adhabu ya milele isingekuwa ikieleweka. Lakini kwa mujibu Wa Biblia kuna namna ambayo Mungu atawahukumu watu ambao hawakupata nafasi ya kumjua kama ambavyo Mimi na wewe tumepata.(mfano walioishi kabla ya injili kuwafikia na ambao hawana uwezo Wa kuielewa injili(labda wenye ulemavu Wa akili na kadhalika)..naomba ninukuu kutoka katika Biblia..." Warumi 2:12. Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea(watahukumiwa) pasipo sheria,na wote waliokosa ,wenye sheria watahukumiwa kwa sheria.....14. Kwa maana watu Wa mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati,hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. 15.hao waionyesha kazi ya torati iliyoa ndikwa mioyoni mwao,dhamiri yao ikiwashuhudia,na mawazo yao ,yenyewe kwa yenyewe ,yakiwashitaki au kuwatetea;16 katika Siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawa sawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu." kwa maandiko hayo ni dhahiri kwamba Mungu(anayehubiriwa na Ukristo) atauhukumu ulimwengu kwa HAKI. Naamini sasa inaeleweka kama tukichukulia ukristo ndiyo dini pekee ya kweli.
 
Hakika mungu km yupo basi ndio mdhambi mkubwa

Kjn wawatu kaishi maisha ya dhiki,magumu yakaraha..ajui hayo mambo ya dini bado anamtupa kwenye moto mkali wa milele

Kweli iman kitu mbaya
Mkuu huyo mungu unayesema ni mdhambi atakuwa ni yule anayehubiriwa na dini ambazo adhabu ya watu ambao hawakupata nafasi ya kumjua ni Kali kiasi hicho. Lakini Mungu Wa Biblia anatoa maelezo kuhusu hukumu ya watu Wa namna hiyo...na bila shaka utagundua kwamba ni hukumu ya haki. Rejea Warumi 2:12-16 nimeinukuu hapo huu. Bila shaka utaona kuwa Ukristo una majibu yanayoridhisha zaidi kuhusu jambo hili.
 
Hakuna kitu kama moto wa milele. Hizo story tu vitabu vya dini vinawaambia mambo kimafumbo au lugha ambayo ni ambiguous. Waliandika wana~sodoma na ghomorrah watachomwa moto wa milele, unataka unambie hadi leo bado wanawaka? moto wa milele ni neno ambiguous sana, linaweza kua linamaanisha unachomwa unapotea milele, tofauti na ile kufa then ukafufuliwa. Sijui kama unapata my point? Kwa lugha rahisi kabisa hakuna anayeelewa chochote kile.

Alafu dini ina complications nyingi tu, utamlaumu vipi mtu kazaliwa Pagan? mtu kazaliwa Mkristo, Muislamu? nani mkweli kati yao? Una uhakika gani maana kila moja anaamini anachokiamini ndio sahihi. In other words wote tunajifanya tunajua ila hakuna anayejua ukweli, wote tunaendaenda tu. Presence ya supernatural power yaweza kuwepo au ikawa coincidence tu, no one knows kwa kua hakuna aliyewahi experience.
Hivi kwanini wanazungumziwa wakristo na waislamu tu kuwa ndiyo kila mmoja hudai yupo sahihi? mbona wanaosema kwa kujiamini kabisa kuwa hakuna mungu na wanaoamini mungu lakini hawana dini hawazungumziwi kuwa nao kila mmoja hudai yeye ndiye sahihi?
 
Kati ya vitu vigumu kuviamini ni pamoja na hili.hakuna mtu amewahi kwenda huko na akaludi kutuhadithia ukweli,tunasoma tu na tunaambiwa tuamini,kama MUNGU aliniumba kwa mfano wake tena akanipendelea akanipa kutawala vitu tofauti na binadamu,akili ya mimi kutamani mwanamke mzuri anaepita barabarani kanipa yeye mwenyewe,na tena ananiambia nikimtazama kwa kumtamani nimekwishazini tayali,yaani huo moto wa milele unanisubili,aisee hapa hua kuna utata,ndo mana kuna watu pia wanaamini siku ya mwisho ni ile utakayokufa mauti hapa duniani,tena wengine wanaenda mbele wanaongezea yamkini ukifa utazaliwa tena ktk namna nyingine,ni kizungu zungu kwa kweli
Utata ni upi sasa hebu fafanua vizuri.
 
Hakuna cha moto wala pepo zile ni story tu kama ilivyo kwa hadithi zingine za kale za mazimwi
Lipi lenye kutufanya tuamini au tukubaliane na maneno yako kuwa ulichokisema ndiyo ukweli wenyewe na sio hisia zako tu?
 
Hilo swali ukiwauliza viongozi wa dini with an open mind ndio utagundua hata wao wanabahatisha.

Sana sana utaambiwa Mungu hachunguziki.

Ila hakuna cha moto wala nini,tena concept ya moto ukiifikiria sana ndio i.amfanya Mungu aonekane mbaya kumbe kuna wajanja wameipandikiza kwa lengi la kuleta hofu kwa watu.
Hao wajanja ni akina nani hebu wataje mkuu tuwatambue.
 
Nikisema kitu fulani hakipo, kazi ya kuthibitisha inahamia kwako wewe unaesema yupo.
Kwahiyo haiitaji kuwa uhakika pindi unapotaka kusema kuwa kitu fulani hakipo? halafu kuna watu hawapingi kuwepo kwa mungu lakini pia hawasemi kuwa mungu yupo je,hawa nao itabidi wakubali tu maneno yako kusema hakuna mungu kwa kuwa wewe umesema tu?
 
Tupo wengi mkuu, mimi naamini yupo, lakini hizi dini siziamin, cuz kila dini inasema vyake, mimi namuabudu mungu sio dini... Nazichukia sana dini cuz zimeleta ubaguzi na wala sio upendo, zimeleta vikwazo vingi... Sioni sababu ya kitabu cha dini kusheheni maelfu kwa maelfu ya kurasa wakati ingetosha kuandika tu kipi tufanye kipi tusifanye , kipi dhambi kipi sio dhambi... Lakini wamepandikiza vitu vingi, historia za mababu waliouna kwa vita... Non sense... Aaaaaah wacha niishie hapa
Je,wewe huo msimamo wako wa kuamini mungu lakini hauamini dini umewezaje kujua kuwa upo sahihi kwa msimamo huo? Na kuna miungu mingi hapa duniani je,mbona hiyo haijakufanya kuacha kuamini imani ya kuwepo kweli mungu kama ulivyoacha na dini?
 
Hakika mungu km yupo basi ndio mdhambi mkubwa

Kjn wawatu kaishi maisha ya dhiki,magumu yakaraha..ajui hayo mambo ya dini bado anamtupa kwenye moto mkali wa milele

Kweli iman kitu mbaya
Unataka kusema hata hapa duniani ukifanya jambo bila ya kujua kuwa kisheria ni kosa je,huwa anasamehewa?
 
Back
Top Bottom