Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Kwa jinsi mambo yanavyoenda kwenye hizi nchi, hazifiki 2030 zikiwa nchi moja.
1. Ethiopia. Muungano wa Ethiopia ni dhaifu sana. Kila mkoa una jeshi lake na "Rais" wake. Wana mikoa 12 iliyogawanyika kimakabila. Watu wa Tigray wamelianzisha tena. Vita vita. Kabla ya 2030 hii haitakuwa nchi moja. Zinaweza hata kutoka nchi 12.
2. UK mchakato wa kuvunjq muungano umeanza na wanataka wapate kura ya kujitengavikiwezekana mapema 2028. Hata nchi Nchi tatu au nne mpya zinaweza kuzaliwa.
3. Mali. Waasi wa Azawad wanawasha moto mwingi. Kabla ya 2030 wanaweza kuwa na nchi yao.
4. DRC. M23 ni kama wameishajipatia kanchi kao.
4. Somalia. Tayari nchi kama Israel imeishawatambua Somaliland. Viongozi wake wanazunguka huku na kule duniani kulobby kutambuliwa.
Nchi gani nyingine unaona haifiki 2030 ikiwa nchi moja.