Ethiopia yenye nguvu ilishindwaje kupenya baharini kupata bandari pembe ya Afrika?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Ethiopia huwa inahesabika kama taifa lenye nguvu na mojawapo la himya za kale zaidi katika bara la Africa, kinachonishangaza ni wao kukosa upenyo wa baharini kuwawezesha kuwa na bandari yao tena wakiwa karibu kabisa na bahari za Hindi na Red Sea.

Karne zote hizo wamishindwaje kumpata mnyonge hata mmoja katika ya Somalia, Somaliland, Djibouti na Eritrea wamdunde awape upenyo kufika baharini wawe na bandari yao wenyewe!
20250204_085026.jpg
 
Conquering is not allowed if you want the country just buy it as US bought Alaska na Hawaii
 
Kama wana fedha za kutosha, waongee na Eritrea, awakatie kipande.
 
Ethiopia huwa inahesabika kama taifa lenye nguvu na mojawapo la himya za kale zaidi katika bara la Africa, kinachonishangaza ni wao kukosa upenyo wa baharini kuwawezesha kuwa na bandari yao tena wakiwa karibu kabisa na bahari za Hindi na Red Sea.

Karne zote hizo wamishindwaje kumpata mnyonge hata mmoja katika ya Somalia, Somaliland, Djibouti na Eritrea wamdunde awape upenyo kufika baharini wawe na bandari yao wenyewe!
View attachment 3224708
Wale nao wazembe waliipoteza Eritrea kifala
 
Ethiopia waliipoteza Eritrea. Ndio ilikuwa na bandari yao.
Hao wazembe sana, walikubaliji kirahisi hivyo! Bora wangepigana miaka mia au hata wangewafidia hao Eritrea upande mwingine wa nchi kama upande wa Ethiopia lakini wapate uchochoro wa baharini
 
Aisee naona sasa hivi wana JF tunawaza ubabe ubabe Kagame ametuinspire 🐼
 
Hao wazembe sana, walikubaliji kirahisi hivyo! Bora wangepigana miaka mia au hata wangewafidia hao Eritrea upande mwingine wa nchi kama upande wa Ethiopia lakini wapate uchochoro wa baharini
Eritreans walikuwa wanapigania kipande cha ardhi ambacho ni asili yao. Kwa jinsi Ethiopia ilivyo usingewachukua Waeritrea uwape ardhi ya watu wengine mfano Waoromo. Ethiopia kila jamii inaichukia nyingine ndio maana vita haiishi. Kila kabila linajitawala na lina kikundi cha wanamgambo wakishindwana na Federal government wanapigana na jeshi la nchi.
 
Back
Top Bottom