Eti kwa sababu mpenzi wake ha-view status zake wala hamposti mitandaoni, ameamua kum-unfollow Instagram na maeneo mengine, ugomvi mkali umeibuka

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni ipi nafasi ya mitandao ya kijamii kwenye mahusiano, uchumba, na ndoa hata paibuke ugomvi, kutoelewana, kutengana, au vurugu baina ya wapenzi au wanandoa kwa sababu tu ya kuposti picha, ku-view status, au ku-unfollow?

Je, migogoro hii ni matokeo ya utoto, kutokuelewa umuhimu, na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, au kuna sababu nyingine?

Unadhani ni kwa kiasi gani mitandao ya kijamii inahatarisha, inavuruga, na kuvunja mahusiano mengi ya kimapenzi, uchumba, na ndoa katika mazingira na jamii unayoishi, hali ya kuwa maendeleo ya teknolojia yanarahisisha mawasiliano?

Ni muhimu kwa watu kuelewa nafasi na athari za mitandao ya kijamii katika mahusiano yao na kutafuta njia bora za kusimamia matumizi yake ili kuepuka migogoro na kuvunja mahusiano 🐒
 
Inategemea mlikutana wapi, mostly kama mapenzi yalianzia ONLINE tegemea pia yataishia huko huko..

Pia umri, uwezo wa akili wa mtu, vipaumbele etc..

Kama Mtu anapoteza 30-50 minutes kujirekodi video ili apost status, na sometimes anafuta na kurekodi nyingine usitegemee akawa sawa kichwani.
 
unadhani ni kwa kiasi gani mitandaoni ya kijamii inahatarisha, inavuruga na kuvunja mahusiano mengi ya kimapenzi, uchumba na ndoa katika mazingira na jamii unayoishi hali ya kua ni maendeleo ya teknologia ya kurahisisha mawasiliano?🐒

Tatizo linaanza kwenye akili za hao wachache wanaotumia ndivyo sivyo hizi social media...Shida ipo kwenye wenye tatizo la afya ya akili
 
Kuna Bi dada mmoja bana alikua na mambo ya kitoto kichizi yaan, kuna siku nilichat nae kawaida akaniambia ye ni mzima yuko poa kabisa kila kitu fresh.

Baada ya nusu saa nikakuta kaweka status eti ni mgonjwa mi nika view bila ku comment chochote maana alishaniambia ni mzima, kilichofata akaanza kunimaindi eti kwanini nimeona status yake kuwa ni mgonjwa alafu nikakausha.

Nilimletea noma balaa nikamwambia sitaki drama na nikafuta namba yake ya WhatsApp siku hiyo hiyo.
 
Inategemea mlikutana wapi, mostly kama mapenzi yalianzia ONLINE tegemea pia yataishia huko huko..

Pia umri, uwezo wa akili wa mtu, vipaumbele etc..

Kama Mtu anapoteza 30-50 minutes kujirekodi video ili apost status, na sometimes anafuta na kurekodi nyingine usitegemee akawa sawa kichwani.
Nakazia
 
Ni ipi nafasi ya mitandao ya kijamii kwenye mahusiano, uchumba, na ndoa hata paibuke ugomvi, kutoelewana, kutengana, au vurugu baina ya wapenzi au wanandoa kwa sababu tu ya kuposti picha, ku-view status, au ku-unfollow?

Je, migogoro hii ni matokeo ya utoto, kutokuelewa umuhimu, na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, au kuna sababu nyingine?

Unadhani ni kwa kiasi gani mitandao ya kijamii inahatarisha, inavuruga, na kuvunja mahusiano mengi ya kimapenzi, uchumba, na ndoa katika mazingira na jamii unayoishi, hali ya kuwa maendeleo ya teknolojia yanarahisisha mawasiliano?

Ni muhimu kwa watu kuelewa nafasi na athari za mitandao ya kijamii katika mahusiano yao na kutafuta njia bora za kusimamia matumizi yake ili kuepuka migogoro na kuvunja mahusiano 🐒
Utoto utoto utoto, akishakuwa atajiona mjinga sana
 
Kuna Bi dada mmoja bana alikua na mambo ya kitoto kichizi yaan, kuna siku nilichat nae kawaida akaniambia ye ni mzima yuko poa kabisa kila kitu fresh.

Baada ya nusu saa nikakuta kaweka status eti ni mgonjwa mi nika view bila ku comment chochote maana alishaniambia ni mzima, kilichofata akaanza kunimaindi eti kwanini nimeona status yake kuwa ni mgonjwa alafu nikakausha.

Nilimletea noma balaa nikamwambia sitaki drama na nikafuta namba yake ya WhatsApp siku hiyo hiyo.
Ungekomenti tu ungepigwa kizinga mujaarab
 
🤔🤔🤔
Kila mtu ana mambo yanayomfanya ajisikie vizuri kihisia na kiakili. Kama ni Mwenza ni muhimu kuzungumza naye na kujua hata kama ni upande wa mitandao ya kijamii. Unaweza ukamuuliza mwenza wako hususa anajisikia vipi pale unapo react kwenye mitandao ya kijamii ?
Mbona mambo mengine hayana hata complications?
 
Kwenye mapenzi kuna small small details ila ni muhimu hususan kwa kizazi chetu kama ambavyo mwanaume utapenda kumuona mkeo kwa mfano anaelewana na ndugu zako vzr kwako una intepret kama kitu muhimu pia wanawake kwao vitu vdg vdg kama birthday, kumfollow mitandaon huwa wanaona ni big deal
 
Back
Top Bottom