Kulingana na muktadha wa swali lako hapo jibu ni RAY C
Jide amekaa kwenye game kwa muda mrefu sana akiwa kwenye ubora wake uleule, na ndani ya muda huo ametoa nyimbo nyingi sana kali
Ray C kadumu kwenye game kwa muda mfupi zaidi ya Jide, lakini ndani ya muda huo mfupi alifika kwenye peak ya juu sana ambayo Jide hajawahi kufikia
Ray C alikua Mzuri wa kuvutia, ana sauti tamu, alikua anajua kuimba na alikua anajua kucheza
Jide alikua anajua kufanya muziki mzuri
So ukichukulia kwa ujumla Jide ameutendea haki zaidi muziki na kipaji chake kuliko Ray C