Nadhani ni tabia ya watanzania kupenda kudharau kitu ikiwa wao hawana hicho kitu,juzi nilipita salooni moja nkaoshe nywele zangu bwana basi wakawa wanendelea na story zao mara nkasikia jamani mwisho wa mwezi mshahara umetoka ila walimu watakuwa wameshamaliza hela tiyari,wakaongezea yaani ile kazi ya kijinga,mmh nkawauliza kwani walimu wanalipwa sh ngapi wakasema si laki tano?nkasema laki tano mbona siyo haba maana watu wengi hapa mjini wanaingiza hela kidogo na wanaishi vizuri iweje hao wa laki tano(nkatoa mfano kuna watu wanafanya kazi viwandani hela yao ni ndogo mbona wanaishi)mi sikuwazingatia nkaondoka zangu basi baada ya siku mbili nkaenda suka nywele pale
Story zao,yaani maisha magumu huyu mtoto nataka nimrudishe kwa baba yake
Mwingine naye akadakia huyu mwezi wa sita anarudi kijijini
Mda kidogo nkasikia we fulani(binti yake) hiyo chai ndo mpaka jioni
Nkasema nyie saloon mbona mna hela sana maana nasikia walimu ndo hawana hela,wakaanza yaani acha tu maisha haya ni magumu kwanza kila siku upo kazini,mara hiki mara kile,ndo nkasema binadamu huwezi kuwaelewa kamwe
Kikubwa sijawahi kumdharau mtu