Eti nyimbo ya ''Usimchezee Chatu'' inamzungumzia kiongozi fulani wa nchi?

Eti nyimbo ya ''Usimchezee Chatu'' inamzungumzia kiongozi fulani wa nchi?

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
Hii nyimbo nilikuwa naisikia nikiwa mdogo,kwa akili yangu nikaelewa kama anaimbwa chatu kweli kwani ni mnyama hatari tuliambiwa anameza watu

Lakini leo hii nimesisikia tena lakini mashairi yake yanaonyesha kama haimbwi chatu kweli, ni kama anaimbwa mtu ambaye anapoteza watu maana kuna sehemu anayosema ukimchezea chatu utapatwa na ajali bila ya kutegemea, utaadhirika ujute na dunia.

Nikaamua kuuliza watu hapa hii nyimbo inamaanisha nini? sasa wengine wanasema ni kiongozi alikuwa anaimbwa wa kipindi hicho wengine wanasema sio kiongozi, hakuna jibu la uhakika 100%.

Mashairi yake

Chatu mkali porini wamuogopa
Mnyama aso kivuli hana mfupa
Tena jabari awindapo hana pupa
Apenda machakani mjini hakuzoea

x2

Ukienda njiani siku amekusudia
Ni mwepesi kubaini adui kumfikia
Usimchezee ndugu utaangamia
Ukufike (mtukutu?) ujute kuzaliwa

x 2

Usimchezee chatuu (chatuu)
Oooh chatuu eeh
Gongo usimtupie, utaukosa ushindi.

X2

Natoa onyo kwa yeyote, anayechezea chatu ni hatari
Atakuwa asipate lolote la manufaa
Na ajali imkute, bila ya kutegemea
Atakuja adhirika ajute na duniaa
 
Hii nyimbo nilikuwa naisikia nikiwa mdogo,kwa akili yangu nikaelewa kama anaimbwa chatu kweli kwani ni mnyama hatari tuliambiwa anameza watu

Lakini leo hii nimesisikia tena lakini mashairi yake yanaonyesha kama haimbwi chatu kweli, ni kama anaimbwa mtu ambaye anapoteza watu maana kuna sehemu anayosema ukimchezea chatu utapatwa na ajali bila ya kutegemea, utaadhirika ujute na dunia,
Nikaamua kuuliza watu hapa hii nyimbo inamaanisha nini? sasa wengine wanasema ni kiongozi alikuwa anaimbwa wa kipindi hicho wengine wanasema sio kiongozi, hakuna jibu la uhakika 100%.

Mashairi yake

Chatu mkali porini wamuogopa
Mnyama aso kivuli hana mfupa
Tena jabari awindapo hana pupa
Apenda machakani mjini hakuzoea

x2

Ukienda njiani siku amekusudia
Ni mwepesi kubaini adui kumfikia
Usimchezee ndugu utaangamia
Ukufike (mtukutu?) ujute kuzaliwa

x 2

Usimchezee chatuu (chatuu)
Oooh chatuu eeh
Gongo usimtupie, utaukosa ushindi.

X2

Natoa onyo kwa yeyote, anayechezea chatu ni hatari
Atakuwa asipate lolote la manufaa
Na ajali imkute, bila ya kutegemea
Atakuja adhirika ajute na duniaa

Nyimbo iko wazi...una umri gani kwanza?...iko hivi chatu ni DUDE...km hujaelewa ni mashine ya kiume...ile hua haina mfupa...inapenda machakani mjini haikuzoea..tena kuna muda inateleza kimasihara.
 
Ndio maana ya utunzi wa watu wenye akili.
Huu ni wimbo unaoishi miaka yote. Upatie tafsiri yoyote unayopenda, itaeleweka.

Unaweza kusema chatu ni "mchonga" utakubali,

Ukisema chatu ni "dusheshelele" unakwenda,

Kama chatu atakuwa "Jembe" sawa tu,

Lakini pia inaweza chatu ni akina Ngurumo wenyewe dhidi ya bendi pinzani za kipindi kile, sawa tu.

Yote ni kuonyesha jinsi gani watunzi wa zamani walivyokuwa na akili mingi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kweli huu wimbo ni fumbo kubwa sana! Mwenye kuelewa vizuri huu wimbo atupe ukweli
 
Huu wimbo uliimbwa na OSS kutokana baadhi ya wasanii walitoka Sikinde walihamia OSS akiwemo Bitchuka na Ngurumo,
Sasa Sikinde waliwaimbia nyimbo OSS ya kuwapiga dongo kuondoka kwa nahodha sio mwisho wa safari,na wao OSS wakawajibu Sikinde kwamba wasimchezee Chatu...
Hvyo ndivyo nijuavyo!lakin maudhui yake unaweza ukayapeleka kwengineko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona kila mtu anakuja na tafsiri yake katika kazi ya sanaa, iwe ya picha, uchongaji, fasihi simulizi, fasihi andishi, nyimbo, ngonjera, mashairi au hadithi basi ujue "fanani" au kwa muktadha wa uzi huu mtunzi wa wimbo kafanikiwa

Wote walioeleza tafsiri na mitazamo yao kuhusu wimbo wa "CHATU MKALI" wapo sahihi. Wameichukua kazi ya msanii na kila mmoja akaondoka nayo na kwenda kuipa maudhui anayohisi yana sadifu kazi hiyo

Nyimbo za siku hizi nyingi zinakosa ufundi huu. Zipo wazi sana, aghalabu zikikosa tafsida japo wasanii kadhaa wa kizazi kipya wamejaaliwa sauti Mashaallah
 
Chatu wako mpake kasongo atakua 🐍 anaconda na utajua maana ya usimchezee chatu
 
Huu wimbo uliimbwa na OSS kutokana baadhi ya wasanii walitoka Sikinde walihamia OSS akiwemo Bitchuka na Ngurumo,
Sasa Sikinde waliwaimbia nyimbo OSS ya kuwapiga dongo kuondoka kwa nahodha sio mwisho wa safari,na wao OSS wakawajibu Sikinde kwamba wasimchezee Chatu...
Hvyo ndivyo nijuavyo!lakin maudhui yake unaweza ukayapeleka kwengineko

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa umenipa mwanga , na inaonesha wazi kuwa wanamuziki wa zamani walikuwa hatari katika kiutumia fasihi
 
Back
Top Bottom