Eti nyimbo ya ''Usimchezee Chatu'' inamzungumzia kiongozi fulani wa nchi?

Eti nyimbo ya ''Usimchezee Chatu'' inamzungumzia kiongozi fulani wa nchi?

Mkuu umemaliza kila kitu
Ndio maana ya utunzi wa watu wenye akili.
Huu ni wimbo unaoishi miaka yote. Upatie tafsiri yoyote unayopenda, itaeleweka.

Unaweza kusema chatu ni "mchonga" utakubali,

Ukisema chatu ni "dusheshelele" unakwenda,

Kama chatu atakuwa "Jembe" sawa tu,

Lakini pia inaweza chatu ni akina Ngurumo wenyewe dhidi ya bendi pinzani za kipindi kile, sawa tu.

Yote ni kuonyesha jinsi gani watunzi wa zamani walivyokuwa na akili mingi!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa umenipa mwanga , na inaonesha wazi kuwa wanamuziki wa zamani walikuwa hatari katika kiutumia fasihi
Zamani RTD kulikuwa na IGIZO saa nne ikiitwa FASIHI NA MUZIKI ilikuwa ni wanaujadili mwimbo mmoja wanautengenezea igizo la nusu saa kisha mwisho wa igizo wanapiga muziki husika.

ilikuwa poa sana.
 
Huu wimbo uliimbwa na OSS kutokana baadhi ya wasanii walitoka Sikinde walihamia OSS akiwemo Bitchuka na Ngurumo,
Sasa Sikinde waliwaimbia nyimbo OSS ya kuwapiga dongo kuondoka kwa nahodha sio mwisho wa safari,na wao OSS wakawajibu Sikinde kwamba wasimchezee Chatu...
Hvyo ndivyo nijuavyo!lakin maudhui yake unaweza ukayapeleka kwengineko

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hii ndio ilikuwa maana halisi ya huu wimbo.
 
Back
Top Bottom