Ndio maana ya utunzi wa watu wenye akili.
Huu ni wimbo unaoishi miaka yote. Upatie tafsiri yoyote unayopenda, itaeleweka.
Unaweza kusema chatu ni "mchonga" utakubali,
Ukisema chatu ni "dusheshelele" unakwenda,
Kama chatu atakuwa "Jembe" sawa tu,
Lakini pia inaweza chatu ni akina Ngurumo wenyewe dhidi ya bendi pinzani za kipindi kile, sawa tu.
Yote ni kuonyesha jinsi gani watunzi wa zamani walivyokuwa na akili mingi!
Sent using Jamii Forums mobile app
Zamani RTD kulikuwa na IGIZO saa nne ikiitwa FASIHI NA MUZIKI ilikuwa ni wanaujadili mwimbo mmoja wanautengenezea igizo la nusu saa kisha mwisho wa igizo wanapiga muziki husika.Hapa umenipa mwanga , na inaonesha wazi kuwa wanamuziki wa zamani walikuwa hatari katika kiutumia fasihi
Na hii ndio ilikuwa maana halisi ya huu wimbo.Huu wimbo uliimbwa na OSS kutokana baadhi ya wasanii walitoka Sikinde walihamia OSS akiwemo Bitchuka na Ngurumo,
Sasa Sikinde waliwaimbia nyimbo OSS ya kuwapiga dongo kuondoka kwa nahodha sio mwisho wa safari,na wao OSS wakawajibu Sikinde kwamba wasimchezee Chatu...
Hvyo ndivyo nijuavyo!lakin maudhui yake unaweza ukayapeleka kwengineko
Sent using Jamii Forums mobile app
Watz waoga sana unaogopa hata kutaja jina unatumia code