Eti, Pana maendeleo yawezayo kupatikana nje ya sanduku la kura?

Eti, Pana maendeleo yawezayo kupatikana nje ya sanduku la kura?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam!

Maendeleo ni kupiga hatua moja ndogo kwenda hatua ya juu Bora zaidi, sasa tujiulize,

Sanduku la kura likinajisiwa, akaingia kiongozi Mkuu asiyetokana na ridhaa ya wananchi, Nini kitatokea?

Wabunge wakiingia kwa kunajisi sanduku la kura, wapate wapi mawazo na hoja za wananchi ikiwa wamejiweka wenyewe kwa wizi wa kura?

Ndani ya wabunge walioingia kwa wizi wa kura, mawaziri Bora wa kusimamia wizara na makatibu wakuu watatoka wapi, na wataweza vipi kusimamia maslah mapana ya nchi?

Swali: Maendeleo yasiyotokana na sanduku la kura halali yanawezekana kupatikana?

Chama Cha kijani kina wanachama mil 36 kwa data za mchengerwa, kwa akili ya kawaida kwanini waogope reforms kupata tume huru ya uchaguzi?

No Reforms, no Election!

Karibuni 🙏
 
Maendeleo Nje ya sanduku la kura yanategemea utashi wa kiongozi alieko madarakani.

Na hatuwezi, kuendesha nchi kwa kutegemea utashi wa Mtu mmoja ambae ni Raisi kua akiamua afanye sawa, akija boya mwingine akiamua kutokufanya, then tunasubiri mpaka aondoke.

Ni lazima sanduku la kura liheshimiwe, ili viongozi waheshimu maoni na matakwa ya CCM.

Tunataka tuwe na power yakuwatoa CCM madarakani na Kuwarudisha siku tukiwahitaji, the same tuwe na uwezo wa kuwatoa chadema na kuwarudisha siku yoyote tukiwaitaji.

Naumia sana, kipindi hiki cha mvua unapinda barabarani Zimejaaa mashimo makubwa kama hatuna uongozi.
 
Ikiwa ubunge utatakiwa kuwa mwelevu kwa kiwango kinachokaribia AI yaani Artificial Intelligence tutawahitaji.Lakini hizi kelele za sasa za ubunge si chochote
ni nafasi ya kupiga hela tu.Democracy is outdated political setup.Nashangaa watu wanashabikia bila kujua undani wa jambo.
Hata China mawakilishi ni watu wachache sana wanaochagua kwa niaba ya wengi, Maendeleo ya China mkomunisti ni mara elfu ya nchi yenye demokrasia kubwa India.China mafanikio yanaonekana bila kelele za demokrasia,mwizi wa mali ya umma mkubwa ananyongwa.
Tulichelewa kutambaa hatutaki tena kelele za vyura za 1961.
 
Back
Top Bottom