Eti STAMICO wanauza Makaa ya Mawe tani moja kwa Tsh 60,000/= Mkataba huu Uvunjwe

Hii ni kwa ROM Coal
 
Haishangazi sana maana kuna ndege iliwahi kuuzwa kwa laki tano.
 
Mama anafungua nchi
Mwendazake alifukuza wawekezaji, Mama kafungua nchi...mijimeli inabeba makaa ya mawe hadi Ulaya, Royal Tour imefanya watalii wamininike kama kumbikumbi, nani kama Mama in Makalla voice!
 
Hongera umetia neno.
 
Sio kweli,
Kama Ni hivyo basi dangote asingeagiza makaa ya mawe kutoka afrika kusini wakati Hapa ya Bei Chee yapo.
Walitaka awahonge kwanza ndo wamuuzie, Nchi ngumu hii!!
 
Inashangaza!
 
Taarifa haijakamilika naona imejaa mihemko.

Stamico na makaa ya mawe wapi na wapi?

Ingawa nahisi kwenye hii tenda walamba asali wamepiga parefi sana.

#MaendeleoHayanaChama
State Mining Corporation
 
Mada ngumu kama hii wapiga mapambio wa Hangaya hutawaona hapa.

Kuna mbunge ametahadharisha huu ufunguaji wa nchi usipofanyika kwa tahadhari utafanya nchi kuwa kama danguro.
 
Picha kipande cha mkataba tuone ama sivyo ni uzushi tu
 
Nadhani mtoa mada hujui ihalisia wa hizo bei za makaa ya mawe, hapa kwetu hiyo ni bei ila kuna ushuru na gharama nyingine juu yake, japo sio kiivyo ila zinafika elfu 30 kwa tani moja.

Pia namna ya usafirishwaji inachangia sana, by the time makaa ya mawe yanafika iwe Mtwara kwa Dangote, Tanga Cement & Rhino Cement Tanga, etc bei ya makaa inakuwa ishapaa kutoa 1.8mil kwa semi moja, hadi 6.3mil kwa semi moja. Kuna gharama kubwa sana kwenye usafiri. Sasa 6.3mil tayari bei inakuwa ipo juu.
 
Kwani waziri wa madini amekwambia za kwake ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…