Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Stamico wao wanakusanya maduhuri tuHiyo ni bei ya stamico kama mtoa mada anavyosema, stamico hajaanza kusafirisha mkaa kama sijakosea , anaye lsafirisha mkaa kwa meli hizi mbili za mwisho ni Ruvuma coal ma hasafitishi kwa bei hiyo
Mkaa una bei zake kulingana na size yake, export price ruvuma nadhan inaanzia 39usd per tonRuvuma coal , wanasafirisha kila siku tani za kutosha sijui kama bei ni hiyo na kama ni hiyo basi kuna tatizo kubwa...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aiseee hichi nacho ni kituko cha mwaka yani tani moja kwa elfu sitini jamani hii nchi hii inabidi iwe na sheria ya kunyonga kabisa!
Hivi ndio kufungua nchi huku? Hakika inachekesha na kuhuzunisha kwa wakati mmoja! Tunajisifu kwa meli kubwa eti imetia nanga kumbe makaa ya mawe ni kama yanaondoka bure kabisa na no one cares aiseeeee
Ngoja ni lale tuuu
Samia Ni mpotoshaji?Kenge ni wewe,mimi Niko hapa kukabiliana na upotoshaji wa aina yeyote wa Samia.
Ndio maana nimewaeleza hapo juu kwamba wangejua Makaa yako kila sehemu ila ni of poor quality Sana, huwezi linganisha na Botswana au South Africa..
Salaam Wakuu,
Imedaiwa Eti, Tanzania kupitia Stamico tumesaini mkataba wa kuuza Madini ya Makaa ya Mawe kwa dola 29.5 ambayo ni sawa na Shilingi 69,444 (Elfu sitini na tisa na Mia nne arobaini na nne tu) kwa Tani moja!
Bei ya Soko la Makaa ya Mawe kwenye Market Insider ni dola 315 sawa na shilingi za Kitanzania 740,250 (laki saba na elfu arobaini na mia mbili na hamsini).
Reuters wameripoti kuwa bei ya Madini ya Makaa ya Mawe inatazamiwa kupanda kwa mwaka 2022 kufikia dola za Kimarekani 500 sawa na shilingi za Kitanzania 1,175,000 (Milioni moja na laki moja na elfu sabini na tano)
Afrika Kusini wanauza makaa ya Mawe kwa bei ya Dola za Kimarekani 140.07 ambayo ni sawa na shilingi 329,164 hii ni bei iliyoporomoka toka kwenye bei ya Dola 214.27 sawa na shilingi 503,534 ya mwezi uliopita!
Ukiangalia bei ya Soko la Madini haya na wastani wa bei inaashiria dhahiri pasi na shaka kuwa Mkataba huu una viashiria vikubwa mno vya Rushwa!
Haiwezekani Madini yetu ya Makaa ya Mawe yauzwe kwa bei inayolingana na bei ya Kifusi cha Udongo/Mchanga!
Watoto na wajukuu zetu watakuta mapango na mashimo watatuuliza hapa palifanyika jambo gani?
Tukiwaambia palikuwa na Madini ya Makaa ya Mawe ambayo yaliuzwa kwa Tani elfu 69,444 watatulaani, watatutukana na kutuadhibu!
Ni heri haya Madini tuyaache vizazi vijavyo viyakute kuliko kuyachimba na kuyauza kwa Mikataba iliyojaa rushwa na Ufisadi!
Haiwezekani Mbuzi mmoja awe na thamani kubwa kuliko Tani moja ya Madini ya Makaa ya Mawe!
Naiomba Serikali kupitia vyombo vyake iuchunguze mkataba huu , iuvunje na ichukue hatua kali kwa kila aliyehusika kuruhusu Mkataba wa kifisadi kama huu ili iwe fundisho kwa watumishi wa Umma wote na wanasiasa wasio waadilifu!
Wizara ya Madini.
Napenda kupata kauli ya STAMICO ilikuwaje wakaingia huu Mkataba
Pia, soma;
Thread 'Meli nyingine iliyobeba makaa ya mawe yaondoka kutokea Mtwara kwenda Ulaya' Meli nyingine iliyobeba makaa ya mawe yaondoka kutokea Mtwara kwenda Ulaya.
View attachment 2245667
Wewe ni kajinga, upotoshaji gani?Acha upotoshaji
Kwa SamiaSamia Ni mpotoshaji?
Awamu ya 5 mlikuwa mnauza bei gani?
Laana unayo wewe maskini usijumuishe wengine
Jibu swali acha blaa blaa za kijingawewe ndio laana kutaka kujua awamu ya tano walikuingilia
Hiyo Bei mtoa mada ameipata wapi? Mbona haweki ushahidi?kaka hii ni tanzania kula kwa urefu. hiyo makaa ya mawe inauzwa bei hiyo na stamico ni danganya toto, kuna wenye nchi wanauziwa bei hiyo na wao wanapiga cha juu. tuendelee kufurahi kifo cha jpm tutajua kama sisi hatujui