Eti STAMICO wanauza Makaa ya Mawe tani moja kwa Tsh 60,000/= Mkataba huu Uvunjwe

Kama nikweli inasikitisha sana,tozo kibao halafu watu wanajichotea tu maliasili yetu
 
Inahitajika reli toka Mtwara hadi ziwa nyasa.
 
Mpaka hapa hajatokea mtaalamu kwenye hii sekta akatoa ufafanuzi. Kwa sie tusiojua kuhusu makaa ya mawe inawezekana tukaona ni kitu chenye thamani kubwa kumbe ni kitu cha kawaida kabisa. Na pia ikawa ni bidhaa inayopatikana kwa wingi duniani. Na uchimbaji wake ukawa sio wa gharama kubwa kama wengi tunavyo jaribu kufikiri.
Naamini kabisa kwenye hii mikataba kuna harufu ya upigaji lakini ukiangalia na bei za nchi nyingine tumezisiwa kwa nusu. (Kwa mujibu wa mleta mada)

Kumbe kina Mkapa RIP walipojimilikisha migodi ya kiwira walijimilikisha miradi ya kawaida kabisa. Lakini kelele zake kuuubwa.

Ningependa kuona mtaalamu kwenye hili eneo, aje atoe ufafanuzi. Sio wanasiasa na wale walamba viatu.
 
Dhambi kunyongana mkuu
 
sasa kama yanauzwa bei ya kutupwa si ukayanunue ukauze huko dola 500 kwa tani, wavunje mkataba uyanunue wewe? watu wengine sijui waliugua degedege utotoni?
 
Tani moja ya makaa ya mawe kwa bei ya mifuko mitatu ya simenti! Huku kama siyo kulogwa ni nini?
 
Uko sahihi,

Ushahidi wa bei upo wapi!?!
Je, ubora wa haya makaa ya mawe upoje!?!

Hata mkaa na kuni tu zinatofautiana bei kufuatana na aina ya mti,
Kuni za mpingo ni gharama kuliko kuni za mkaratusi,
Mkaa wa Mkorosho au Iringa. Ubora wake ni tofauti na mkaa wa miti pori!
 
Mkuu, swali kama hili siyo level yako, usijishushe kiasi hicho, please.
Bei hutegemea current market demand, haitegemei awamu ya 5 au 4 waliuza kiasi gani.
Tuna mawazo ya kisiasa Sana, very sad! Kuna vitu vipo nje ya uwezo wa wanasiasa na watawala,
Watu hatuelewi hata kuwa haya mambo yanaendana kufuatana na soko la dunia.
Nafikiri watu tuelimishwe, tokea primary, soko

Mfano, kwanini vitunguu nyanya bei hupanda na kushuka.
Kwamba waweza kufika sokoni ukakuta Kkoo nzima zipo fusso 3 Tu za nyanya, hapa bei itapanda!
Na unaweza kufika sokoni ukakuta fusso 100 za nyanya! Hapa bei inaporomoka!
 
Sio kweli,
Kama Ni hivyo basi dangote asingeagiza makaa ya mawe kutoka afrika kusini wakati Hapa ya Bei Chee yapo.
Kwani nguzo za umeme zinatoka wapi?? Je Tz hakuna nguzo?
 
Sio kweli,
Kama Ni hivyo basi dangote asingeagiza makaa ya mawe kutoka afrika kusini wakati Hapa ya Bei Chee yapo.
Bei ya bidhaa yoyote hutegemea ubora, gharama za uzalishaji na usafirishaji.
Pili chimbo letu bado jipya kuuza duniani.
Huenda ni bei ya matangazo...nawaza tu.

Tatu...niliwahi kusikia Dangote akisema kuwa anaagiza hayo makitu nje ya nchi kwasababu makaa yetu hayana ubora.
 
Stamico to the best of my knowledge anamiliki mgodi wa kiwira coal , coal ya kiwira ni moja ya coal zenye ash content kubwa na low calorific value , kiufupi ni coal dhaifu sokoni, inawezekana bei hiyo ni sahihi kulingana na ubora wa makaa yale.
 
Kwa sasa duniani sisi ndo tuna coal bora ,
 
Kwa Tsh 60,000 kwa tani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hakika nchi imefungukooooooooooooo
Hiyo ni bei ya stamico kama mtoa mada anavyosema, stamico hajaanza kusafirisha mkaa kama sijakosea , anaye lsafirisha mkaa kwa meli hizi mbili za mwisho ni Ruvuma coal ma hasafitishi kwa bei hiyo
 
Tunamshinda Mrusi?
Siwezi kujua ila sisi ndo tunaanza kuchimba , wezetu walianza siku nyingi na almost ile coal bora washamaliza , hata coal ya southern Africa ni shallow kwa ubora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…