ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Hawa wanaopanga na kufanya hii miradi Huwa wanajua wanachokifanya au wanakurupuka tuu?
Yaani Mizigo Mingi inayopita Tunduma inaenda DRC(Lubumbashi), Zambia na Zimbabwe ambako route Yao fupi ni via Tunduma..
Sasa inawezekanaje mizigo itoke Dar iende Karema then ivuke Ziwa itafute Barabara ndio iende huko nilikotaja..
Kwa Jiografia Ipi? Hivi huko Wizarani hakuna Wataalamu Hadi kufanya miradi ya kukurupuka isiyo na Tija?
Imeshindikana Kwa Bandari ya Kasanga ambayo nayo ilijengwa Kwa mabilioni na lami ikafikishwa Bandarini lakini hakuna hata Lori Moja linatumika njia hiyo na kupunguza msongamano Tunduma..
Serikali acheni blaa blaa zisizo na msingi,Jenga Sgr Dar Hadi Zambia Hadi Lubumbashi na njia zote ziwe Dual Carriage ndio walau utapunguza msongamano Tunduma sio hizo hadithi na blaa blaa zisizo na msingi.
----
Ubovu wa barabara na kutokuwepo kwa reli kutoka Mpanda kwenda Bandari ya Karema iliyopo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi imetajwa kuwa sababu ya bandari hiyo kuzorota kinyume na matarajio.
Akizungumza mara baada ya kuzuru mradi huo wa kimkakati wa bandari ya Karema, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Silaa, amesema tangu ilipofunguliwa rasmi mwezi Septemba 2022 hadi sasa, bandari hiyo imeingiza kiasi cha shilingi milioni nne na laki nane tu ambazo amesema ni kiasi kidogo ukilinganisha na uwekezaji uliofanyika wa shilingi Bilioni 47.97
Amesema kukamilika kwa miundombinu hiyo itasaidia malori yanayopeleka mizigo DRC badala ya kupitia Tunduma yatapitia Mpanda hadi Karema na baada ya kufika Bandari ya Karema ni rahisi kufika Bandari ya Karemii iliyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na baadaye Lubumbashi, jimbo kubwa la kibiashara nchini humo.
Silaa amesema Mpango wa serikali uliopo sasa ni kujenga barabara ya kilomita 110 kutoka Kijiji cha Kagwira hadi bandari ya Karema pamoja na kujenga reli kutoka Mpanda hadi Karema.
Ujenzi wa mradi wa Bandari ya Karema uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 47.97, ulianza kutekelezwa Oktoba 2019 na kukamilika mei 2022 na kuanza kazi rasmi Septemba 2022