BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Baada ya USB-C kulazimika kuwa ndio port ambayo itakuwa katika simu zote duniani na kampuni kama Apple kukubali kuanza kutengeneza iPhone ambazo zitakuwa na port na cable ya USB-C; kinachofuata ni replaceable batteries.
๐ฅ๐ฒ๐ฝ๐น๐ฎ๐ฐ๐ฒ๐ฎ๐ฏ๐น๐ฒ ๐๐ฎ๐๐๐ฒ๐ฟ๐ถ๐ฒ๐ ๐ป๐ถ ๐ป๐ถ๐ป๐ถ?
Kwa wale ambao wameanza kutumia simu tangu miaka ya zamani, watakuwa wanakumbuka betri za zamani katika simu zilikuwa ni rahisi kuifungua simu na kuibadilisha betri. Enzi hizo aina ya betri hizo zilikuwa zinaitwa replaceable batteries (au pia kwa majina mengine ni user-replaceable au user-serviceable batteries). Ni betri ambazo zinatoka na kubadilisha kwenye simu bila kulazimika kuifungua simu yote au kupeleka simu kwa fundi.
๐๐ ๐ช๐ฎ๐ฆ๐ด๐ฆ๐ฎ๐ข ๐ฏ๐ช ๐ญ๐ข๐ป๐ช๐ฎ๐ข ๐ฃ๐ฆ๐ต๐ณ๐ช ๐ป๐ฐ๐ต๐ฆ ๐ป๐ช๐ธ๐ฆ ๐ป๐ช๐ฏ๐ข๐ธ๐ฆ๐ป๐ข ๐ฌ๐ถ๐ฃ๐ข๐ฅ๐ช๐ญ๐ช๐ด๐ฉ๐ช๐ฌ๐ข!
Kwanini Betri zimekuwa zinafungwa na cover na haziwezi kubadilishika?
1๏ธโฃ Kuhakikisha maji hayaingii kwenye simu
2๏ธโฃ Kulazimisha betri ikiharibika watumiaji walazimike kununua betri nyingine
3๏ธโฃ Kulazimisha watu wasiweke ufundi wao wenyewe hivyo walazimike kwenda kwa mafundi ili kubadilisha betri
Umoja wa nchi za Ulaya umetoa Miaka 3 na Nusu kwa makampuni ya simu kuweka cover za simu ambazo zitaruhusu mtumiaji kufungua na kubadili betri yeye mwenyewe. Pia kampuni za simu zimelazimishwa ziweke muundo ambao bado hautaruhusu maji kuingia kwenye simu endapo kama mtu hatafungua simu yake.
Kampuni kama Apple, Samsung, Google zitalazimika kuweka utaratibu huo. Lakini kampuni kama Xioami tayari imeamua itakuwa inatengeneza brands tofauti kuendana na masoko mfano itakuwa na simu zake maalum kwa ajili ya EU na mabara mengine yataendelea kutumia design yake ambao sio lazima ifanane na EU.