Wewe unafurahia nchi yako kukemewa kwa jambo ambalo halina msingi???!!! Kukemewa siyo issue...hoja hapa ni kuwa unakemea kitu gani au jambo gani???!!! Tanzania tumefanya kosa lipi mpaka tukemewe....Je, Marekani amekemewa wapi??!! Pale alipokiuka sheria za kimataifa kwa kuivamia Irak bila ruhusa ya Umoja wa Mataifa alifanywa nini??? Je, Uingereza ilikuwa sahihi kumuua Sadam Hussein??!! Je, Marekani na washirika wake walikuwa sahihi kumuua Ghadafi??!! Je, silaha za maangamizi huko Irak zilipatikana baada ya uvamizi ule wa kinyama??? Je, unajua ni nchi gani inayomiliki silaha nyingi kwa maelfu ya matani?? N i Marekani...Sasa Marekani inataka yenyewe ndiyo iwe na mamlaka ya kutumia silaha za kemikali na siyo mwingine...Je, unajua ni nchi gani iliyowahi kutumia silaha za nyuklia?? Ni Marekani, na ilitumia huko Japan ambako watu kwa maelfu walikufa na mpaka leo kiziazi kingine kinaendelea kufa kwa magonjwa ya kansa yanayotokana na bomu la nyuklia...Je, unajua ni nchi gani imewahi kutumia silaha za sumu na kuua maelfu ya watu?? Ni Marekani, ambayo ilitumia silaha za sumu katika vita vya Vietnam miaka ya 1960 kwa kumimina mabomu ya napalm katika miji ya Vietnam....Je, unajua ni nchi gani iliyokithiri kwa ubaguzi wa rangi?? Ni Marekani, ambako mpaka miaka ya 1960 weusi walikuwa na shule zao, migahawa yao na vyombo vyao vya usafiri vya umma tofauti na wazungu..na mpaka leo ingawa ubaguzi huo umetokomezwa na tunaambiwa hivyo lakini mabaki ya ubaguzi bado yapo huko Marekani...Je, unajua kuhusu mauaji kwa raia yanayoendelea huko Marekani??