EU yaizuia Tanzania na yaziruhusu Rwanda na Uganda kuingia kwao

EU yaizuia Tanzania na yaziruhusu Rwanda na Uganda kuingia kwao

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,266
Reaction score
25,555
Umoja wa Ulaya umetoa taarifa kwa mataifa kadhaa ambayo raia wake wanaweza kupata Visa kuingia nchi Wanachama wa umoja huo huku zitizuia raia wa baadhi ya mataifa ikiwepo Tanzania kutoruhusu raia wake kupata Visa.

Hayo yamejiri kutokana na hatua stahiki zinazochukuliwa na mataifa hayo dhidi ya gonjwa la corona kwa kuwaweka lockdown kama siyo lockup na kusababisha kuenea kwa kasi hali ambayo inaweza kuwa ni tofauti na uharisia.

Vilevile marekani ikiwepo Brazil nazo zimewekwa kundi moia na mataifa mengine ya bara la Afrika kama Burundi nk.

Kutokana na hilo kutotoa taarifa au kuchukua hatua zaidi imekuwa ni chanzo kwa mataifa mbalimbali kukosa kupewa visa raia wake mpaka hapo kutakapotolewa taarifa nyingine.
 
Nchi itakayoondoa lockdown baada ya kuitokomeza Covid19 100% ndo ilete mbwembwe. Marekani wananchi wako kwenye maandamano, Trump yuko kwenye kampeni bila barakoa halafu EU inajitutumua na ukoloni wa kimaskini.
 
Ujue Wazungu walivyo wanafiki

Wameruhusa USA na Brazil kuingia Ulaya ila Nchi nyingi za Africa hazijaruhusiwa

Tukumbuke Brazil na USA ndio zimeathirika zaidi na malaria
Brazil na USA zimezingatia "pandemic data publication" protocol.
Tanzania sijui ipo sayari gani isijue vitu basic kama hivi!
 
Waache upuuzi hawa kuna kitu wanakitafuta!.. hivi unatangaza maambukizi halafu hauna dawa Wala kinga ndo unini..??
Mi sifikirii dhana ya kutangaza ndo stahiki maana mwisho wasiku utangaze usitangaze kama dawa huna au kinga bado utaathirika tu!!..
Kilichobaki ni kuvaa barakoa na kutumia sanitizer but still watu wanaongezeka!.. sahivi marekani maambukizi yameongezeka mpk mzee baba trump kaanza kusema spidi ya upimaji ipunguzwe!!..

Taarifa hii na itufumbue waafrika kuwa cha mtu mavi na kwenu ni kutamu kushinda popote!.. tujenge nchi zetu.
 
hivi hawa EU wana nini mpaka sisi donor country tujipendekeze kwao
 
Back
Top Bottom