Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Sisi Ureno mechi na Ujerumani tutaua mtu
sisi wareno wa tandahimba hatuna sababu ya kushindwa kutetea ubingwa wa euro kama walivyofanya spain, adui yetu mkubwa tunayemuogopa ni kocha wetu anayeitwa Fernando Santos mwenye nidhamu ya uoga ndani yake.
Unalindwa na ukuta unaoongozwa na pepe, ruben diaz, rui patricio, semedo mpaka hapo sielewi mantiki ya kulazimisha mfumo wa kucheza na double pivot ya danilo na william carvalho (wote hao wana mlingano mkubwa sana wa kiuchezaji)

wachezaji waliopo benchi wenye ubora
  1. João Moutinho (8) = playmaker wa uhakika
  2. Renato Sanches (16)
  3. Rúben Neves (18)
  4. Pedro Gonçalves (19) = likumbuke hili jina
  5. André Silva (9)= mshambuliaji wa uhakika
  6. João Félix (23)v= hakuna asiyemfahamu
ukitaka kushuhudia kivumbi cha wanaume subiria mechi ya france
 
Danilo nitamuangalia tena kesho vs Germany..game ile ya Hungary alinikosha sana.
 
Sisi wa [emoji629] tutawachapa nyie [emoji1201] kichapo cha mbwa koko.
 
Naungana na ww, kiukwel huyo kocha anatukosea sana. Mchezo dhidi ya Hungary nilishangaa sana kile kikosi, Joao Felix hivi kwann hakupata nafasi ata ya kucheza? Kwann kocha alimkata Joao Cancelo kuelekea michuano hii?

Kiukwel Ureno wana kikosi kizuri mno kule mbele wana washambuliaji hatari sana. Cristiano Ronaldo, Joao Felix, Diogo Jota, Andre Silva na Bwana mdogo Pedro Goncalves. Huyo Andre Silva we msikie hivyo hivyo ila ana balaa lake. Kocha inabidi abadilike katika mbinu maana ana wachezaji wazuri shida ni namna ya kuwatumia.
 
Cancelo aliumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…