Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

4-3-3 haina namba [emoji647] [emoji849] kivipi chief?[emoji848] Unazungumzia namba 10 kwemye formation ama kimajukumu.. Kimajukumu namba 10 yupo uwanjani.
 
4-3-3 haina namba [emoji647] [emoji849] kivipi chief?[emoji848] Unazungumzia namba 10 kwemye formation ama kimajukumu.. Kimajukumu namba 10 yupo uwanjani.


4-3-3 inakuwa na mabeki 4, midfield 3 na striker 3, yenyewe nayo ina variation zake. Ila waliyocheza Portugal jana midfield ilikuwa palinha, renato na moutinho..

Palinha kama CDM na mbele yake Kuna Moutinho na Renato kama CM.

Mfumo huu hakuna attacking midfielder ama no 10,

Bernardo Alikuwa winga/forward wa kulia na Jota same role kushoto.

Hivyo huu mfumo hauna nafasi kwa Bruno, Joao Felix, na hata Huyo Bernardo.
 
Na hiki ndio kiliwaponza jana Ureno, kocha alifeli kimajukumu hawakuwa na namba [emoji647] uwanjani, ndio maana walikuwa wanacjeza vizuri wakifika kwenye robo ya adui, wanakosa mipango yakinifu, wanaishia kupiga krosi tu. Ni kosa la kocha wao.

Huwezi kucheza na timu bila nambari 10,labda wapinzani wawe na mapungufu fulani.
 
Zipo timu zinacheza hivi Sema Kuna Aina fulani fulani za wachezaji wanaijua hii mifumo, mfano Barca ya Enrique ina messi kulia, Neymar kushoto, Iniesta midfield wa kushoto wote hawa ni creators wazuri, hivyo unacheza vizuri bila dedicated 10. pia mfumo huu unataka mabeki wanaopanda vizuri.

Ila portugal wao hawana watu hao, mentality ya kocha haina tofauti na 2016 bado anafikiri wao ni underdog anajihami zaidi na kujaza wakabaji wa kutosha kila eneo. Angecheza tu 4-2-3-1 Ronaldo mbele nyuma yake awaeke kina Bruno, silva na Felix hata double pivot akikaa palinha na renato mbele uhakika upo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…