EV zina gharama ndogo za uendeshaji kuliko magari ya ICE. Sema ngumu sana kumshawishi Mtanzania

EV zina gharama ndogo za uendeshaji kuliko magari ya ICE. Sema ngumu sana kumshawishi Mtanzania

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Wakuu, nimekutana na mjadala wa magari ya EV (electric vehicles) vs ICE (internal combustion engine) kwamba ipi ni afadhali kwa mtu mwenye mizunguko mingi (~km 50 hivi kwa siku). Mabishano yakikua kwenye issue kuu tatu, gharama za matengenezo, uendeshaji na uwoga wa battery kuchakaa.

Najua kwa hapa Tanzania bado ni ngumu kumshawishi mtu kwamba EV ni nafuu zaidi kuliko magari ya engine. Tukiachana na gharama za kununua, tuangalie kwa mifano halisi ya magari matatu, yote ya mwaka mmoja:
  • Tesla Model 3 (EV 2020)
    IMG_2008.jpeg
  • Toyota Corolla 2020 (ICE)
    IMG_2009.jpeg
  • BMW 3 Series 2020 (ICE)
    IMG_2010.jpeg
Kwa kila sekta, EV atashinda kihurahisi sana, na hapa nitaeleza kwanini:

1. Tukianza na Gharama za Matengenezo.
  • Tesla Model 3 (EV)
    • Ina moving parts chache, wastani wa 20–30 tu kwenye drivetrain.
      IMG_2011.jpeg
    • Hakuna pistoni, valves, crankshaft, timing belt, turbo, gearbox yenye gears nyingi, fuel pump, oil pump, exhaust system.
    • Matengenezo makubwa yanabaki kwenye brakes, suspension, tyres na fluids ndogo za cooling.

  • Toyota Corolla (ICE)
    • Ina moving parts wastani wa 800–1,500 hivi.
      IMG_2007.jpeg
    • Kila pistoni, valve, crankshaft, camshaft, gear, turbo (kwa baadhi ya trims) zote zinahesabiwa kwenye hizi moving parts.
    • Kila sehemu inahitaji service: engine oil, plugs, filters, timing chain/belt, na gearbox oil (hasa CVT).

  • BMW 3 Series (ICE)
    • Ina moving parts nyingi zaidi, mambo ya Germany Engineering, wastani wa 1,000–2,000+, kwa sababu ya turbo, gearbox complex (ZF 8HP), pumps nyingi, sensors, n.k.
      IMG_2006.jpeg
    • Matengenezo yake ni magumu na ghali zaidi ukilinganisha na Corolla.
IMG_2004.jpeg

Kila sehemu inayosogea (moving part) = sehemu inayoweza kuharibika. Ndiyo maana EV zina advantage kubwa.

2. Gharama ya Mafuta vs Umeme (Tuta assume unaendesha km 50 kwa siku, kwa muda wa miaka 2)
  • Umbali wa miaka 2:
    • 50 km × 365 siku = 18,250 km kwa mwaka
    • Miaka 2 = 36,500 km jumla

Tesla Model 3 (EV)
  • Range: base model ina range ya 400 km kwa full charge (60 kWh battery)
  • Hii ni kama kusema 6.6 km/unit.
  • Kwahiyo kilometa 50 kwa siku, ni sawa na 50 km/6.6 =7.576 units.
  • Kwa gharama ya unit 1 = Tsh 350 ni sawa na Tsh 2,650 kwa siku.
  • Miaka 2 (730 siku) = 1,935,000 Tsh

Toyota Corolla 2020 (ICE)
  • Consumption: 15 km/l (kwa hizi foleni za Dar)
  • 50 km = ~3.3 lita × 3,300 Tsh = 10,890 Tsh kwa siku
  • Miaka 2 = 7,954,000 Tsh
BMW 3 Series 2020 (ICE, 2.0L Turbo)
  • Consumption: ~12 km/l
  • 50 km = ~4.2 lita × 3,300 Tsh = 13,860 Tsh kwa siku
  • Miaka 2 = 10,117,000 Tsh
Hii inamaanisha EV ni nafuu mara 4–5 zaidi kwenye gharama za kuendesha gari kwenye issue ya mafuta.

3. Gharama za Service (36,500 km kwa Miaka 2)
  • Tesla Model 3
    • Hakuna engine oil (ambayo ndio service kubwa kwa ICE)
    • Hakuna gearbox oil (inatumia single reduction gear)
    • Brakes zake zinadumu muda mrefu kwa sababu ya regenerative braking
    • Service ndogo tu: rotation ya tyres, coolant check, cabin filter
    • Nitakadiria: chini ya 1 million Tsh kwa miaka 2

  • Toyota Corolla
    • Oil service kila 5,000–10,000 km = kwahiyo wastani wa 5–7 service kwa 36,500 km
    • Kila service andaa 200k Tsh (oil, filter, fundi), jumla ~1.2M Tsh
    • Brake pads zitabadilishwa angalau mara 1 kwa iyo miaka 200k Tsh
    • Gearbox CVT oil angalau mara moja, andaa 500k Tsh
    • Jumla: ~1.9M Tsh

  • BMW 3 Series
    • Oil service (synthetic) × ~7 = ~2.5M Tsh
    • Brake pads (mbele + nyuma) ~1M Tsh
    • Gearbox oil service (ZF 8HP) ~1.2M Tsh
    • Vitu vingine vinavyoweza taka service (sensors, turbo hoses, filters) ~2M Tsh
    • Jumla: ~6.5M Tsh
Hapa pia tunaona EV inamatengenezo madogo zaidi kwasababu ni vitu vichache binahitaji service.

4. Battery Life (Kwa mazingira ya Dar es Salaam)

Hofu kubwa tuliyonayo hapa ni battery zikichakaa gharama kubwa kuinunua mpya. Ni kweli. Ila kuna vitu tucheki hapa:
  • Tesla Model 3 warranty miaka 8 au 160,000–192,000 km.
  • Zinaweza kufika 300,000–500,000 km kabla capacity kushuka sana.
  • BYD na Toyota EVs (LFP batteries) zinaweza fika zaidi ya 500,000 km.

Mazinga ya Dar es Salaam (joto na humidity):
  • Joto kali hupunguza ufanisi wa battery, lakini EV za kisasa zina thermal management systems (liquid cooling) zinazolinda battery isi-overheat.
  • Tatizo kubwa litakuwa kwa cheap EVs zisizo na cooling nzuri (hasa zile ndogo za Kichina).
  • Njia ya kujilinda: usiache gari juani muda mrefu, hakikisha software updates zinatumika kudhibiti charging & discharging.

Kwa miaka 2, Tesla Model 3 inaweza kukuokoa ~6M Tsh ukilinganisha na Corolla, na karibu ~9M Tsh ukilinganisha na BMW, kwenye fuel/umeme tu.

Ukijumlisha service, gap linakuwa kubwa zaidi.

Hafu battery sio tishio kubwa kama inavyodhaniwa: zinaweza kudumu zaidi ya miaka 8–10 bila shida kubwa, hata kwenye joto la Dar es Salaam.
 
Mimi Nina uhakika kuwa haya magari tutanunua Tu kumbuka Sisi wabongo hatuna maisha ya kujilipua mpaka tuone watanzania wenzetu wanaendesha barabarani.

Wengi tutanunua magari Kwa kusikia , kwahiyo hata hizo EVs tukianza kuziona mtaani tutaingia Tu. Kumbuka mabus ya kichina kipindi yanaingia kila MTU aliponda ila sikuhizi Hadi serikalini yapo
 
So interesting

Na hiyo gharama ya betri inayohofiwa ikoje mkuu, lakini pia hivi namna ya kulipia huo umeme ni kama tunavyolipia luku majumbani😁 au imekaaje? Mbona kwa hayo maelezo kama EV ni much better option, vipi huko kwa wenzetu inaonekana washaachana na ICE au nako bado haijachanganya, ukiachana na Tesla kampuni gani nyengine ni machaguo rafiki
 
Shukrani mkuu, maswali mazuri na fikirishi.

1. Kusema kweli gharama za battery ni kubwa, ni kama useme gari lako unabadirisha engine. Kwahiyo expect kuanzia Mil 5-10 kutegemea na gari. Kwa mfano Tesla Model 3 nilioitolea mfano kwenye mada hapo juu, battery yake mpya ni zaidi ya $10,000. Ukipata used ni $3,000 hadi $6,000.

Ila kuna option ya kufix battery incase ikizngua. Yaani ni hivi, battery inaundwa na modules (cells) kwahiyo tukisema battery imezingua ni baadhi ya cells zimezingua.

Mfano mdogo chukulia battery ni kreti la soda, hafu zile chupa ndio cells. Kwahiyo hauwezi sema kreti limeharibika kwahiyo la kutupa, ila kuna chupa zimepasuka na zingine nzima. Kwahiyo kurudisha kreti kwenye matumizi tuna replace zile chupa tu. Hapa bei inaweza kua ndogo ata 1/3 ya bei ya battery used.

2. Kuhusu umeme wa kuchaji, yes, haya magari unachaji home kwako (au nyumba ya kupanga) kama unavyochaji simu, saa, pikipiki, etc.

Ila kama unataka maelezo zaidi, kuna aina tatu za charging system zinaitwa Level (Level 1, 2 na 3). Nitajaribu kusimplify.

Level 1 ni umeme wa nyumbani, kama ambao unatumia kuchomeka TV, friji, subwoofer, iPhone yako nk. Hii ni slow charger inakupa kama km 5 hadi 20 hivi kwa saa ukichaji, kutegemea na uwezo wa gari.

Level 2 ni umeme pia wa majumbani, nao same volts 230 kama L1, ila wenyewe una current kubwa zaidi ya L1 kwahiyo kidogo ni fast charger. Hii itakupa 40 hadi 120 km kwa kila saa unayochaji kutegemea na gari.

Level 3 sasa ni DC fast charger. Hii unakuta inapiga hadi km 200 ndani ya saa 1 la kuchaji. Hizi hauzikuti majumbani. Unazikuta njiani, mitaani au kwenye commercial buildings mfano Mlimani City. Hizi unachaji na kulipia pale pale kutegemea umechaji asilimia ngapi.

Level 1 hauhitaji anything unavyochaji ni kama tu unaunganisha waya kutoka kwenye soketi hadi gari ila Level 2 utatakiwa uweke special box ya kuchajia. Fundi yoyote wa umeme anakuwekea zipo kuanzia 500k Tsh na kuendelea.

Kwahiyo nikirudi kwenye swali, matumizi ya umeme ni haya haya kama ya home, na unajaza LUKU kawaida kabisa.

3. Wenzetu EV zinakua kwa kasi sana kwasababu nyingi, moja wapo miundo mbinu (mfano charging systems), mafundi, nk lakini pia serikali ina support EV technology kwa kupunguza kodi na support viwanda.

Kuna baadhi ya Mataifa kufika 2035 ni marufuku kununua gari la ICE jipya na ya zamani yanawekewa masharti magumu.

Sisi bado serikali haijakazia. Ushuru wa magari ya EV ni wa moto kama ICE tu.

4. Kila kampuni sasa hivi wana EV kuanzia Toyota, Subaru, Nissan, Honda, BMW, Mazda nk. Makampuni yote.

Kwa maisha yetu, EV nzuri ya kuanzia ni Nissan Leaf wanazo mbili first generation na second (Third gen ipo ila bado haijaanza kuuzwa hadi mwakani 2026). Hii was my dream car ila ushuru walikataa kushusha so nimeweka kiporo.

Kwanini nasema Nissan Leaf, kwasababu bei ya kununua JP ni rafiki, chini ya $6,500 unapata second generation ya 2019 safi kabisa. Ushuru kidogo wamoto kama Mil 20 hivi.

Hasara kubwa ya hii gari ni battery dogo, 40 kWh ikiwa full inakupa kilometa 350 hivi tu.

Ni nzuri kama misele ya mjini tu ila ukisema unaenda Dar to Moro inabidi uwe na uhakika wa kuchaji kabla haujarudi.

Ila, kama haujataka EV direct kuna options mbili naweza sema zifuatilie. Hizi ni kama daraja la kufanya transition ya kutoka ICE kwenda EV:

1. PHEV - Plugin Hybrid Electric Vehicle
Hizi ni hybrid (gari za engine na battery) ila za kuchaji mfano Toyota Prius (sio zote) na Mitsubishi Outlander PHEV. Hizi unaweza tembelea hadi km 60 kwa umeme tu.

2. Nissan e-power hybrid
Nissan wana hybrid zao zinaitwa e-power hybrid, tamu sana. Ni kama EV kwasababu pamoja na kua zina engine ila engine haitembezi matairi ila inachaji battery na motor ndio inatembeza matairi kama EV.

Sorry nimejibu kwa urefu sana.
 
Vipi kuhusu tofauti ya bei ya kununua?
Ev inaweza kuwa imeshakava tofauti ya bei kwa muda huo wa miaka miwili?

Na vipi pia kuhusu power hasa kwenye kupanda milima, Evs zinaweza kuperform vizuri?
Pamoja mkuu.

1. Hapo kwenye bei ya kununua ICE vs EV umeongea kitu cha msingi. Mfano Tesla Mode 3 ya 2022 bila Mil 60 kupata ngumu sana. Ni kweli ndani ya miaka miwili haitakua umesave kitu labda tufananishe na gari kama BMW ya 2022 kidogo bei zitafanana za kununulia.

Ila kuna EV ambazo sio za bei ya moto sana mfano wangu mkuu ni Nissan Leaf. Unaweza kuzipata kwa bei ata ya Mil 30 kushuka na izo ni za 2019 ukitaka first generation za 2016 kurudi nyuma izo ata kwa Mil 15 unazipata.

2. Kuhusu power, EV zina acceleration kubwa kuliko ICE kwasababu zenyewe zinaendeshwa kwa mota, hazina gear. Pia kwenye milima ina perform vizuri na (au) ata zaidi ya ICE.

Kufupisha jibu, sabau kuu ni mbili: instant torque na single gear speed.
 
Mimi Nina uhakika kuwa haya magari tutanunua Tu kumbuka Sisi wabongo hatuna maisha ya kujilipua mpaka tuone watanzania wenzetu wanaendesha barabarani.

Wengi tutanunua magari Kwa kusikia , kwahiyo hata hizo EVs tukianza kuziona mtaani tutaingia Tu. Kumbuka mabus ya kichina kipindi yanaingia kila MTU aliponda ila sikuhizi Hadi serikalini yapo
Yeah sisi wagumu sana kubadirika. Nawaza nani tajiri ajilipue swala na mafundi na spea litakuja tu machuma yakianza kuzurura.
 
Wakuu, nimekutana na mjadala wa magari ya EV (electric vehicles) vs ICE (internal combustion engine) kwamba ipi ni afadhali kwa mtu mwenye mizunguko mingi (~km 50 hivi kwa siku). Mabishano yakikua kwenye issue kuu tatu, gharama za matengenezo, uendeshaji na uwoga wa battery kuchakaa.

Najua kwa hapa Tanzania bado ni ngumu kumshawishi mtu kwamba EV ni nafuu zaidi kuliko magari ya engine. Tukiachana na gharama za kununua, tuangalie kwa mifano halisi ya magari matatu, yote ya mwaka mmoja:
Kwa kila sekta, EV atashinda kihurahisi sana, na hapa nitaeleza kwanini:

1. Tukianza na Gharama za Matengenezo.
  • Tesla Model 3 (EV)
    • Ina moving parts chache, wastani wa 20–30 tu kwenye drivetrain.View attachment 3452503
    • Hakuna pistoni, valves, crankshaft, timing belt, turbo, gearbox yenye gears nyingi, fuel pump, oil pump, exhaust system.
    • Matengenezo makubwa yanabaki kwenye brakes, suspension, tyres na fluids ndogo za cooling.

  • Toyota Corolla (ICE)
    • Ina moving parts wastani wa 800–1,500 hivi.View attachment 3452504
    • Kila pistoni, valve, crankshaft, camshaft, gear, turbo (kwa baadhi ya trims) zote zinahesabiwa kwenye hizi moving parts.
    • Kila sehemu inahitaji service: engine oil, plugs, filters, timing chain/belt, na gearbox oil (hasa CVT).

  • BMW 3 Series (ICE)
    • Ina moving parts nyingi zaidi, mambo ya Germany Engineering, wastani wa 1,000–2,000+, kwa sababu ya turbo, gearbox complex (ZF 8HP), pumps nyingi, sensors, n.k.View attachment 3452505
    • Matengenezo yake ni magumu na ghali zaidi ukilinganisha na Corolla.
View attachment 3452507
Kila sehemu inayosogea (moving part) = sehemu inayoweza kuharibika. Ndiyo maana EV zina advantage kubwa.

2. Gharama ya Mafuta vs Umeme (Tuta assume unaendesha km 50 kwa siku, kwa muda wa miaka 2)
  • Umbali wa miaka 2:
    • 50 km × 365 siku = 18,250 km kwa mwaka
    • Miaka 2 = 36,500 km jumla

Tesla Model 3 (EV)
  • Range: base model ina range ya 400 km kwa full charge (60 kWh battery)
  • Hii ni kama kusema 6.6 km/unit.
  • Kwahiyo kilometa 50 kwa siku, ni sawa na 50 km/6.6 =7.576 units.
  • Kwa gharama ya unit 1 = Tsh 350 ni sawa na Tsh 2,650 kwa siku.
  • Miaka 2 (730 siku) = 1,935,000 Tsh

Toyota Corolla 2020 (ICE)
  • Consumption: 15 km/l (kwa hizi foleni za Dar)
  • 50 km = ~3.3 lita × 3,300 Tsh = 10,890 Tsh kwa siku
  • Miaka 2 = 7,954,000 Tsh
BMW 3 Series 2020 (ICE, 2.0L Turbo)
  • Consumption: ~12 km/l
  • 50 km = ~4.2 lita × 3,300 Tsh = 13,860 Tsh kwa siku
  • Miaka 2 = 10,117,000 Tsh
Hii inamaanisha EV ni nafuu mara 4–5 zaidi kwenye gharama za kuendesha gari kwenye issue ya mafuta.

3. Gharama za Service (36,500 km kwa Miaka 2)
  • Tesla Model 3
    • Hakuna engine oil (ambayo ndio service kubwa kwa ICE)
    • Hakuna gearbox oil (inatumia single reduction gear)
    • Brakes zake zinadumu muda mrefu kwa sababu ya regenerative braking
    • Service ndogo tu: rotation ya tyres, coolant check, cabin filter
    • Nitakadiria: chini ya 1 million Tsh kwa miaka 2

  • Toyota Corolla
    • Oil service kila 5,000–10,000 km = kwahiyo wastani wa 5–7 service kwa 36,500 km
    • Kila service andaa 200k Tsh (oil, filter, fundi), jumla ~1.2M Tsh
    • Brake pads zitabadilishwa angalau mara 1 kwa iyo miaka 200k Tsh
    • Gearbox CVT oil angalau mara moja, andaa 500k Tsh
    • Jumla: ~1.9M Tsh

  • BMW 3 Series
    • Oil service (synthetic) × ~7 = ~2.5M Tsh
    • Brake pads (mbele + nyuma) ~1M Tsh
    • Gearbox oil service (ZF 8HP) ~1.2M Tsh
    • Vitu vingine vinavyoweza taka service (sensors, turbo hoses, filters) ~2M Tsh
    • Jumla: ~6.5M Tsh
Hapa pia tunaona EV inamatengenezo madogo zaidi kwasababu ni vitu vichache binahitaji service.

4. Battery Life (Kwa mazingira ya Dar es Salaam)

Hofu kubwa tuliyonayo hapa ni battery zikichakaa gharama kubwa kuinunua mpya. Ni kweli. Ila kuna vitu tucheki hapa:
  • Tesla Model 3 warranty miaka 8 au 160,000–192,000 km.
  • Zinaweza kufika 300,000–500,000 km kabla capacity kushuka sana.
  • BYD na Toyota EVs (LFP batteries) zinaweza fika zaidi ya 500,000 km.

Mazinga ya Dar es Salaam (joto na humidity):
  • Joto kali hupunguza ufanisi wa battery, lakini EV za kisasa zina thermal management systems (liquid cooling) zinazolinda battery isi-overheat.
  • Tatizo kubwa litakuwa kwa cheap EVs zisizo na cooling nzuri (hasa zile ndogo za Kichina).
  • Njia ya kujilinda: usiache gari juani muda mrefu, hakikisha software updates zinatumika kudhibiti charging & discharging.

Kwa miaka 2, Tesla Model 3 inaweza kukuokoa ~6M Tsh ukilinganisha na Corolla, na karibu ~9M Tsh ukilinganisha na BMW, kwenye fuel/umeme tu.

Ukijumlisha service, gap linakuwa kubwa zaidi.

Hafu battery sio tishio kubwa kama inavyodhaniwa: zinaweza kudumu zaidi ya miaka 8–10 bila shida kubwa, hata kwenye joto la Dar es Salaam.
Acha kutuharibia biashara wenye sheli.
 
Back
Top Bottom