EV zina gharama ndogo za uendeshaji kuliko magari ya ICE. Sema ngumu sana kumshawishi Mtanzania

EV zina gharama ndogo za uendeshaji kuliko magari ya ICE. Sema ngumu sana kumshawishi Mtanzania

Shukrani mkuu, maswali mazuri na fikirishi.

1. Kusema kweli gharama za battery ni kubwa, ni kama useme gari lako unabadirisha engine. Kwahiyo expect kuanzia Mil 5-10 kutegemea na gari. Kwa mfano Tesla Model 3 nilioitolea mfano kwenye mada hapo juu, battery yake mpya ni zaidi ya $10,000. Ukipata used ni $3,000 hadi $6,000.

Ila kuna option ya kufix battery incase ikizngua. Yaani ni hivi, battery inaundwa na modules (cells) kwahiyo tukisema battery imezingua ni baadhi ya cells zimezingua.

Mfano mdogo chukulia battery ni kreti la soda, hafu zile chupa ndio cells. Kwahiyo hauwezi sema kreti limeharibika kwahiyo la kutupa, ila kuna chupa zimepasuka na zingine nzima. Kwahiyo kurudisha kreti kwenye matumizi tuna replace zile chupa tu. Hapa bei inaweza kua ndogo ata 1/3 ya bei ya battery used.

2. Kuhusu umeme wa kuchaji, yes, haya magari unachaji home kwako (au nyumba ya kupanga) kama unavyochaji simu, saa, pikipiki, etc.

Ila kama unataka maelezo zaidi, kuna aina tatu za charging system zinaitwa Level (Level 1, 2 na 3). Nitajaribu kusimplify.

Level 1 ni umeme wa nyumbani, kama ambao unatumia kuchomeka TV, friji, subwoofer, iPhone yako nk. Hii ni slow charger inakupa kama km 5 hadi 20 hivi kwa saa ukichaji, kutegemea na uwezo wa gari.

Level 2 ni umeme pia wa majumbani, nao same volts 230 kama L1, ila wenyewe una current kubwa zaidi ya L1 kwahiyo kidogo ni fast charger. Hii itakupa 40 hadi 120 km kwa kila saa unayochaji kutegemea na gari.

Level 3 sasa ni DC fast charger. Hii unakuta inapiga hadi km 200 ndani ya saa 1 la kuchaji. Hizi hauzikuti majumbani. Unazikuta njiani, mitaani au kwenye commercial buildings mfano Mlimani City. Hizi unachaji na kulipia pale pale kutegemea umechaji asilimia ngapi.

Level 1 hauhitaji anything unavyochaji ni kama tu unaunganisha waya kutoka kwenye soketi hadi gari ila Level 2 utatakiwa uweke special box ya kuchajia. Fundi yoyote wa umeme anakuwekea zipo kuanzia 500k Tsh na kuendelea.

Kwahiyo nikirudi kwenye swali, matumizi ya umeme ni haya haya kama ya home, na unajaza LUKU kawaida kabisa.

3. Wenzetu EV zinakua kwa kasi sana kwasababu nyingi, moja wapo miundo mbinu (mfano charging systems), mafundi, nk lakini pia serikali ina support EV technology kwa kupunguza kodi na support viwanda.

Kuna baadhi ya Mataifa kufika 2035 ni marufuku kununua gari la ICE jipya na ya zamani yanawekewa masharti magumu.

Sisi bado serikali haijakazia. Ushuru wa magari ya EV ni wa moto kama ICE tu.

4. Kila kampuni sasa hivi wana EV kuanzia Toyota, Subaru, Nissan, Honda, BMW, Mazda nk. Makampuni yote.

Kwa maisha yetu, EV nzuri ya kuanzia ni Nissan Leaf wanazo mbili first generation na second (Third gen ipo ila bado haijaanza kuuzwa hadi mwakani 2026). Hii was my dream car ila ushuru walikataa kushusha so nimeweka kiporo.

Kwanini nasema Nissan Leaf, kwasababu bei ya kununua JP ni rafiki, chini ya $6,500 unapata second generation ya 2019 safi kabisa. Ushuru kidogo wamoto kama Mil 20 hivi.

Hasara kubwa ya hii gari ni battery dogo, 40 kWh ikiwa full inakupa kilometa 350 hivi tu.

Ni nzuri kama misele ya mjini tu ila ukisema unaenda Dar to Moro inabidi uwe na uhakika wa kuchaji kabla haujarudi.

Ila, kama haujataka EV direct kuna options mbili naweza sema zifuatilie. Hizi ni kama daraja la kufanya transition ya kutoka ICE kwenda EV:

1. PHEV - Plugin Hybrid Electric Vehicle
Hizi ni hybrid (gari za engine na battery) ila za kuchaji mfano Toyota Prius (sio zote) na Mitsubishi Outlander PHEV. Hizi unaweza tembelea hadi km 60 kwa umeme tu.

2. Nissan e-power hybrid
Nissan wana hybrid zao zinaitwa e-power hybrid, tamu sana. Ni kama EV kwasababu pamoja na kua zina engine ila engine haitembezi matairi ila inachaji battery na motor ndio inatembeza matairi kama EV.

Sorry nimejibu kwa urefu sana.
Nashukuru sana kwa ufafanuzi yakinifu kabisa huu mkuu nimekupata vema sana shukrani, nje ya mada kidogo paragraph kadhaa hapo zimenipa swali moja ambalo ni kama umeanza kulijibu kidogo japo sina hakika

Kuhusu haya magari tunayoona yameandikwa hybrid mfano vits honda fit na kadhalika ninachosikiaga tu ni kwamba yanatumia umeme na mafuta ina maana kwa hiyo segment ya umeme ni swala la kuchaji pia au hiyo ni moja kwa moja inakuja na hiyo sijui tuiite teknolojia , msaada tafadhali
 
Pamoja mkuu.

Magari ya hybrid yapo ya aina tofauti tofauti, ila naweza kukupa mchanganuo hapa kidogo ambao sio official.

1. Mild hybrid (MHEV)
Hizi zina battery na motor ndogo, ambavyo kazi yake ni ku-assist engine mfano unapanda mlima au una
Gari haliwezi kutembea kwa EV lazima engine iwe on muda wote, sema kidogo fuel inaimprove. Mfano Suzuki Swift.

2. Parallel Hybrid
Hizi engine na motor vyote vinaendesha matairi, ila motor na battery yake ni vikubwa zaidi kwahiyo mafuta vina improve zaidi na perfomance.
Mfano Hodna Fit za mwaka 2013 kurudi nyuma, IMA tenchnology.

3. Series Hybrid
Hizi mfano Nissan Note e-Power, ambavyo engine haizungushi matairi kazi yake ni kuchaji battery tu. Motor ndio inayoendesga matairi.

4. Series - Parallel Hybrid
Hizi ndio hybrid za kawaida, zinatumia engine kuendesha matairi wakati engine inachaji battery, kwahiyo kuna muda gari linaenda full EV mfano Prius.

5. Plug-in-Hybrid (PHEV)
Hizi ni kama hybrid za namba 4 ila zimeongezewa feature ya kuchaji. Unaweza kutembea hadi km 20-80 full EV mfano Mitsubishi Outlander PHEV.

Kwahiyo sio hybrid zote za kuchaji, za kuchaji ni ilo kundi la 5 tu. Hybrid nyingine zinajichaji zenyewe gari linavyotembea (law of conservation of energy, from III).
 
Nashukuru sana nimekupata
 
Back
Top Bottom