Evelyn wa chumvi...

Evelyn wa chumvi...

Maji yabaridi yalinigutua nakunirudisha katika ufahamu!.
Ndo kwanza nikazirudia fahamu zangu huku nikifumbua macho yangu kwa tabu!.

Kwa mbele ilionekana taswira ya mtu mwanaume alishikilia ndoo ndogo mikononi pake kisha nikasikia tena
"Ongeza"
Punde ikaletwa ndoo nyengine ndogo ikiwa na maji tele!.

"Waaaaa"
Nilimwagiwa maji mengine na yote yakaishia kwenye mwili wangu!.
Ndo kwanza nikatahamaki kuwa mikono yangu ilikuwa imefungwa kwa kamba ngumu iliyotokea juu,miguu yangu pia ilikuwa imefungwa kiasi cha kusikia maumivi!.

Matone ya maji yaliendelea kunidondoka toka katika mwili wangu,nguo zangu nazo zililowa chepechepe!.
Twasira ya mtu yule aliekuwa ananimwagia maji alinisogelea na kunikaribia kisha akanitazama kwa tuo Kama akinidadisi ndipo akainua mkono wake wakushoto uliokiwa umeshikilia chupa ndogo ya pombe ambayo sikuweza kuitambua jina,isipokuwa kimiminika chake kilikuwa kama maji mepesi!.
Aligida nakushusha mkono na kuendelea kunitazama.

"Yaonyesha mtu huyu si mwenyeji katika hizi kazi"
Aliongea mtu huyu huku akiwageukia watu watatu waliokuwa wamesimama nyuma yake.
Aliniacha nakwenda kujiunga na watu wale watatu kisha wakafungua mlango nakutokomea nje.

Harufu nzito zilinifikia katika pua zangu!,kwa mara ya kwanza sikuweza kugundua kuwa ilikuwa ni harufu yanini lakini kadri muda ulivyozidi kwenda niligundua ilikuwa ni harufu ya mafuta ya mashine maarufu kama oil.
Niliyazungusha macho yangu huku na huko nakuambulia kiza hafifu.. kwa pembeni Kama hatua tano hivi niliona machuma mazito ya magari yakitapakaa pasipo mpangilio!.
Upande wapili napo niliona pipa kubwa jeusi likiwa limesimamishwa,huku chini yake kukiwa na makorokoro ya chuma ambayo sikuyaelewa kazi yake..

Niligundua nilikuwa nimetekwa nakuletwa kwenye chumba hichi kikubwa kilichoonekana kama sehemu ya matengenezo ya magari (garage).
Si eve wala Anitha wote hawakuwa nami!.. kwenye chumba hichi nilijikuta peke yangu nisijue hata nilifikaje.. kumbukumbu zangu zilinijia nakukumbuka mara ya mwisho nilikuwa kwenye gari mimi,eve,anitha na yule mtu tuliemuweka nyuma ya buti.. Kisha mshindo mzito ulisikika wa gari letu kugongwa baada ya hapo sikukumbuka chochote zaidi ya kujikuta kwenye chumba hiki chenye makorokoro!.

Maswali lukuki yakaivaa akili yangu..
"Eve na anitha wako wapi..?"
"Ama walikufa kwenye ajali..?"
"Na hawa walionishika ni wakina nani..?"

Hakuna swali hata moja nililotoka na majibu yake!. Nani angenijibu katika chumba hichi kilichotulia na chenye makorokoro ya chuma kila mahali!.
Niliinua kichwa changu nakuitazama kamba ile iliyoifunga mikono yangu kwa kuikutanisha!,juu zaidi niliona dari la mabati likinizodoa kwa kutoa joto kutokana na mwanga wa jua huko nje!.

Maumivu ya kamba katika mikono na miguu yangu nayo ilizidi kunifukuta,kiu nacho kilikuwa bayana katika koo langu.
Nilizoea kulisema neno "mateso" mdomoni mwangu lakini mara hii nilikuwa nikiliishi vilivyo!,hata zile filamu za utekaji nilizoziona runingani leo hii mimi ndo nilikuwa nikiyaishi mateso hayo!.
Kuna muda nilitamani iwe ni ndoto lakini haikuwa.. hata kazi yangu ya dereva taksi niliyoiona haifai leo hii niliiona heri yenyewe kuliko Mambo haya nayopitia huku nisijue chanzo chake!.
Kutokana na maumivu nikaamua kujivuta na kusimama japo miguu na mikono iliongeza maumivu zaidi, dakika mbili tu za kusimama zilitosha nijisikie ahueni lakini katika wakati huohuo mlango ulifunguliwa nakusababisha macho yangu kulakiwa na mwanga ulioniumiza macho!..

Nilianza kuona vivuli vyao vikiwa tayari vimenifikia,Kisha taswira za watu zikajengeka mbele yangu na hatimae watu wale niliwaona vilivyo.
Mara hii hawakuwa wanne tena bali aliongezeka mmoja ambae alikuwa ni yule mzungu mwenye pua ndefu!.
Walinisogelea nakunizunguka huku yule mzungu akiwa mbele yangu akiniangalia pasipo kusema chochote isipokuwa aliendelea kuvuta sigara yake kubwa huku akinitazama!.

Alinisogelea zaidi kisha akanipulizia moshi wake wa sigara ulionifanya nikohoe.. aliniendelea kunitazama huku akinizunguka,punde akamshika begani yule mtu wa awali aliekuwa akinimwagia maji!.
Sikujua haraka ishara ile ilikuwa na maana gani lakini punde hiyohiyo mtu Yule alinisogelea mbele yangu nakuanza kukita ngumi zake kwenye tumbo langu!.

Ngumi yake ya kwanza ilitua upande wakulia wa tumbo langu, yapili nayo haikuchelewa ikatua katikati ya tumbo langu huku ngumi yake yatatu ikitua upande wakushoto wa tumbo langu!.. ngumi zake zilinipepesua nakufanya nigugumie kwa maumivu huku nikitoe ukelele!.
Alitulia nakulirudia zoezi lake kwa mara nyengine!,mapigo yake kadhaa katika mwili wangu yaliirudisha miguu yangu nakupiga magoti huku maumivi nayo yakinikabili vilivyo!.

Nilitulia kwa sekunde kadhaa kisha sauti ya mtu yule ikakita katika maskio yangu!.
"Usiposema fedha zetu zipo wapi yatakuja mafuriko ya ngumi zaidi!"

Akili yangu ndo kwanza ilikumbwa na taharuki kutokana na taarifa hiyo niliyoisikia!.. nilijiuliza "fedha zipi mimi Jonas kileo nimezichukua??"
Nikiwa katika tafakuri hiyo ghafla nilipokea pigo la teke lililokita katika kifua changu nakufanya nirudi nyuma huku nikizuiwa na kamba za mikononi!..
Nikiwa katika maumivu bado ndipo nikahisi mtu mwengine nyuma yangu akininyanyua nakuniweka sawa tayari kwa mtu yule mbele yangu aendelee kutoa mapigo!.
Hakuchelewa,ngumi zake tena ziliulaki mwili wangu kwa fujo huku zikiwa hazichagui mahala pakutua!..
Mfululiza wa mapigo yake uliendelea mpaka nilipomsikia mzungu Yule akisema

"Tosha"

Alitulia mtu yule kwa kutii amri,hata aliekuwa nyuma yangu nae akaniachia nikitapatapa kwa maumivu ya kipigo!. Nikiwa bado natapatapa mzungu na sigara yake alinisogelea na kwazarau akanipulizia moshi wake mfululizo!.

"Sina pesa zenu na wala sijui chochote kuhusu fedha hizo!"
Nilijibu kwa uchungu huku nikimuangalia mzungu yule kwa tabu!

Alicheka kidogo na kunitazama kwa dharau kisha akaongea kwa kubahatisha maneno!.
"Wapi mke zako..?"

Nilijua swali aliwaulizia eve na anitha lakini sikujua aliniuniliza kwasababu gani!,kwani alifahamu fika kuwa sikujua walikuwa wapi!.

"Sifahamu" nilijibu huku nikikohoa na kuhema kidogo!
Kwa mara nyengine mzungu yule akanipulizia moshi wake huku akicheka kwa kebehi na kunyanyuka akirudi nyuma kwenda mbali nami!.
Kikohozi kidogo kikanitoka tena kutokana na moshi ule ulionivagaa kwa pupa!.

"Hufahamu walipo..? Usiposema fedha zetu ziko wapi utaenda kuzungumza nao kwa mwili wa roho!"
Aliendelea mzungu yule huku maneno yake yakinijaza taharuki!.

Nilimtizama kwa umakini sura yake ilionyesha dhamira ya kile alichokisema!
Simanzi ikanijaa huku tafakuri zikinitawala juu ya eve na anitha ambao wakati huu hawakuwa karibu nami,nikagutuliwa tena kwa konde la shavu huku nikipewa maneno ya vitisho na mtu yule mtesaji..
Punde waliondoka nakufunga mlango.

******

THE BITE

Harakati nje ya jengo hili ziliendelea huku kila mmoja akionekana kuwa na shauku kwa kile ambacho muda mfupi kingetokea,suti zilizonyooshwa ipasavyo ziliisitiri miili ya watu hawa mashuhuri huku wengine wakijazwa na vitambi vyastarehe!.
Vinywaji mezani vilisheheni na kila alikamatilia kile kilichomfaa,mziki nao haukukosa uliendelea kutumbuiza huku kukiwa na wadada walioumbika vilivyo wakinengua kufuata mapigo ya mziki ule.

Mambo yote haya yalifanyika katika uwanja wa nje wa jengo hili lililopakana na majengo mengine machache yaliyokuwa pembezoni!.

Walionekana pale huku mshehereshaji wa sherehe akishika kipaza sauti nakuanza kutangaza watu wajiandae kwaaji ya kumpokea mkurugenzi wa kampuni hii ya THE BITE.
Kampuni hii ilijihusisha nakutengeneza vitafunwa mbalimbali vya mkate lakini leo hii walikusanyika hapa ili kuzindua kitu chengine ambacho kingeleta tija na kuongeza wigo wa kampuni kibiashara.. hawakutaka tena kujihusisha pekee na vitafunwa bali pia wigo wao mara hii ulijipanua katika vinywaji!.
Hawakuishia hapo katika tafrija hii walidhamiria pia kulibadirisha jina la kampuni ambapo mara hii wangejiita IDOLA COMPANY.

Makofi na vifijo vilishamiri pale mkurugenzi wa kampuni hii aliposogea katika viwanja hivi huku akiwa amevalia suti nyeusi na moka zilizomkaa kisawasawa.. umri wake ulikuwa katikati akiwa kama akielekea katika uzee na kuanza kuuvua ujana,ndevu zake kidevuni alizichonga vyema huku akiliachia tabasam la mafanikio alipokuwa akisalimiana na wageni waalikwa kabla ya kuendea kiti chake alichoandaliwa kama mkurugenzi wa kampuni hii.

Aliketi kisha mshehereshaji akaendelea na ratiba nyengine kama zilivyopangwa.

Jengo hili lilielekeana na moja kati ya jengo la ghorofa tatu ambalo lilikuwa bado katika ujenzi,majengo haya mawili yalitenganishwa na barabara ya rami iliyokuwa ikikatisha.. na humu ndimo alikuwepo mgeni mwengine ambae yeye hakupenda kwenda kujionyesha ktk tafrija hii!..
Kwa hadubini yake aliweza kuchungulia nakufatila matukio yote yaliyoendelea kwenye tafrija hii..
Alipomuona mzee huyu akiwasili katika viwanja hivi alijikuta akilitaja jina lake

"Godwin masimba!"

Aliendelea kutazama kwa hadubini yake huku akiwa kama akisubiri kitu.

"Bila kupoteza muda ningependa tumkaribishe mkurugenzi wetu ili aseme machache kisha akatuzindulie kampuni yetu,mheshimiwa Godwin karibu"
Maneno hayo yalisemwa na mshehereshaji huku akiwa mwenye bashasha. Punde tu aliposema maneno hayo makofi yalipigwa kwa wingi yakimkaribisha Godwin.

Kwa tabasam la tashtiti Godwin aliikaribia steji nakushika kipaza sauti,kabla ya kusema chochote aliirekebisha sauti yake Kisha akaanza kuushukuru umma ule wa watu uliojitokeza katika tafrija ile!..

"Sema baba sema baba!" Ilisikika sauti moja ikimhamasisha godwin aseme yale ambayo walitaka kuyasikia. Vicheko hafifu viliwatoka watu nae Mr Godwin aliendelea.

Ulikuwa ni wakati kama huu ambao mtu huyu aliusubiria,mgeni huyu aliejialika pasipo kualikwa aliiweka hadubini yake pembeni na kisha kuchukua bunduki kubwa ya kudungua iliyokuwa pembeni yake!.
Akiwa amelala chini katika floor hii ya tatu ya jengo hili,mtu huyu alilitupa jicho lake mpaka katika lenzi ya bunduki hii.. kitu chakwanza kukiona ilikuwa ni jina la THE BITE ambalo liliandikwa mbele ya jengo hili kulipofanyika tafrija!.

Taratibu aliihamisha uelekeo wa bunduki yake mpaka alipolifikia steji nakumuona yule aliemuhitaji..
Bwana Godwin bado aliendelea kutamba katika steji hii huku akionekana kuwa mtulivu na mwenye bashasha zaidi.

Kipimo cha lenzi kiliwekwa vyema Kisha mdunguaji huyu aliivuta pumzi ndefu nakuitoa huku bado akiendelea kumuangalia bwana huyu akinena katika steji hii,makofi machache yalipigwa Kisha Godwin akaendelea tena..

"Hivyo kamati ya kurugenzi yetu ikaamua itafute jina jipya na hata kuongeza wigo wa biashara yetu" alitulia nakuvuta pumzi kidogo..

Mtu huyu aliendelea kumtizama Mr Godwin kupitia lenzi ya bunduki yake,huku midomo yake ikichezacheza kwa kutafuna jojo!.

Alilala pale huku umakini wake wote akiuhamishia alipo mtu aliemwekea tageti,kwa Mara ya pili tena alizivuta pumzi zake na kutulia pasipo kuzishusha ndio hapohapo kidole chake kilichokuwa kimeshikilia tufe la bunduki hii kiliibonyeza pasipo kusita!.

Ulitokea mwanga hafifu kama cheche ndipo punde hiyohiyo bwana Godwin alijikuta akisukumwa nakitu asichokijua kilitokea wapi!.. Kama furushi la mzigo alitupwa nyuma ya steji huku damu chache zikipaa nakutua chini,mike ilitupwa kwele hata spika nazo zikakita kwa mike ile kudondoka..
Kelele zilisikika huku watu wakitawanyika wasijue chakufanya! Vitu vyote vilivyokuwa vimewekwa kwa mpangilio vilitupwa hovyo.

Aliendelea kutazama lenzi yake nakuona kile kilichojili eneo lile!,mwili wa Godwin ulikuwa chini huku ukiwa bado umevalia nadhifu lakini katika sekunde hizi chache damu ilikuwa ikimtiririka na kutapakaa hata katika steji.

Kwa haraka mtu huyu baada yakuona kazi yake ilikwenda sawia alishuka katika jengo hili nakutokomea pasipo julikana!.

******

Maumivu ya kipigo yaliendelea kuukumbatia mwili wangu!.. njaa na kiu navyo vilikuwa mlangoni kwangu vikiniadhibu!.
Mikono yangu ilichoka kifungo hichi kisichokuwa na majibu ya ukomo wake,miguu yangu nayo iliendelea kuuma huku ikikosa ganzi!.

Mlango ulifunguliwa ndipo nilipogundua giza lilikuwa limeshatawala!,tochi yenye mwanga mkali ilitua usoni kwangu nakusababisha macho yangu kuugulia maumivu.
Nilisikia hatua zikinisogelea huku bado mwanga wa tochi ukiendelea kunimulika!..
Kwa tabu niliyafumbua macho yangu nakukutanisha sura yangu na Yule mtesaji aliekuwa akinirushia ngumi mchana!..
Akiniangalia huku akicheka pasipo kutoa sauti kisha..

"Bado hujui fedha zetu zilipo..?" Aliniuliza kwa dharau kisha akatulia kwa sekunde chache nakuendelea
"Si useme tu tukuachie ukaendelee na maisha yako kuliko kupitia haya mateso!"
Niliinua kichwa changu nakumuangalia tena usoni pake!,nilipokelewa na macho yake makundu ambayo hayakuonekana kuwa na huruma!.
Alinyanyuka nakumulika pande nyengine mwa chumba hiki!.

"Nafikiri mimi sio mtu sahihi!,Sina fedha zenu na wala sijui mnachokizungumza" nilisema kwa tabu.

Kicheko kikubwa kikamtoka huku akiurudisha mwanga wa tochi yake kunimulika!.. baada ya kicheko chake hakuzungumza kitu bali tochi niliiona ikianguka chini na hapohapo alinivagaa nakuanza kunitia ngumi mfululizo!.
Yale maumivu yaliyoanza kutulia yaliamshwa tena!
Kipigo cha mara hii kilichanganywa mateke na ngumi pasipo kutulia huku nikitweta kwa maumivu!.
Hakika cha mtema kuni nilikiona hata damu nayo ikaanza kunibubujika mdomoni!.

Alitulia nakuniangalia nilivyozamia katika lindi la maumivu huku nikipiga kelele ambazo hazikuwa na msaada!.
Punde akaingia mtu mwengine nakumpa taarifa mtesaji wangu!.

"Gari tayari" alisema mtu yule huku akiondoka!
"Okay nakuja" alijibu mtesaji wangu huku akitoa shingo yake kwa mgeni Yule nakunigeuzia mimi!.

Coming back...

We are waiting
 
Mkuu toka jana nachungulia tu ngoma bado [emoji23]
 
We kenzy hebu lete mzigo ngosha acha tabia ya kishoiya, ukitaka kujua maana ya kishoiya ni nini muulize miss chaga atakupa maana ya kishoiya.
 
Natamani kumtukana ili achangamke, ila kwa kuwa leo ni Sabato ngoja nimuache kwanza ila Sabato ikipita matukano yatamhusu huyu kishoiya [emoji1][emoji1]
Anapandisha ghadhabu sana
FB_IMG_16363797939350890.jpg
 
Back
Top Bottom