Kiza hafifu kilianza kutawala huku kukiwa na kibaridi chepesi, niliendelea kukanyaga moto nakutupia macho yangu kwa chati nikimtazama binti yule alieweweseka kufuata mitetemeko ya gari akiwa bado kapoteza fahamu!. Tulikatiza katika njia ya vumbi huku pembezoni kukiwa na miti mingi, niliendelea kuambaambaa kwenye msitu nikiwa sijui uelekeo wowote zaidi ya kufuata njia nazo sikufahamu ziliekea wapi!.
Njaa,uchovu na kiu viliendelea kunitafuna kila punde,maumivu nayo hayakuwa mbali bado yalinizodoa kama jinamizi!. Hata nilipojitazama katika vioo vya gari sura yangu ilionekana kutapakaa vumbi na alama ndogo ya kuumia kwenye paji la uso iliyovilia damu!,mikono iliyotapakaa vumbi na michubuko iliendelea kuukamatilia usukani vilivyo huku miguu yangu pia ikikanyaga breki na moto kwa kupokezana kufuatisha barabara hili la lafu lilivyo. Baada ya mwendo wa Kama dakika tano kwa mbele niliweza kuiona barabara ya rami,hili lilikuwa Kama tumaini jipya kwangu nakuona angalau nilipata pa kuanzia japo bado sikufahamu ni uelekeo upi wa kwenda!. Nilikoleza moto wa gari mpaka kuifikia rami bila hata kuwaza zaidi nikaamua nichukue uelekeo wa kulia,Mara hii baada ya kuishika rami ndipo nikakumbuka hata kuutazama mshale wa mafuta!,bahati ilikuwa kwetu mafuta yalionyesha kuwepo yakutosha.
Baada ya kulitambua hilo nikakoleza moto zaidi katika kuicharaza rami nayo gari hii aina ya Ford iliitika wito nakuanza kuyatandaza matairi yake kwa spidi iliyotukuka. Kwa mwendo wa dakika kumi sikuweza kupishana na gari la aina yoyote ile mpaka sasa!,giza nalo likazidi kuiva nikayatupia macho yangu kwenye saa ya gari ambayo ilisoma mida ya saa moja na dakika hamsini na kenda.. macho Tena nikayahamishia siti za nyuma nilipomuweka abiria huyu aliegoma kuamka ambae sikumfahamu hata jina isipokuwa tu Sweta lake lililoandikwa "Sweetie" nilipoyarudisha macho mbele ya gari kwa mbali nikaona mwanga wa gari jengine likija kwa spidi lakini hata kabla ya kupishana nalo lilionyesha indiketa ya kukata kona ktk moja ya barabara ndogo iliyochepuka kwa pembeni!. Mawazo yakanirejesha kwa binti huyu aliepoteza fahamu nikamchungulia tena kwenye kioo chagari kilichoonyesha kwanyuma,nami nikapata tena wasaa wa kuiona sura yangu ambayo aidha ingekutisha Kama sio kukuchekesha!. Nikayarudisha macho yangu mbele huku kinywa changu kikijikuta kikitamka neno "Shetani!".
Hakuna mwengine nilieweza kumuita hivyo zaidi ya yule binti mwenye uzuri wake,binti alieuteka moyo wangu kwa muda mchache nakujikuta nikitopea kwenye mtanange wa nipe nikupe!.
Mtanange uliofanya nipumbazike nakujikuta kwenye dhahama ambayo sikufikiri hapo kabla kama ningeweza kuwa mimi leo hii wa kushika bunduki na kutumbukiza risasi kwenye mwili wa mtu!. Binadamu wawili nisiowafahamu hata majina yao tayari niliwapoka uhai wao!. Tusi zito lilinitoka nilipojiona kuwa nimeshakuwa muuwaji!,hapohapo nikayakumbuka na yale mateso niliyopitia ambayo sikujua sababu yake zaidi ya kulazimishwa nitoe taarifa za eve ambae nilijisingizia ni mchumba wangu baada ya kuminywa korodani,mtu ambae nilimjua kwa punje tu leo hii ameniingiza kwenye shimo la mabalaa yasiyoeleweka.. nilijiuliza "Nitamuitaje tena jina lake lile zuri..?" Jibu lililotoka ni shetani tu ndo jina ambalo lingemfaa na kumpendeza. Japo niliyalaumu matokeo haya lakini bado moyo wangu ulitaka kumjua zaidi Evelyn!, Lilinijia swali "huyu ni Nani..?" Nikajijubu tena "shetani!" Anafanya nini..? Hapo hata sikuwa na jibu zaidi ya kumpachika sifa nyengine niliyomuona nayo "Nunda mla watu!".
Mawazo haya yakipuuzi yaliendelea kuzunguka kichwani yakishahabiana na njaa huku kiu nacho kikilikorofisha koo langu!.
Mara hii nilitokea sana kumchukia eve licha ya uzuri wake wenye kugalagaza mamia ya marijali!. Hamu na shauku ya kutaka kumjua zaidi ilinitapakaa akilini huku nikiukumbuka ule umaridadi wake wa kimapigano na haya yote sikuweza kuyajua hapo kabla mpaka pale nilipomshuhudia akiyafanya!.
Nikiwa nimetopea ktk lindi la mawazo ghafla nikashitushwa na sauti ya kikohozi kutokea nyuma yangu!,niliyatumbua macho yangu kama fundi saa Kisha nikaangalia kioo kile kilichoonyesha siti za nyuma!.
Macho yangu yakakutana na binti yule nae akitizama katika kioo kile huku akiendelea kukohoa!,aliyatumbua macho yake Kama mjusi aliebanwa kwenye mlango! Nafikiri hakutegemea kukutana na sura ya mpauko namna hii. Labda alihisi mimi ni jini!!
Akiwa bado ametandwa na hofu huku akiwa haelewi kile alichokiona alionekana Kama mtu alietaka kuuliza kitu lakini alisita!. Nikaamua kuvunja ukimya "pole" kabla ya kujibu aliendelea kukohoa huku akiambaa macho yake ktk gari lile!. Hakujibu chochote zaidi ya kuyatumbua macho yake zaidi! Kilipita kimya kifupi akauliza maswali lukuki "wewe ni nani..?,unanipeleka wapi..? Na lameki yupo wapi..?"
Sikujua hata nianze nalipi ila nilichoona ni Kama aliniongezea mzigo wa maswali ambao nami sikuwa na majibu yake!.
Nilitulia Kisha nikachagua swali moja la kumjibu ili kumtoa wasiwasi! "Mimi ni raia mwema!" Nilimjibu huku nikimtazama kupitia kioo. Nae akanitazama lakini kwa muonekano ule nilijua alikosa imani na jibu langu!.
Tulitulia tena kwa muda akanitupia swali jengine nililoliacha kumjibu "Lameki yuko wapi..?"
Sikujua hata nianzie wapi ila nilichofahamu kuwa alimzungumzia yule mwanaume aliekuwanae ktk chumba kile kidogo!. Nilijiuliza nimwambie ukweli..?
Hilo wazo nikalitupilia mbali ndipo nikamjibu "utafahamu tukifika!" Hapohapo akanitunuku swali jengine tena nililoliacha pia! "Tukifika wapi..?"
Swali hili lilikuwa ndo kwanza likiugutua ubongo wangu!
Sikujua kamili wapi hasa ningeelekea baada ya kuipata ramani,punde nikajikuta nawaza "nielekee nyumbani kwangu...?" Wazo hilo nikalipinga kutokana na maadui hawa nisiowafahamu,bado nilihofu kuhusu usalama wangu haswa nilipomfikiria eve!.
Bado sikufahamu vyema kama alikuwa mtu mwema kwangu isitoshe hao wanaomtafuta waliweza kuutishia uhai wangu japo nimeweza kutoka kwenye shimo la mamba!.
Nikamtazama tena kupitia kioo alibaki kunikodolea macho yake akisubiri jibu toka kwangu.
Nilitulia Kisha nikamjibu "tunaelekea sehemu salama!"
Aliguna "mh!" Kisha akauliza "sehemu gani hiyo salama isiyo na jina..?" Nikajisaula Kisha nikaendelea "binti usihofu nimekutoa mikononi mwa watu wabaya,kuwa mtulivu utaelewa kila kitu!"
Jibu hilo walau lilianza kuvuna uaminifu japo haikumpa moja kwa moja uhakika wenye ithibati. Kilipita kimya kifupi akauliza tena "waitwa nani..?" Nikamjibu kwa ufupi "jonas".
Baada ya hapo alitulia tuli mara hii akaamua awe mtalii tu wakuangalia namna tulivyoiacha miti na mito kadhaa.
Nikaamua nami niuvunje ukimya nikamtupia swali "unaitwa nani..?"
"Anitha" akajibu. Kwa mara nyengine tena nikampa pole ambayo hii haikupita patupu aliijibu Kama mtu tuliezoeana nae miaka kenda.
Ilinipa tabu kuanza kufikiri kuwa binti mdogo Kama yeye Tayari alianza kupata mabalaa kama haya,maswali mengi yasiyo majibu yaligonga kichwani pangu huku nikipata hamasa ya kutaka kuijua historia yake iliyofanya mpaka yeye akatumbukia kwenye lile pagala bovu!.
Tulipita mito na vijito ndipo kwambali tukaanza kuona mataa ya jiji yakimetameta na kutupokea kwa shangwe japo kwetu sisi wageni hawa wawili tulijawa na huzuni!. Tulianza kupishana na magari kadhaa hata ramani ya barabara nizitambuazo zikaanza kujichora katika kichwa changu.
Nilimtupia jicho anitha,alionekana aleichoka na mwenye huzuni huku akiwa ameegamia kioo akiwa ametumbukia katika lindi la mawazo!. Sikupenda kumuona katika hali hii lakini sikuwa na namna,nilipoyarudisha macho yangu mbele masikio yangu yakanasa sauti yake
"Nina kiu!"
Laiti angelifahamu nami pia nilikuwa vivyohivyo hata asingelinena maana aliliamsha tena koo langu lianze kuukumbuka ule mziki wa kiu!.
"Subiri tufike hapo mbele huenda tukapata huduma ya maji" nilimjibu.
Punde hii likanijia tena lile wazo la wapi nakwenda!,nilimuahidi anitha sehemu salama lakini hata kwangu hivi Sasa hapakuwa salama tena! Katika kuchekecha akili nikamkumba rafiki yangu Jeff!.
Jeff alikuwa rafiki yangu toka kitambo tuliefahamiana huko kwenye machimbo ya madini,ambako nako kwa miaka miwili tuliambulia fedha ya kula tu na milungula kadhaa ya kutanua siku mbili tatu!. Baadae tukapotezana kila mmoja akatafuta njia yake mpaka baada ya miaka kadhaa tena tukakutana ndani ya jiji,yeye akiwa daktari nami nikiwa Kama dreva taksi.
Mara hii ya pili nilipokutana nae nilidhani huenda akawa amebadilika lakini Jeff niliemjua alikuwa ni yuleyule aliependa wanawake na muziki!. Alikuwa mtu wa kuponda raha asietaka kujichosha. Karia yake yasasa ya udaktari ndio angalau kidogo ilimbadilisha nakuwa Kama mtu alietulia japo ule utundu wake hakuuacha ndipo hapo ule usemi wa "jasili haachi asili" kwa Jeff bado ulishika hatamu.
Nilikumbuka moja ya tukio lake la kufumwa na mke wa mtu ambapo aliponea chupuchupu kwa kupitia dirishani huku akiwa uchi wa mnyama!.
Japo alikuwa mwingi wa matukio lakini kwangu ndie alikuwa mtu Bora na nilieweza kumuamini zaidi. Niliwaza breki zangu zitatua kwenye kiota chake ambacho kilikuwa nje kidogo ya mji.
Mji ulitupokea kwa mng'ao wa mataa na kelele za magari,watu walionekana wenye pilikapilika za huku na kule,nilipunguza spidi ya gari huku nikiisoma ramani vizuri ili nianzishe safari kukifikia kiota cha jeff. Niliunyonga usukani kufuata kona kadhaa za round about Kisha nikashika njia iliyoelekea kule nilipohitaji.
Ilikuwa ni safari iliyotuchukua nusu saa tu nasasa tulikuwa mbele ya nyumba ya Jeff iliyozungushiwa ukuta Kama fensi huku ikipendezeshwa na geti kubwa jeusi,gari ilibidi tulipaki kwa kuliacha mbali kidogo kwani tulihofu wahalifu wetu wangeendelea kutusakama,Kama wangekuwa wameweka teknolojia ya GPS .
Moja kwa moja nililisogelea geti lile kubwa jeusi nakubonyeza kitufe cha kengele kilichokuwepo pembezoni mwa ukuta. Baada ya dakika nzima kukata tukasikia geti likifunguliwa tahamaki alikuwa ni rafiki yangu Jeff akitushangaa wageni ambao tulikuja bila taarifa.
Alituangalia juu mpaka chini Kisha akaita "Jonas" nami nikaitika "naam"
Kimekupata nini..? Aliuliza Jeff
"Ni stori ndefu kaka!" Nilimjibu huku nikivua kiatu changu kile kimoja! Alibaki akitushangaa kwa sekunde Kisha akatukaribisha mpaka ndani.
Sikuwa Mimi Wala anitha hatukuweza kujivunga kwa haraka tukaifikia fridge nakuanza kudigida maji Kama wenda wazimu.. Jeff alibaki akituangalia asijue nini kimejili Kisha akatoweka katika korido za nyumba yake.. baada ya kuduguda maji kwa pupa tulitulia nakuanza kushusha pumzi kama watu tuliotoka kwenye vilele vya mlima Kilimanjaro!. Punde alirudi Jeff akiwa na hotpot kubwa,ni Kama alijua tulikuwa na njaa isiyopimika.. aliweka mezani kisha akatukaribisha wageni wake.
Tulijipatia ndizi roast zikichanganywa na nyama huku juisi ya embe ikitusindikiza taratibu.. Jeff hakutaka hata kutusemesha kujua kilichotupata kwani alijua hakuna hadithi ingesimulika hapo.. aliingia zake chumbani akatoka na box lake la huduma ya kwanza akitutaka tukimaliza kula tukaoge kisha ajaribu kutuziba viraka kadhaa katika miili yetu!.. alianza anitha kwenda kukoga Kisha nikafuata mimi..............