Ewe CEO wa kampuni hakikisha unafanya haya kabla ya tarehe 30/6/2025 kuepuka faini ya TZS 300,000

Ewe CEO wa kampuni hakikisha unafanya haya kabla ya tarehe 30/6/2025 kuepuka faini ya TZS 300,000

akwilau

Member
Joined
Jun 18, 2020
Posts
70
Reaction score
56
• Kulingana na Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, pamoja na kifungu cha 39 na 48 ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015, kila kampuni iliyosajiliwa, biashara ya ubia, na biashara binafsi yenye mauzo ya kuanzia TZS milioni 100 kwa mwaka, inatakiwa kuandaa na kuwasilisha ritani ya kodi ya mapato kwa mwaka 2024 kwa Kamishna Mkuu ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita baada ya mwisho wa mwaka wa fedha.

• Kwa muktadha huo wa hitaji hili la kisheria, ikiwa mwaka wa fedha wa biashara yako unaanza Januari hadi Desemba, unatakiwa kuwasilisha ritani ya kodi ya mapato kabla au kufikia tarehe 30 Juni 2025.

• Hata kama kampuni yako haikufanya shughuli yoyote ya kibiashara katika mwaka 2024, bado unatakiwa kuwasilisha ritani ya "kutokuwa na mapato" (nil return) kufikia tarehe 30 Juni 2025.

• Hata hivyo, chini ya Kifungu cha 78(1) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015, ikiwa utawasilisha ritani ya kodi ya mapato baada ya tarehe 30 Juni 2025, utawajibika kulipa faini ya TZS 300,000 kwa kila mwezi ambao hukuweza kuwasirisha ritani husika.

• Epuka kulipa faini zisizo za lazima kwa kuwasilisha ritani yako ya kodi ya mapato kabla ya tarehe 30/6/2025.

HALA Consultants,
Certified Public Accountants
NSSF Hifadhi House, 9th Floor,
Azikiwe Street/Samora Avenue.
Dar es Salaam, Tanzania.

Contacts:
[email protected]
0752 187 434
 
Back
Top Bottom