Ewe Jobless usiwahi haribu au katisha maisha yako kisa changamoto yoyote

Ewe Jobless usiwahi haribu au katisha maisha yako kisa changamoto yoyote

Pia tutumie wasaa huu kuwakumbusha jobless kuwa tunapojitolea kuwapa nafasi za kazi hata kama mshahara mdogo wajitahidi sana kuheshimu nafasi walizopewa sababu hata sisi tunapambana sana kuwatafutia hizi nafasi ndogo za ajira.

Unakuta mtu anakudharau sababu wewe mtanzania mwenzake unamlipa 100K,200K au 300K kama mshahara bila makato. Ila anadharau hiyo nafasi na kuanza kukufanyia vituko siku chache baada ya kumpa nafasi ya kazi anaharibu kazi makusudi, naleta ajizi,mara uzembe,uvivu,viburi,ujuaji ,udokozi, matokeo anaharibu mahusiano yenu na kukurudisha nyuma plus majuto.

Hii kitu inatufanya kukosa moyo wa kujitolea hata unapowaona wanateseka mtaani maana unajua unakaribisha matatizo kwenye shughuli zako. Unaamua yale majukumu kufanya mwenyewe hata kama yanakuelemea.

Vijana mnapopewa nafasi ya kazi hata kama mshahara haukidhi matarajio yako haimaanishi sasa uanze kuwa mkorofi. Its better kuiambia akili yako nje ya hii kazi una maisha gani,why ndani ya muda mfupi umeshakata tamaa na hata haujaonyesha uwezo wako na mchango wako wa kutosha kwa mtu aliyekupa nafasi?

Mbona bila hiyo ajira unazurura tu mtaani na kuishia kuomba omba tu au kupiga dili ambazo hazina uhakika wa kuwapo kila siku. Why mnafosi kutoboa kwa nguvu namna hiyo. Kijana mdogo wa miaka 18 hadi 30 unakimbilia wapi?

Unatazama sana maisha ya mtandaoni ndio maana unahisi unachelewa sehemu si ndio?🤔

MUNGU awapambanie sana majobless mjitambue pale ambapo watu wanawashika mkono.
Kijana wa miaka 30 ni Kijana mdogo Nimelia sana🥶🤣assume una kijana wa kuzaa wa umri huo Anakuomba hela kununua hela boksa utajisikiaje
 
Back
Top Bottom