Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Hili ni angalizo ambalo nalipeleka moja kwa moja kwa vijana wachache ambao bado ni wanaCCM, maana vijana wengi wameachana na hicho chama, vijana wa CCM wa hapa JF na kwingineko nawaomba sana mtambue kwamba CCM haina nia wala uwezo wa kuwasaidia mnapopata matatizo , tena matatizo yenyewe ni yale yanayosababishwa na siasa hizo hizo mnazokesha kuzifanya hadharani na mitandaoni.
Ukipata tatizo na hata kama ulipata tatizo baada ya kutumwa na chama chako utatelekezwa , naandika haya baada ya ID nyingi mpya za wafia chama kumwagwa humu JF utadhani nzige wa Kenya, bahati mbaya ni kwamba waliomwagwa wana uwezo mdogo mno wa kujenga hoja hivyo hawasumbui chochote, tambueni kwamba kazi mnayoifanya ya kutetea CCM humu ni sawa na kazi ya bure.
Jiulize kati ya wewe kapuku na Nape, January, Lugola, Manji, MO, Kinana, Makamba, Kikwete nani ni zaidi? ukishapata majibu endelea kutoa povu humu na kwingineko ukidhani ccm itakusaidia .