Kama umekuwa ukivutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) sababu ya kodi inayotokana na uandaaji wa hesabu za shule au chuo chako…Basi soma mpaka mwisho…
UKWELI USIOPINGIKA…Zipo shule pamoja na vyuo mbalimbali hadi leo hii wamelemewa na madeni makubwa yatokanayo na kodi kutoka TRA. Hili siyo kosa la TRA bali tatizo linaanzia kwa shule/vyuo husika kutokana na aina ya uandaaji wa hesabu zao.
Ukumbukwe kuwa biashara ya kuendesha shule/chuo zilizo nyingi zinaendeshwa kwa mikopo kutoka kwenye taasisi mbalimbali za kifedha. Hivyo basi kutozingatia sheria za kodi utakuwa unaiweka biashara yako ktk hali ya hatari.
Kwa mujibu wa kifungu namba 91 (1) sheria ya kodi ya mapato, 2004 ikisomwa sambamba na kifungu namba 39 na 48 sheria ya usimamizi wa kodi, 2015 kila kampuni, biashara ya ubia na biashara binafsi yenye mauzo kuanzia TZS 100M wanawajibika kuandaa hesabu zilizo kaguliwa na mkaguzi aliyesajiliwa na Bodi ya Wahasibu Tanzania (NBAA).
Hivyo acha kuweka mikopo ya biashara yako hatarini kufirisiwa na mabenki kwa kuandaa hesabu hatarishi kwa biashara yako.
kupitia Makala hii wewe kama mmiliki wa shule/chuo utapata faida hizi;
(a) Makala hii inakupa mwongozo wa kuandaa hesabu zako kwa ufasaha, kwahiyo utaweza kuepuka riba na faini ambazo ungelipa TRA, inamaana hela ambayo ingelipa kama faini utaitumia kuwekeza kwenye miundo mbinu ya shule/chuo.
(b) Itakusaidia kufahamu wapi kuna viashiria vya hatari kwenye biashara yako, kwahiyo itakuwa rahisi kufahamu wapi pa kuboresha, inamaana ufanisi wa biashara utaongezeka dhidi ya washindani wako sokoni.
(c) Itakupunguzia mgogoro na TRA, kwahiyo utatumia muda wako kujikita ktk kusimamia biashara zako, inamaana mapato ya biashara yataongezeka maradufu.
(d) Itasaidia kuwajengea uwezo wafanyakazi wako wa uhasibu, kwahiyo utendaji wa usimamizi wa fedha utaongezeka, inamaana itakupunguzia kulipa riba na faini zisizo za lazima kwenda TRA.
NI KAMA BAHATI KWAKO…Hizi ndo njia salama zitakazokusaidia kuandaa hesabu zako ambazo zitaiweka biashara yako salama na katika mazingira rafiki ya kiushindani sokoni dhidi ya washindani wako…Soma makala hii MPAKA MWISHO
1. Mauzo kwenye EFD mashine dhidi ya jumla ya ada,usafiri, mauzo ya uniform na bidhaa nyingine zinauzwa hapo shuleni/chuoni.
Hakikisha unapoandaa hesabu zako, mauzo ya kwenye mashine ya EFD yawe sawia na jumla ya mapato yatokanayo na ada, usafiri na mauzo ya uniform ambayo yataonekana kwenye hesabu zako. Kwa mjibu wa kifungu namba 86 (1) sheria ya usimamizi wa kodi, 2015 (Finance Bill 2024), endapo kutaonekana kuna tofauti utatozwa riba ya 20% ya thamani ya huduma uliyotoa au Tshs 2,000,000 lakini isiyo zidi 20,000,000 na itachukuliwa ambayo ni kubwa kwa kosa la kutotumia EFD machine inavyotakiwa.
2. Nyaraka zitokanazo na manunuzi ya mali kwa mahitaji ya shule/chuo
Kifungu namba 11 (2) sheria ya kodi ya mapato, 2004 inamtaka mfanya biashara kudai na kutoa risiti ya manunuzi au mauzo atakayo fanya. Sambamba na mabadiriko ya kodi ya 2024 ya kifungu husika, inasisitiza kuwa ili manunuzi (gharama) zako zikubaliwe kupunguzwa kwenye mapato ya biashara yako lazima yaambatanishwe na risiti za EFD tofauti na hapo manunuzi yatakataliwa na kutozwa kodi 30% (corporate tax). Kuna yale manunuzi yanayopatikana kwa wauzaji wasiotumia mashine za kielektroniki kama nyanya, vitunguu, mchicha na mengineyo hakikisha unaifadhi taarifa za manunuzi yake kwa usahihi ili wakati wa ukaguzi wa TRA iwe rahisi kutambulika.
3. Taarifa za mikopo kutoka taasisi za kifedha.
Wakati wa kuandaa hesabu za shule/chuo hakikisha unaweka bayana taarifa za mikopo, kitakachoonekana kwenye hesabu zako ni lile deni la mkopo lililosalia pamoja na riba yake, hii ni kwa mjibu wa kifungu namba 12 (1) (a) sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004. Endapo hutaanisha mikopo yako kwenye hesabu, na TRA wakafanya uchambuzi wa kifedha (cash analysis) itaonesha kuna pesa imeingiza kwenye mzunguko wa biashara yako lkn haijulikani imetoka wapi. Mwisho TRA wataitafiri hiyo pesa kama ni ada ambayo hukuitolea risti za kielektroniki na itapigwa kodi 30% na kupigwa faini sambamba na kutozwa riba.
4. Kodi itokanayo na ajira (Employment tax)
Mishahara inayolipwa kwa walimu na wasaidizi wa kazi hakikisha kiasi husika kimelipiwa PAYE, WCF na NSSF. Vile vile hakikisha unafanya ulinganifu (reconciliation) kati ya mshahara ulioneshwa kwenye hesabu zako pamoja na zile ambazo ulifanya marejesho (return) za PAYE kwenye mfumo wa TRA (Taxpayer’s portal). Kwa mjibu wa kifungu namba 7 (2) sheria ya kodi ya mapato, 2004 kile apatacho mfanyakazi toka kwenye ajira yake inatakiwa kulipia kodi ikiwa mshahara wake unaanzia Tshs 270,000.
5. Mali zisizohamishika zinazomilikiwa na shule/chuo.
Kuna mali kama majengo, viwanja, samani, komputa na vinginevyo vinavyomilikiwa na shule/chuo, hakikisha taarifa zake ziwe ktk mpangilio wa wazi ujulikanao kama rejista ya mali zisizohamishika. Kuna baadhi ya uongozi wa shule/chuo wanapenda kuwatumia fundi John ktk ujenzi wa majengo au samani za shule/chuo ambao hawatoi risiti za EFD hupelekea kuwa vigumu kupata thamani ya mali hizo. Kama thamani ya majengo au mali zingine hazifahamiki, shule/chuo inaweza kufanya uthamini (valuation) ili kupata thamani ya sasa ya mali hizo ambayo itaioneshwa kwenye hesabu za shule/chuo.
6. Kodi ya zuio (Withholding tax)
Kama kuna watoa huduma uliwalipa kwa mwaka wa fedha 2024, mfano wa huduma ni kama ukaguzi (audit), ushauri wa kodi, ushauri wa kisheria, ulinzi, kampuni za usafi, ukarabati na matengenezo na huduma nyingine hakikisha kwenye malipo hayo unakata 5% kabla ya VAT. Hii ni kwa mjibu wa kifungu namba 83 sheria ya kodi ya mapato sambamba na aya ya 4 ya kipengele kikuu (First schedule).
7. Gharama ya usimamizi (Management fees)
Katika shughuli za usimamizi wa shule/chuo kuna wale wakurugenzi (Non-executive directors) ambao hawashiriki ktk shughuli za kila siku za uendeshaji wa shule/chuo, endapo shule inaamua kuwalipa gharama za usimamizi wa baadhi ya shuguli za kuutendaji hakikisha umelipia kodi ya zuio ambayo ni 15% ya gharama ya malipo hayo.
Kama hutoichukulia hiyo changamoto kwa ukubwa muda sio mrefu shule/chuo itaingia kwenye matatizo dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na taasisi ambazo zimekukopesha fedha ambayo inaweza pelekea biashara ikafungwa.
BY THE WAY….Unaweza kutuchagua kuwa wakaguzi (auditors) wako wa hesabu za shule/chuo kwa mwaka wa fedha 2024. Ili kupata huduma hii tuma ujumbe sasa hivi kwenda 0752187434 au [email protected].
Tuma ujumbe huo ndani ya saa 24 ili uwekwe kwenye mpango kazi wa wateja wetu, nje ya muda huo tutakuwa tumefunga dirisha la kupokea wateja wapya.