Ewe Raia mwema wa Tanzania usidanganyike, tii Sheria bila shuruti, zingatia wito na uamuzi wa Mahakama na Wananchi kwa hekima na busara

tuliza mihemko kidogo,
wacha ghadhabu na kuendelea kujichanganya zaid....

yale ambayo yako chini ya serikali za wanadamu ambazo ni Neema na Baraka za Mungu yanafanyika kwa kiwango hicho vizuri sana...

yale ambayo Mwenyezi Mungu kaishaamua mwenyewe kama wanadamu hatuwez kuingilia kwa namna yoyote ile au hata kulaumu japo yanaumiza mtima...

Jambo la muhimu na la maana zaid ni ushirikiano na sio ushirikina. ikiwa una taarifa za kihalifu popote nchini, tafadhali usisite kutoa taarifa panapohusika ili atua stahiki zichukuliwe na haki itendeke ๐Ÿ’
 
Vipi kuhusu hao wa Noah nyeusi na gari zenye namba bandia wanaokamata watu bila kuwapeleka Polisi?
nadhani uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea, utakapo kamililika taarifa rasmi ya kina itatolewa kwa umma ๐Ÿ’
 
Kwani wale wafanya biashara wa mahenge walivyowakamata waliwafanya nini,waliwapeleka picnic au kutembea ๐Ÿ˜„
Mwanangu we polisi uione hivyo hivyo juu juu

Ova
hebu elezea vizur mrangi,
wewe uliyoiona kwa chini chini kabisaa ili tujue kwa undrani zaid ๐Ÿ’
 
nadhani uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea, utakapo kamililika taarifa rasmi ya kina itatolewa kwa umma ๐Ÿ’
kwahiyo kesi ya wizi wa mahindi wa ngedere amepewa ngedere huyo huyo ajichunguze,
sijui nikuite nani
 
H7jawahi kusikia mtu ambaye ni mhalifu sugu mwisho wa siku inatoka amri ya kumtoa uhai
Unajuwa hiyo huwa inafanyikaga

Ova
sifahamu mrangi, na hiyo hazikubaliki licha ya kuhatarisha uhai wa wananchi hata wa wahusika wanaofanya kazi za kiusalama katika vyombo vya ulinzi na usalama ๐Ÿ’
 
kwahiyo kesi ya wizi wa mahindi wa ngedere amepewa ngedere huyo huyo ajichunguze,
sijui nikuite nani
bila mihemko,
hebu toa mawazo mapya au fikra mbdala dhidi ya namna ya kushughulika na jambo hilo tafadhali gentleman ๐Ÿ’
 
lakini kiuhalisia hakuna zaid ya Mungu Mwenyezi Mwenyewe kuamua hatma ya kila mja wake humu duniani..
Pale unapokosa hoja unaleta vihoja...jibu swali, Je kuna taasisi yoyote inayoruhusiwa kuuwa mtu yoyote asiyekuwa na silaha zaidi ya mdomo wake!?
 
Maelezo yako yana'make sense' kama mambo yote yako sawa/yanafanywa kwa mujibu wa Katiba/sheria. Shida ni kwamba kuna tofauti kati ya 1) kutii Katiba/sheria na utaratibu wote ambao sheria imeuweka katika kufanya mambo mbalimbali na 2) kutii maagizo yanayokiuka sheria au utaratibu wa kufanya mambo mbalimbali uliowekwa na sheria. Watu wengi wanalalamikia hili la 2. Labda ungetusaidia kufafanua zaidi ili kutupa mwanga. Sijui hapa unasemaje?
 
Wewe ni mshirikina sio bure mkuu. kiwango cha kujipendekeza kimepitiliza
 
ni muhimu sana kufahamu kwamba katiba ndiyo sheria mama wa sheria, kanuni na taratibu nyingine zote zinazohusu sheria,

anaesimamia sheria anapaswa kujua hilo apende asipende lakini pia anae paswa kutekeleza anapaswa kufahamu hilo pia apende asipende....

nikiri tu,
saa zingine ni katika uelewa na ufahamu wa mambo haya ndipo changamoto hutokea kwa pande zote mbili au upande moja mjuaji kuliko mwingine na hapo mabishano yanayozaa kiburi na ujeuri huibuka miongoni mwa wahusika na ndipo haya yote yanayoendelea yanaweza kutokea...

na kidogo zaid kuna weza kua na kutokuwajibika ipasavyo au kulegalega kidogo kwa wahusika katika kutekeleza majukumu na kuleta majawabu ya haki kwa umma. nadhani vyombo husika vimeskia hisia za wananchi na kwakweli kuna kazi kubwa inaendelea kubadili hali hiyo,

muhimu zaid,
ni wananchi kujizuia kurubuniwa kifikra na kushawishiwa na wanasiasa au wanaharakati uchwara kutokutii sheria bila shuruti...

tuwe wazalendo tafadhali kwa kutii bila shuruti sheria na katiba ya nchi yetu ๐Ÿ’
 
Wewe ni mshirikina sio bure mkuu. kiwango cha kujipendekeza kimepitiliza
gentleman,
mimi siwezi kubabaika na hisia au huruma za mtu yeyote kwenye masuala muhimu sana ya sheria na katiba ya nchi...

watu wengi mno wamepoteza haki zao kwasabb ya hisia na huruma za kufuata mkumbo mitandaoni, lakini ikifika kwenye vyombo vya kutolea haki unakuta kumbe hakuna ushahidi ni ushabiki, hisia na huruma tu za mitandaoni,

bure kabisa,
toka huko nyuma kwa keyboard njoo field, sawa?๐Ÿ’
 
Pale unapokosa hoja unaleta vihoja...jibu swali, Je kuna taasisi yoyote inayoruhusiwa kuuwa mtu yoyote asiyekuwa na silaha zaidi ya mdomo wake!?
kama ipo popote duniani itaje, na itasaidia nini sasa...

unaniuliza kisichokuwepo ambacho pia unajua hakuna ni kupoteza wakati...

embu toa nafasi kwa wenye maswali ya maana wapate majibu kutoka kwa kiongozi wao, alaaa๐Ÿ’
 
1. Kuna kutofautiana kati ya watu ambao wako upande wa chama tawala na wale wa upinzani.
2. Wapinzani wanachukuliwa kama wanasiasa wanaorubuni watu au wanaotaka fujo au wasiotaka mambo mazuri yatokee hapa nchini. Binafsi huwa naliona hili kama exaggeration. Wapinzani ninaowafahamu mimi huwa wanataka mambo yafanywe kwa kufuata Katiba/sheria.
3. Shida ni kwamba watu walio wengi hawawezi kuvumilia hoja kinzani. X anaweza kuwa na 'wazo zuri' (good point/idea) na Y akawa na wazo 'zuri zaidi' (better point/idea).
4. Sasa mvutano unaweza kujitokeza X kutaka jambo hilo lifanyike kwa 'kiwango cha kuwa zuri' na Y kutaka lifanyike kwa 'kiwango cha kuwa zuri' zaidi'.
5. Na baadhi ya watu hawaoni tofauti, badala yake ni kuona kwamba Y anataka kupotosha umma na kuna propaganda nyingi kuhusu tofauti ya mitazamo hii.
 
maelezo yako, maoni na mtazamo wako baadhi uko sahihi na baadhi yafaa ufadanuzi zaid ila siyo mabaya kiujumla...

unajua ikifikia mahali wanasiasa au hawa wanaoitwa wapinzani wakabadilika na wakaja na mawazo mapya na fikra mbdala dhidi ya yanayo lalamikiwa tunaweza kupiga hatua kubwa mbele na kwa haraka sana....

hii ya kiongozi kulalamika kwa hisia na tuhuma za kusadikika na mwananchi kuchochewa ili aone huruma haiwezi kuleta mabadiliko kijamii, kisiasa au kiuchumi ๐Ÿ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ