Ewe Raia mwema wa Tanzania usidanganyike, tii Sheria bila shuruti, zingatia wito na uamuzi wa Mahakama na Wananchi kwa hekima na busara

Ewe Raia mwema wa Tanzania usidanganyike, tii Sheria bila shuruti, zingatia wito na uamuzi wa Mahakama na Wananchi kwa hekima na busara

Ni uzalendo wa maana sana kuitikia wito wa dola, kutii maelekezo, ilani au amri za vyombo vya ulinzi na usalama bila ukaidi, ubishi wala kiburi kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi..

Jitahidi sana uwe Raia mwema siku zote, muungwana, mzalendo, mtiifu kwa sheria na katiba ya nchi, na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ikihitajika, kamwe usikubali kuchochewa, kudanyanywa au kuhamasishwa na viongozi wa kisiasa wenye viburi na jeuri kwa dola, na wenye dhamira ya kuhatarisha au kuvuruga umoja, amani na utulivu wa wengine.

Usikubali kufundishwa ukaidi, jeuri na kiburi kwa Dola. daima, kumbuka akili za kuambiwa, ni vizuri ukanchanganya na zako.

Daima jitenge dhidi ya ukaidi kwa dola, kwasababu utaumia na utapata tabu sana ukiwa mwenyewe pekeyako na utalazimishwa kutii na kuheshimu katiba kwa shuruti na nguvu inayoweza kukusababishia madhara kimwili au kiakili.

kutii Sheria bila shuruti ndio mpango mzima wa amani na salama yako..🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Hata kukamatwa kisheria kunaleta amani ila kukamatwa na kupelekwa kusikojulikana ndo penye shida kunakomfundisha mtu ujeuri. Usuwalaumu raia.
 
kwan kuna Tatizo gentleman kusema ukweli? 🐒
Mimi sikushangai hata kidogo kwani ni wajibu kwa shetani mdogo kumtetea shetani mkubwa. Kesho ukiamka jitazame vizuri kwenye kioo...huo unaouona mbele yako ndio uovu katika sura ya binadamu!
 
kwa assessment yangu binafsi,
mimi si muovu, licha ya huenda nikawa na mapungufu na madhaifu ya kibinadamu kama wengine, hata hivyo ni Mungu Mwenyezi pekee ananijua vyema. Namshukuru sana kwa Neema na Baraka zake alizonijaalia hata nikawa hivi nilivyo...

wananchi jimboni wananipenda sana, wananiamini sana na kwa uhakika wananikubali sana kwa bidii ya kazi ile ambayo wamenipatia niwafanyie kwa maslahi mapana ya jimbo zima la uchaguzi...

hata hivyo,
wananiamini na kumkubali zaid kipenz cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan ambae ni kiongozi na mkuu wa nchi yetu Tanzania.
kwa hakika tupo mikono salama, chini ya mama huyu...

jambo la mwisho,
simulizi yako ya kubuni inasisimia na kusikitisha sana, ama kwahakika unaweza kutunga stori zenye kuhuzunisha namna hiyo,

lakini ungekua ni halisi,
hakuna mpenda haki angethubutu kukaa kimya kwa unyama na uovu na ukatiki wa aina hiyo....

ila kwakua ni simulizi ni sawa tu ilisha kama ilivyo isha na binafsi sina hata cha kuongeza, kwasabb humu nchini hapajawahi kutokea kisa kama hicho tangu uhuru popote nchini Tanzania 🐒
Simulizi ya kubuni?? Kuwa serious ndugu kwenye masuala ya hatari Kama haya. Nikieleza kisa chote hapa naamini kwamba nitapewa Kesi nzito ya uchochezi au nitabambikwa Kesi ya kichwa, kwa sababu baadhi ya wahusika wa mkasa huo wengine bado ni Wafanyakazi wa huko. Sitaki kuhatarisha vibarua na maisha ya mtu yoyote yule.
 
huo ni upotoshaji,

vyombo imara na vya kisasa vya ulinzi na usalama nchini vipo kwaajili ya kulinda umoja, amani, utulivu na usalama wa watu, mali zao na makazi ya wananchi na waTanzania wote...

ni upotoshaji na uchochezi chuki dhaifu na usio na madhara yoyote dhidi ya vyombo hivi muhimu vya kiuchunguzi na kiusalama..

nitoe wito kwa raia mwema yeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kuwatia nguvuni wahalifu wa aina mbalimbali ili nchi yetu iendelee kufurahia matunda ya Amani yaliyopo 🐒
Wahalifu waliouwa kule Simiyu unataka taatifa zao zikatolewe wapi? Wanaoteka watu waripotiwe wapi? Polisi wanapotoa taarifa zenye utata waripotiwe wapi? Au taarifa za ubadhirifu mkubwa unaofanywa na viongozi wa umma umeona wapi zikifanyiwa kazi? Wewe ni mnufaika wa mfumo ovu unata kushawishi jamii inayonyimwa haki ikae kwa kutulia kama wanyama wanaoswagwa kuelekezwa machinjioni.
 
Simulizi ya kubuni?? Kuwa serious ndugu kwenye masuala ya hatari Kama haya. Nikieleza kisa chote hapa naamini kwamba nitapewa Kesi nzito ya uchochezi au nitabambikwa Kesi ya kichwa, kwa sababu baadhi ya wahusika wa mkasa huo wengine bado ni Wafanyakazi wa huko. Sitaki kuhatarisha vibarua na maisha ya mtu yoyote yule.
sasa wewe inatofauti gani na yule mtu,

mathalani mko kwenye usafiri wa umma, kisha unaona kibaka anadokoa kwenye mkoba wa abiria mwenzako,

halafu wewe umekaa kimya unaangalia tu, kisha kibaka kashuka na kutokomea kusikojulikana,

ndipo baada ya abiria kugundua kaibiwa ndipo unajitokeza na kimbelembele chako eti uliona tukio zima tangu kibaka anafungua begi hadi anaiba alichoiba...

sasa zawadi yako si makofi tu 🐒
 
Wahalifu waliouwa kule Simiyu unataka taatifa zao zikatolewe wapi? Wanaoteka watu waripotiwe wapi? Polisi wanapotoa taarifa zenye utata waripotiwe wapi? Au taarifa za ubadhirifu mkubwa unaofanywa na viongozi wa umma umeona wapi zikifanyiwa kazi? Wewe ni mnufaika wa mfumo ovu unata kushawishi jamii inayonyimwa haki ikae kwa kutulia kama wanyama wanaoswagwa kuelekezwa machinjioni.
kwahiyo,
unakuja kuripoti hapa ili uonewe huruma right?

sasa kama hutaki kuripoti uhalifu wowote panapohusika, baki na imani potofu na ushirikina wako karipoti unapo amini utasaidika...

hata hivyo,
vyombo husika vya uchunguzi, ulinzi na usalama viko tayari kushirikiana na wananchi wowote wenye taarifa sahihi za wahalifu katika kudhibiti uhalifu na kushughulika na masuala yote ya dhuluma za haki za kibinadamu popote nchini kwa maslahi mapana ya amani, umoja na utulivu wa wananchi 🐒
 
Mimi sikushangai hata kidogo kwani ni wajibu kwa shetani mdogo kumtetea shetani mkubwa. Kesho ukiamka jitazame vizuri kwenye kioo...huo unaouona mbele yako ndio uovu katika sura ya binadamu!
kwamba unamuhubiria nabii au unatoa ushuhuda gentleman 🤣
 
Hata kukamatwa kisheria kunaleta amani ila kukamatwa na kupelekwa kusikojulikana ndo penye shida kunakomfundisha mtu ujeuri. Usuwalaumu raia.
ume make sense kirahisi kwa lugha nyepesi 👊💪
 
maoni na mtazamo potofu ni sehemu ya mjadala huu muhimu,

Jambo la maana zaid ni kuepuka imani potofu za kishirikina kwenye masuala muhimu ya kitaifa na yenye maslahi mapana ya waTanzania wote 🐒
Kuna washirikina zaidi ya hawa watekaji na wauaji?
 
Back
Top Bottom