EWURA inatia aibu kufungia vituo vya mafuta visivyouza

EWURA inatia aibu kufungia vituo vya mafuta visivyouza

ni mbinu tu za kubrand ..biashara ..nauzia benzi, Bmw, Vwagon,Nissan n.k
Wenye Toyota pita hivi...in rose voice!

halafu anakuja mtu kukufungia kwa kosa gani? Wafanyabiashara wangijitambua tusingepelekeshwa Wakileta barua ya kufunga tunawaburuza mahakan wakathibitishe ...dharula yangu ya kutokufungua inaniwajiibishaje kunifungia biashara, kwa sheria gani!

Ndiyo maaana wakifunga wanapiga blaa blaa tu ...mbona zimefunguliwa zinauza kamakawaida?
NI KWASABABU KUTOKUFUNGUA SIYO KOSA NI HAKI YA MNYABIASHARA cha msingi havunji sheria ya usalama na ubora
Msitutese bana...tunetegemeana acheni dharau...nyie madon wa mafuta..
 
Hao wenye vituo vya mafuta ni haohao waliopo ktk system acha wauane
 
Habari Wananchi

Ifahamike kwamba Siyo jukumu la serikali kulazimisha kuuza!

Ewura kama mdhibiti mkuu anatakiwa afanye kazi kisomi siyo kikoloni!

Ifahamike Ewura hana shea yoyote kwenye mitaji ya wafanyabiashara ya mafuta:

  • Wakati mfanyabiashara anatafta mtaji huwa peke yake,
  • Anapotafta eneo la kujenga huwa peke yake
  • Anapodaiwa mikopo huwa peke yake,
  • Anapojenga kituo gharama huwa juu yake
  • Anapoomba kibari Ewura hutozwa fedha ili kupatiwa kibali
  • Mafuta yakishuka huwa ni hasara kwa mfanyabiashara mwenyewe

Kwa maana hiyo mfanyabiashara huyu mamlaka zinamtaka kuzingatia hali ya usalama na kuuza mafuta katika hali ya usalama lakini hawapaswi kabisa kumpangia wa kuwauzia!

Mfanyabiashara anayo haki ya kuamua Baadhi ya magari asiyauzie mafuta hiyo ni haki yake na hapaswi kushurutishwa

Mfanyabiashara anaweza kuamua kuuzia magari mfano aina Benz na BMW tu na akagoma kuuzia gari za toyota ni haki yake hapaswi kuuadhibiwa

Anaweza kataa kuuza kwa kuomboleza kifo cha ndugu yake ni haki yake hapaswi kushurutishwa

Anaweza kuamua kujipa likizo na wafanyakazi na hutakiwi kumshurutisha

Mtu ambaye hajawahi kuuza hata mihogo kisa kapewa mamlaka ya kudhibiti anaamua kufungia watu waliowekeza akili, pesa na nguvu! hii siyo sawa kabisa!

Ewura ni mdhibiti lakini ni katika hali ya ubora na usalama na siyo kupangia watu wakati na muda wa kuuza!

Ewura walipaswa kujiuliza wanakosea wapi kwanini wafanya biashara wafiche mafuta,

Kama wanaona ni raha kuuza basi wauze wao kila wilaya wajenge kituo cha mafuta wauze kwa bei rahisi kubalance soko,

Hebu tuwaze kidogo tu kama kweli Ewura wanawapenda sana wananchi kwanini bei inapanda kiholeka?

Kama Ewura wanajali wananchi kwanini hawaruhusu vibali vya vituo vya gesi barabara za mikoani? kwanini huwa wanagoma kutoa leseni za kujenga vituo vingi vya gesi CNG ukiachilia hivi viwili/vitatu dar nzima?

Kwanini vituo vya CNG vipo limited nani anayetoa hayo maelekezo kuzuia visijengwe kwa faida gani?

Badala ya kufungia hivi vituo vinavyojitafta kimaisha soko huria, Yangekuwa maoni yangu ningelifukuza team nzima ya Ewura ije akili mpya ambayo itadhibiti kwa Akili na siyo kizamani namna hii ambako kunaleta mwanya wa rushwa!

Nani atakuwa salama kama kituo kinaweza fungwa kwasababu kimejipa off? VIPI Kama watendaji wa Ewura wakiamua kuitumia hiyo kama fimbo kuomba rushwa na wasipopewa wanakifunga kwa KAULI ZA NAMNA HIYO?

Ni akili ya hovyo sana kufungia Wachuuzi wakati wenye matatizo ni EWURA WENYEWE
Hapo lazima wafanya biashara wajifunze jinsi kuongeza mauzo kwenye kituo cha mafuta.

 
Back
Top Bottom