View attachment 2739153
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (EWURA) Dkt. James Andilile amesema hayo na kufafanua kuwa Petrol iliyopo inatosheleza matumizi ya siku 19 na Dizeli ipo ya kutumika kwa siku 18.
Aidha, EWURA imevifungia kwa miezi 6 Vituo 2 vya Mafuta ambavyo ni Camel Oil na Mtemba vilivyopo Msamvu na Turiani Morogoro huku Kituo GBP cha Ipuli Tabora kikifungiwa kwa muda usiojulikana baada ya kutuhumiwa kuficha Mafuta.
Takwimu za Mahitaji ya Mafuta Nchini zinaonesha Tanzania inatumia Lita Milioni 4.5 za Petroli kwa siku na Dizeli Lita Milioni 6.6 kwa siku.