EWURA yatangaza kupanda kwa bei ya mafuta leo Septemba 6, 2023

Lakin mkuu huoni kua mteja hapangi bei siku zote.
Alaf ni soko la dunia limepanda asa tutalazimisha kununua bei ya zaman akati wao wamepandisha bei
Au hizi bei ni kwetu tuh tz
Mkuu swali ni kwamba kwanini yaadimike kukiwa na taarifa ya kupanda bei?
 
Mkuu swali ni kwamba kwanini yaadimike kukiwa na taarifa ya kupanda bei?

Ni suala la biashara mkuu wauza mafuta wao ni wafanyabiashara kama wengine wanataka faida.pia kitu kikipanda bei dunian kwa wao lazima wacheze kiakili bila ivo ni hasara na hakuna mtu anayependa hasara
Hata wewe ungekua kwenye position hio ungefanya ivo
 
Ifahamike mkurugenzi wa UWURA alisema mafuta yapo ya kutumia kwa siku 19 zijazo.

Chakushangaza wamepandisha bei za mafuta kwa maelezo kuwa soko la mafuta limekuwa juu dunia nzima.

Swali kwanini wamepandisha bei ya mafuta ambayo yalikuwa yamenunuliwa kwa matumizi ya siku 19 zijazo kabla hata ya soko la mafuta halijaongeza? FaizaFoxy The Boss tusaidieni majibu
 
Mpaka unauwezo wa kuagiza hiyo chuma basi msamiati wa mafuta kupanda bei hauwezi kukuathiri wala hutoona tofauti na awali.
hakika mkuu, nilitoa mfano mkubwa.. kuna ile hali ya mtu unakuta anaotea chuma flani.. alafu ana fail maintain.. unaona hadi gari nyingi bongo services mbaya.. mtu anekuwa na hiyo chuma ana uchumi imara sana
 
Shida ni kwamba hao hao wenye hizo kampuni ndo hao hao wako uko sirikalini.kwahiyo usitegemee jambo latofauti.
 
Walivyokuwa wanapondwa vichwa walikuja na kauli hatufai ni dikteta wanasiasa wakala vyao nasi tukaimba nao pambio.

Wacha watunishe mifuko yao wenda akili zitatukaa sawa.
 

Ewura si ipo chini ya wizara ya Nishati ambayo sasa Biteko ndo waziri wake au sivyo? Ndo maana nasema Biteko kapewa jumba bovu.
 
Shida ni kwamba hao hao wenye hizo kampuni ndo hao hao wako uko sirikalini.kwahiyo usitegemee jambo latofauti.
Mimi nakubali kila mfumo unachangamoto zake lakini ni bora uwe na waletaji mafuta 10 kuliko mmoja. Hawa wafanya biashara sio wote wanapendana ushindani utakuwepo. Shida mtu mmoja alete mafuta halafu auzie wengine wote na zaidi uwapangie bei elekezi ndio shida. Chukuwa mfano umeenda sokoni unataka nyanya lakini wauzaji wote wa nyanya wananunua kwa mtu mmoja hivi kweli hata uzunguke soko zima unadhani utapata unafuu? tuache soko pana halafu to regulate tu.
 
Kama dar Bei ndo Hii,
Mlioko kagera na kigoma msipouziwa Lita elfu4 Sijui[emoji848]
Mkuu jambo usilojua huko Mikoani kuanzia Kakonko, Biharamuro, Geita, Kagera(mpakani) bei ya mafuta ipo chini sana 70% ya bei ya DSM.
Nadhani hata mpakani na Zambia bei chini kuliko Dar.
 
Kwani wewe ulikatazwa kununuwa na kuleta mafuta ya bei poa?

Unangoja nini badala ya porojo?
Hizo Cartels zilizokaa hapo juu napenyea wapi..
Na wala tatizo sio bei, tatizo ni kuficha ili bei ipande.

To be fair, hii sio Sawa kabisa.
 
Kwanin mafuta yafichwe?

Manake Kuna usimamizi mbovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…