Yapo mambo mengi yanayoweza kumsababisha mwanaume aliyeoa kutaka kumrudia ex-GF. Mojawapo inawezekana mwanaume akang'amua baada ya kuoa kuwa alifanya makosa makubwa sana kuoa huyo aliyeoa. Mimi mwenyewe yalinitokea, niliacha GF tuliyekuwa tunaelewana sana nikaoa mwingine ambaye hapo kabla alikuwa ex wangu pia, kwa hiyo aliporudi nikaona 'awali ni awali hakuna awali mbovu'. Kumbe wakati mwingine 'awali mbovu' zipo, nikagundua baadae kuwa nilichemsha vibaya. Huyu ex wangu alishaolewa na kwa mujibu wa yale ambayo huwa ananiambia tunapoonana, ana maisha matamu sana na mumewe, maelewano 100%. Kutokana na ukaribu ambao tunao, anafahamu jinsi nilivyochemsha maana tumeshayaongea mara nyingi, lakini huwa anasema tu ananionea huruma na ananiombea, hatujawahi kumegana tena hata siku moja tangu nilipooa. Mara nyingi huwa ananikumbuka tu ananipigia simu kunijulia hali, kuna wakati akinipigia husema amehisi tu kuwa niko na tatizo, na ajabu mara zote inapotokea hivyo huwa ni kweli nakuwa na tatizo. Hadi najiuliza inakuwaje shida yangu yeye anahisi kitu kabla sijamwambia! Kwa kweli nam-miss sana, na hata tunapoonana huwa anasema hivyohivyo kwangu lakini siku zote huwa yuko makini kumalizia kwa kusema kuwa ni bahati mbaya hana zaidi cha kufanya zaidi ya kuniliwaza kwa maneno tu na company za siku mojamoja. Kwa hiyo wewe uliyeuliza swali usimshangae huyo bwana.